Jamani kuna tetesi ya mtu muhimu mmoja wa chadema aliekuwa akifuatilia database in making comparison of what has been published by NEC has been lost since yesterday.
A case has been reported to Oysterbay police station.
Mwenye zaidi ajalizie
Nawakilisha
Hii ni hatari sana, vitendo hivyo vilifanyika wakati wa ujima. Kwa vile Tanzania ya leo tumeisha hama kwenye enzi za ujima nashauri washauri wa serikali na viongozi wa serikali wachukue tahadhali.
Serikali iliyoendeshwa kwa mabavu enzi hizo iliweza tu kwa vile wananchi wengi walikuwa gizani.
sasa hawapo tena gizani, mtu yeyote makini akiangalia na kusikiliza maelezo ya Lewis Makame na tume yake analojibu kwamba lipo tatizo kubwa ktk tume hiyo ambayo haiko kwa manufaa ya taifa bali kwa kulinda masilahi ya watu kadhaa. Makame anasitahili kustafishwa kwa manufaa ya nchi kwani ni vitendo vya tume yake vinavyoelekea kutuletea maafa. Tunajua si rahisi kwa Makame kuwa mkweli na muwazi kwani naye kula yake ipo hapo,lakini pamoja na kula kwake kusitusababishie balaa.
Endapo kuna mtu amechukuliwa na kufichwa na vyombo vya dola kwa vile ana siri nyeti za chama fulani yote yanasababishwa na demokrasia finyu ambayo inasababishwa na tume hiyo ambayo imefumba sauti ya watu kwa kuamua kufanya wanayoyaona. Watanzania walinyamanza na kulifumbia macho hilo la Makame sasa wasiwasi wangu ni pale vyombo vya dola vitakapo anza kuingilia wananchi kama vile ni wahaini, Ningeshauri vyombo husika kwa namna yoyote kama vina husika na kupotea kwa mtu huyo, vijue kuwa Tanzania ya sasa siyo ile ya ujima watu wanauelewa mkubwa
mabavu na vitisho visiwe sehemu ya utendaji wao kwa jamii ambayo hivi sasa imeelevuka.
Nina imani kiutendaji usalama wa taifa kwa hali na uvumba watajitahidi kujua siri zao zinavuja na kumfikia Dr.Slaa namna gani, na ikibidi watataka kujua miongoni mwao nani wanavujisha siri hizo hivyo
targets wakwanza watakuwa watu wanao kisiwa kuwa karibu na Slaa na hasa watu wa Information Technology.Lakini mimi ningeshauri endapo hilo lopo wawe makini kwani wasi waongezee wananchi vidonda ambavyo wamepewa tayari na hali ya kutoheshimu demokrasia nchini.
Nchi nyingi ambazo vurugu na maafa yametokea zimesababishwa na vyombo na serikali kuendesha nchi kimabavu hali wakisahau kuwa hata hiyo jeuri wanayotumia ni nguvu ya wananchi. Mwisho washauri na viongozi wa serikali tunawaomba kuwa makini kwani upepo umeisha badilika wajaribu kwenda na wakati.