Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.
Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.
Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.
Source:Mwananchi Jumatatu
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?.....
Big up CDM the earlier the better! Madereva waende mafunzo sio kununua leseni maana watakufa kabla ya 2015. Vilevile wafundishwe jinsi ya kufanya service ili vyombo vidumu beyond 2015.....
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe ametangaza mkakati wa Uchaguzi mkuu wa 2015 na moja ya mkakati huo ni kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa lengo la kuwafikia wananchi na kueneza elimu ya uraia.Pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu ambazo zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Mbowe aliyasema hayo mjini Hanang jana wakati akiwa anazungumza na viongozi wa chama na wadau wakuu wa CDM mjini hapa.
Mbowe alisema wameanza mkakati wa kuhakikisha chama kinawafikia wananchi kila mahali.Kiongozi huyo machachari amesema lengo kubwa ni kutaka kusikiliza matatizo ya wananchi na hata kule ambako kuna shida ya usafiri basi kwa pikipiki chama kitafika.
Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na Ruzuku ya chama pamoja na ufadhili kutoka kwa wanachama na marafiki wa chama chake walioko nje ya nchi.Huku mikakati yote hii ikiwa inasimamiwa na yeye mwenyewe chini ya uratibu wa Katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa.
Source:Mwananchi Jumatatu.......
Ni jambo zuri, ila ingefaa hizo Pikipiki zingepelekwa haswa vijijini watu wakafanye kazi huko mjini watu ni waelewa sasa hazina haja sana ni mtazamo tu!......
safi sana, ila nilitaka kujua operation sangara imeishia wapi? make tuliambiwa kipindi fulani ilisimamishwa kupisha ile tume ya wakina Nchimbi, na baada ya hapo ingeendelea lakini hadi leo kimya, vipi kulikoni?....
Nafurahi sana nikiona moja ya maoni ya wanachama yanafanyiwa kazi......