CHADEMA Yasambaratisha CCM Iramba Mashariki

CHADEMA Yasambaratisha CCM Iramba Mashariki

Mkuu Molemo,

CCM haikuwahi kuwepo Singida Mashariki. Hao watu uliowaona majuzi kwenye mkutano wa Jangili Kinana na Mzee wa Mekako na Diprosoni walimwagwa kwa mabasi ya Mtei kutoka kila kona ya Singida, Dodoma, Manyara...

Siku hiyo nilikuwa natoka Singida kuelekea Dar nimepanda basi la ABC. Acha kabisa.

Asante sana mkuu SEBM kwa Taarifa yako.
 
Last edited by a moderator:
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kushabikia magamba coz ndio waliotia umasikini.
 
Leo molemo ana raha ya ajabu moyoni mwake, pamoja dr slaa na mbowe. Ndio mana wanashusha threds nyingi nyingi kukisifia chama
Namuona kamamda joji akipokea pesa zilizotolewa na Kinana na Nape ili ahamie ccm,watanzania kaeni chonjo hela zile bilioni 200 huenda ndio zinawatia kiburi kuzunguka nchi nzima na kushawishi mjiunge ccm ,chukueni mkalipie ada na kumalizia nyumbs zenu ala!,
Namsifu mnyiramba huyu chukua kadi na pesa kisha rudi zizini,jenga chama,
ila ninachowasihi watani zangu Mwigullu akija,pandeni gari mwende mkutanoni mwombeni chenji ya Rada alizopewa mgawane
 
mnajipa matumaini wa2 wanashangaa chopa nyie ooh!! ccm imevunjika

Haya ,Dau la mnyonge haliendi josho!, ngoja daftari liboreshwe,huku tuliko m/ kiti ccm ameuza eneo lililotengwa kuzikia ,mtoto umuleavyo ndivyo akuavyo,watz watatoa adhabu kali!
 
Leo chadema wanasherekea mafanikio ya kazi yao waliyohangaika nayo mda mrefu bila mafanikio.rest in peace mama zitto

mkuu wahi kuwaona madaktari utakufa kwa kijiba cha roho. Halo halo haloooo.....!!!!
 
Kwa hali niliyoiona nkungi kwenye mkutano wa CHADEMA lazima tukubali CCM wamekalia kuti kavu.
 
Kwa hali niliyoiona nkungi kwenye mkutano wa CHADEMA lazima tukubali CCM wamekalia kuti kavu.

Ulea leane kaka! Jana nilikuwepo Nkungi hivi unaweza kufananisha na Ule mkutano wa Kinana? Tuwe wakweli na tuache ushabiki pembeni!

Kwa hakika Jana palikuwa patupu na wewe uwe mkweli kabisa ndugu yangu! Nilikuja nikitokea Shelui nilipitia Msingi, Gumanga, Nduguti hadi Nkungi lakini CDM Jana mumeaibika sana!

Nitaweka Picha ili umati ujionee wenyewe! Kati ya Kinana na mbwembwe zenu za Jana!
 
Kata mti - panda miti. wataelewa tu.
 
Umati mkubwa wa wananchi uliofurika katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA Kata ya Nkungi Jimbo la Iramba Mashariki leo umesababisha shughuli zote kusimama kwa zaidi ya saa tatu.

Mkutano huo ulihutubiwa na viongozi kadhaa wa kitaifa na mkoa wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Mwita Mwikabe Waitara na Kamanda maarufu wa Chadema katika Jimbo hilo George Gunda.

Akizungumza katika mkutano huo Kamanda George alishambulia CCM kwa umaskini wa wananchi na sera mbovu za huduma ya Afya.

Kamanda George pia alilaani CCM kutukana matusi viongozi wa Chadema wakati walipohutubia jimboni humo.

Kamanda George ambaye ni mwiba kwa CCM na amekuwa akiwatia sana ujasiri vijana wa jimbo hilo aliwataka wananchi wajiandae kuing'oa CCM katika chaguzi zote zijazo wakianzia na Serikali za Mitaa.

Naye Mwita Waitara aliyekuwa mgeni Rasmi ameendelea kuzungumzia umuhimu wa wananchi kujitambua na kuikataa CCM huku akifurahishwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza.

Waitara pia alizungumzia umuhimu wa wananchi kuunganisha nguvu katika suala la Katiba mpya na kuunga mkono Rasimu ya Tume ya Warioba ambapo umati mkubwa ulipiga kelele kwamba unataka Serikali Tatu.

Baadaye mamia ya wananchi wamechukua kadi mpya za Chadema huku wengine wengi wakirudisha kadi za CCM.

Kati ya waliorudisha kadi ni vijana zaidi ya 20 waliopewa kadi za CCM wiki mbili tu zilizopita na Katibu Mkuu wa CCM alipotembelea Kata hiyo.

weka picha haraka
 
Hivi angekufa mama yake ni kiongozi yoyote wq Chadema kutoka kaskazini mikutano ya chama ingeendelea.

mbowe alishasema hata yeye akifa watu wasilie bali wazidishe mapambano mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom