Umati mkubwa wa wananchi uliofurika katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA Kata ya Nkungi Jimbo la Iramba Mashariki leo umesababisha shughuli zote kusimama kwa zaidi ya saa tatu.
Mkutano huo ulihutubiwa na viongozi kadhaa wa kitaifa na mkoa wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Mwita Mwikabe Waitara na Kamanda maarufu wa Chadema katika Jimbo hilo George Gunda.
Akizungumza katika mkutano huo Kamanda George alishambulia CCM kwa umaskini wa wananchi na sera mbovu za huduma ya Afya.
Kamanda George pia alilaani CCM kutukana matusi viongozi wa Chadema wakati walipohutubia jimboni humo.
Kamanda George ambaye ni mwiba kwa CCM na amekuwa akiwatia sana ujasiri vijana wa jimbo hilo aliwataka wananchi wajiandae kuing'oa CCM katika chaguzi zote zijazo wakianzia na Serikali za Mitaa.
Naye Mwita Waitara aliyekuwa mgeni Rasmi ameendelea kuzungumzia umuhimu wa wananchi kujitambua na kuikataa CCM huku akifurahishwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza.
Waitara pia alizungumzia umuhimu wa wananchi kuunganisha nguvu katika suala la Katiba mpya na kuunga mkono Rasimu ya Tume ya Warioba ambapo umati mkubwa ulipiga kelele kwamba unataka Serikali Tatu.
Baadaye mamia ya wananchi wamechukua kadi mpya za Chadema huku wengine wengi wakirudisha kadi za CCM.
Kati ya waliorudisha kadi ni vijana zaidi ya 20 waliopewa kadi za CCM wiki mbili tu zilizopita na Katibu Mkuu wa CCM alipotembelea Kata hiyo.