CHADEMA yapongezwa kwa kujenga msikiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yapongezwa kwa kujenga msikiti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 9, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Taasisi ya Amani ya Kiislam (IFP) imekipongeza chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kwa kujenga msikiti katika kijiji cha Nshara mkoani Kilimanjaro, msikiti ambao umejengwa kutokana na michango ya wabunge wa chama hicho.

  Mkurugenzi wa taasisi hiyo Sheikh Sadik Godigodi amesema kitendo kilichofanywa na chama hicho kinafaa kuungwa mkono vyama na watu wengine kwani wameisaidia jamii. Sheikh Godigodi amesema wabunge wa chama hicho walichanga zaidi ya shilingi milioni 30 kiwango ambacho ni zaidi ya sh milioni 16 zilizokuwa zikihitajika.

  Pia Sheikh Godigodi aliitaka serikali kutokupuuza maoni yaliyowasilishwa Ikulu na Chadema kuhusiana na mchakato wa katiba mpya kwani Chadema ni chama kikuu cha upinzani nchini na kinachopendwa na watanzania wengi.

  SOURCE: MTANZANIA uk. 5
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  CHADEMA ni chama cha watanzania wote-wakristo, waislam, wapagani, wahindu nk!! nami nawapongeza pia!!
   
 3. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wanaongoza kwa taasisi Tanzania.
   
 4. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Si vibaya kumuombea mtu mabaya,ila mara mia ungekufa wewe abaki mchawi wa JK Sheik yahya
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  wewe siku zote una roho ya kiuaji tu. hufikirii amani hata kidogo. unataka kuleta ubo haramu hapa bongo?
   
 6. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ni vibaya kumuombea mtu mabaya,ila mara mia ungekufa wewe abaki mchawi wa JK Sheik yahya
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  kwani bila OIC hamuabudu? tunachohitaji tanzania ni uhuru wa kuabudu, siyo ionekane kundi moja lina nguvu kuliko lingine, ndo madhara ya boko haramu haya
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kumbe makanisa nayo yana sauti bungeni???
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Maneno ya Biblia na Quran yaweza kutumika vizuri au vibaya, itategemeana na Muhusika anataka nini? kwa mfano aya/mstari huu kuuleta hapa nia yako ilikuwa ni kukidhi haja yako ambayo ni kuonyesha kupinga kila linalofanywa na CHADEMA hata kama viongozi wako wa dini wamegundua ni zuri
   
 10. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  waislamu hawahitaji msikiti wanazo za kuwatosha! Wanachohitaji waislamu ni mikakati ya kuwanasua na umaskini, shule, hospitali, ajira, ubaguzi wa kidini, mfumo kristo tz, nk. Hivyo chadema wasijidanganye kwa kuwajengea waislamu vijisikiti ili wapate sapoti ya waislamu ktk uchaguzi wa 2015!!

  Wakati wa kudanganywa na vijikofia, kanga, fedha nk. Umepitwa na wakati na waislamu wako macho na hila za vyama vya siasa bali waislamu wa tz wanajipanga imara kwa kuchagua chama madhubuti kitakacho kuja na sera safi mbele ya waislamu na ndipo waislamu watakapo ingia mkataba na hicho chama ikiwa wanataka kura ya waislamu basi wawe tayari kukubali masharti yao!!!

  Kinyume chake waislamu watapokea kanga, vikofia au fedha zenu lakini kura ng,oo
   
 11. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Jana umeliponda Nipashe,Tz Daima na leo Mtanzania la Fisadi mwenzenu haya basi waambie Al nuur na lle gazeti waandike mazuri uyatakayo
   
 12. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  "Umesema CDM wasijidanganye kuwajengea Waislam Misikiti ili wapigiwe kura 2015" Swali langu kwako wewe MDINI je hivi unajua Waislamu ni % ngapi ya waTz 45 million? Acha kuropoka na kung'ang'ana na Udini utawafikisha pabaya sana
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  kweli ubinadamu kazi, ukimsapoti atakwambia unajipendekeza, ukimuacha asimame mwenyewe atakuita mbaguzi aaaaaaaarghhhhhhhhhhhhh!!!!1

  halafu wengine wanajidai hawajaridhika utafikiri wao ndo wanaswali kwenye huo msikiti...
  utafikiri walitoka kwenda kuwapiga tafu wenzao kujenga msikiti.............................
  utafikiri walipeleka mifuuko ya saruji kuchangia ujenzi..................

  wakazi wa nshara walijua wanahitaji nini, wakaomba wenye mapenzi mema wawachangie, wakachanga nyie huku mnapondaponda mnajua shida ya kuswali walokuwa wakiipata? mnajua walikuwa wakiswali kwenye mazingira gani? mbona hamkujitokeza kuwachangia hata nondo moja?
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hapo nilipo RED ndio ilikuwa mzizi wa makala yake na kutaka kutupa ujumbe hadhwira.

  Masjid Al Chadema.

   
 15. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hivi mdini ndio nini? Na hiyo dini ni ipi?
   
 16. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Nimeamini kweli kuwa usijieleze kwa yeyote kwa kuwa anayekupenda hahitaji kujeleza kwako, na asiyekupenda hata kama ukijieleza namna gani hatakuamini kamwe
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa takwimu zisizo rasmi. Katika Tanganyika inakadiriwa waislam na wakristo ni 50% each. Na ukisema kwa Tanzania waislam wanafika 54% na wakristo ni 46%.

  Kumbuka unaposema wakristo kuna wakatoliki na wengine (protestant) ambao ni 58%.

  Hizo ni takwimu zisizo sahihi kwa sababu TZ bado haijawa na takwimu rasmi za watu since hakuna sensa iliyofanyika miaka 5 iliyopita.

   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Swadaka Allahu L'adhim.

  Hakika umeweka kitu mujarabu kabisa. Na kwa kuwamaliza kabisa watu hao wana macho ila hawaoni, wanamasikio hawasikii, wana pua lakini hawanusi. Na siku zote hao ndio watakao pata adhabu kali sana.

  Mola atuepushilie mbali na adhabu hizo na kuwa miongoni mwa wanafiki.

   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  NI SAHIHI KABISA.

  Kwanza kosa lake ni kukihusianisha CDM na ukristo, kitu ambacho si kweli na havina uhusiana.

  Pili mwisilamu aliyefundishwa vizuri, ameamriwa kuwaheshimu na kuishi vizuri na wakristo na wayahudi, kwa kuwa quruan inawataja kuwa ni wa kwanza kupewa vitabu vya Mungu, uislamu ulifuata baadae.(SIKUMBUKI NI QURUAN NGAPI) ila najua mtatujuza

  Sasa huku kupingana waisalamu wanakutoa wapi enye FF NA MS boko haramu wa Tanzania?
   
 20. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu,ila wapo wale wenye fikra mgando watakuambia chadema ni chama cha wakristo,tena wakatoliki!
   
Loading...