CHADEMA yasitisha maandamano-Arusha

CHADEMA yasitisha maandamano-Arusha

Polisi wamefanikiwa kudhibiti huu uhuni uliopangwa kufanywa na LEMA. huu ni ushindi dhidi ya uonevu unyanyasaji, ukabaji, uporaji na kila aina ya dhuluma wanaofanyiwa raia wema na hawa waandamanaji.
 
Uamuzi wa busara sana CDM !

Ninaamini haya maandamano yalikuwa halali na yangekuwa ya amani ila ninadhani Polisi ya CCM wangetumia nguvu kubwa mno kutawanya hayo maandamano na kuleta vurugu kubwa na probably ingeweza hata kusababaisha vifo na wangetupotezea focus kabisa na si ajabu wangepata sababu nzuri za kuahirisha uchaguzi wa jpili.......

PolisiCCM walikuwa wameshajipanga kufanya huo uahalifu. Mmepiga mkwara, wamekusanya hasira zao na nguvu kuwaumiza wanaCDM halafu mwishoni kabisa mkasema tumeahirisha, mihemko yao na silaha walizoandaa na hasira zao zimebaki zinahang !. Ninaamini wamesikitika sana kukosa opportunity hiyo ya kufanya uhalifu na kusingizia CDM. On the surface itaonekana kama CDM imegwaya lakini CDM imewapiga Polisi + CCM bao la nguvu sana !

Sasa tuweke nguvu zetu zote kwenye uchaguzi wa jpili.....Hongera sana CDM kwa uamuzi wa busara !

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA)
H/SE NO 8.NHC STREET
NGARENARO
www.Chadema.or.tz
TAARIFA KWA UMMA
Tunachukua fursa hii kuujulisha umma wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuwa maandamano yetu ya amani yaliyokuwa yafanyike Feb 5 yameahirishwa hadi hapo tutakapotangaza tena,
Hata hivyo tunawashukuru sana umma wa Arusha kwa utayari wao wa kupinga Ukandamizaji,dhuluma,na ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu.Tunauhakikishia umma kuwa CHADEMA tutaendelea kuwa msitari mbele katika mapambano haya hadi kieleweke.Tunauhakikishia umma wa sombetini na Arusha na Tanzania kwa ujumla kuwa vikosi vyetu vya B 52,Qx Mapambano,Mandela scorpion,Guerila 40,El Che889,Lenin 34PH,na Mama Haki,vimekamilisha maandalizi kabambe kwa ajili ya Sombetini ili kulinda ushindi wetu ambao ni wa 95%+.Kamwe hatutavumilia hujuma yoyote kutoka kwa yeyote.
CHADEMA tupo imara sana,tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu

Nanyaro EJ
Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Arusha mjini
 
tuandamane, tusiandamane ile kata inakwenda chadema..
Mkuu hili liko wazi na ccm wanajua sasa hivi wanaandaa mbinu chafu za kuvuruga kama walivofanikiwa kwa kata zile zingine uchaguzi ukaarishwa lakini bado wakapigwa chini
 
Mnatishia kujamba wakati mna tumbo la kuhara mtaaibika kwasasa hamna mazezeta tena chuga
 
Polisi wamefanikiwa kudhibiti huu uhuni uliopangwa kufanywa na LEMA. huu ni ushindi dhidi ya uonevu unyanyasaji, ukabaji, uporaji na kila aina ya dhuluma wanaofanyiwa raia wema na hawa waandamanaji.

vijana wa unga Ltd, esso, Sokon wani, matejoo,ngarenaro,kijenge ,watakuwa wamekasirika sana, polisi wamewatibulia dili lao
 
Kwa watu tuliopo Arusha tunajionea umbulula wa hili jeshi la polisi, maana leo kila kona ya jiji wamepaki Defender zisizo pungua mbili na magari ya maji ya kuwasha mawili na hapo ni katikati ya jiji. Kwenye kata yenyewe ya Sombetini ndo usiseme mitaa yote utafikiri ni makambi ya Feed-force jinsi askari walivyojazana na bunduki zao.

Swali:
Je Chadema Arusha ikiamua kutangaza maandamano kila week polisi si itafilisika?
 
Mkuu Msuki naomba kutofautiana na wewe katika hili. Kwanza,ki-nadharia napinga hatua ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya amani iwe kwa CCM, Chadema, CUF or whatever party or socio-political group. Si kweli kuwa eti Chadema wakiandamana ni chanzo cha fujo na uporaji kwani matukio haya hutokea popote utakapotokea mkusanyiko wa watu. Vibaka kumbuka ni opportunists, mwizi hana itikadi isipokuwa wizi. Pili napinga hii dhana kuwa uchumi wa Arusha unashushwa na maandamano ya Chadema. Hili haliingii akilini; iweje maandamano ya siku moja yakashusha uchumi wa jiji zima? Mimi namuunga mkono Mheshimiwa Lowassa lakini kwenye hili nasema mnawaonea Chadema bure.

Tuandamane kudai uboreshwaji wa usafiri wa reli. Hili ndilo lenye manufaa kwa umma.
 
Lema unatishia kujamba wakati unaarisha utahaibika ndugu Arusha kwasasa imekuchoka
 
hayo maandamano haramu ya lema na wahuni wenzake yamepigwa marufuku na jeshi la polisi, ucha upotoshaji

Lazima utakuwa ulizaliwa chooni wewe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mnatishia kujamba wakati mna tumbo la kuhara mtaaibika kwasasa hamna mazezeta tena chuga

Naamini upo Arusha, ccm kwa Sombetini sijui mtaficha wapi nyuso zenu, kumbuka matokeo ya kata nne Arusha Mwigulu alikutwa KIA kukwepa aibu. Sijui kama bado yupo na yule msukule wa kutengenezwa.

Cc: aminangalo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Magamba aka mizigo wanawashwa kweli na kamanda Lema......sasa tunangojea jimbo la kalenga na Chalinze muone mshikeshike wake...
 
Sijawahi kuunga mkono maandamano sijui ni kwanini Lema hataki kubadilika.Maandamano mpaka leo hayajawahi kumwondoa Meya lakini watu wasiokuwa nahatia walikufa.
 
Kwa watu tuliopo Arusha tunajionea umbulula wa hili jeshi la polisi, maana leo kila kona ya jiji wamepaki Defender zisizo pungua mbili na magari ya maji ya kuwasha mawili na hapo ni katikati ya jiji. Kwenye kata yenyewe ya Sombetini ndo usiseme mitaa yote utafikiri ni makambi ya Feed-force jinsi askari walivyojazana na bunduki zao.

Swali:
Je Chadema Arusha ikiamua kutangaza maandamano kila week polisi si itafilisika?

Kweli akili zako umeshikiwa na bwana LEMA, unapoona polisi wanafanya kazi ya kudhibiti fujo mnazozisababisha, jua fika kuwa ni hela za kodi zinatumika, kwahiyo usifurahie maandamano ya LEMA ukadhani unawakomoa Polisi au serikali, la! gharama zote ni sisi walipa kodi tunalipa!
 
Baada ya kutangaza maandamano na wafuasi wake maana tunajua hawana wanachama, serikali yayapiga stop maandamano hayo yenye lengo lilofunikwa la kupora mali za raia.

Tumekuwa tukishuhudia kila yanapotokea maandamano; wapo watu wanaopata hasara kubwa kwa kuporwa na waandamanaji, kupoteza mali n.k. Kikubwa kinachotokea ni uporaji hasa maeneo yafuatayo; bar, hotelini, maduka, vibandani, wapo pia wanaoporwa mikoba, pochi, walet, simu na vitu vingine vya thamani na waandamanaji ndio maana wanajitokeza kwa wingi maana ni siku yao ya kutengeneza

kama chadema wameshaona dalili za kushindwa huo uchaguzi ni vema wakajipanga upya maana bado kuna chaguz kibao zinakuja. Yanini kutumia vurugu kama timu ambayo imeshafungwa inavuruga mchezo?

Na kama chadema wanaamini askari wengi wanawaunga mkono kwanini wasiheshimu kazi yao ya uaskari?

Nakushukuru kwa habari mkuu,
Itakuwa vizuri jumatatu kama utatupa habari ya sombetini?

5-0
 
Ndio maana nawapongeza sana CDM kwa kuahirisha.....

Hawa polisi walijipanga kupiga watu na wangewaumiza sana watu, hata wangeweza kusababisha vifo....Sasa wamebaki na maslaha yao na hasira zao.....watakuwa wamechukia mno kukosa nafasi ya kuumiza watu !

Kuwapiga kwenye sanduku la kura tu ndio dawa yao stahiki na hili wataliona jpili !

Back
Top Bottom