Chadema yapingana rasmi na CCM kuhamishia makao makuu Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yapingana rasmi na CCM kuhamishia makao makuu Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 8, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Moja ya sera rasmi mpya za Chadema zilizotangazwa hivi karibuni ni kutohamishia makao makuu ya mji mkuu wa kiserikali na kibiashara kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa mambo ya nje wa chama hicho Bw. John Mnyika

  Alisema mbali na azma yao ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia Makao Makuu kwenda Dodoma majengo yote ya serikali Dodoma yatageuzwa kuwa vyuo vikuu vya elimu na vyuo vya ufundi ili jiji hilo liwe kitovu cha elimu nchini.

  ......ni kitu gani kilichokifanya Chama cha Mapinduzi CCM miaka ya sabini kiwe na kusudio la kuhamia Dodoma je hilo kusudio kwa sasa bado lipo na je kwa nini Chadema hawataki makao makuu ya nchi yawe Dodoma, tujiulize ni gharama au ni kutaka tu kutofautiana
   
 2. N

  Nanu JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  katika presentation yao si walisema ni nini tatizo sasa kwanini usiweke thread iliyokamilika?
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Mkuu kweli mimi sijui tatizo ndiyo maana nimesema tujiulize
   
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi CHADEMA wanadhani they are the only 'brains' in this country? John Mnyika aende Lagos na Abuja aone jinsi ambavyo kutenganisha Lagos kuwa mji wa biashara na Abuja kuwa mji wa Serikali kulivyoisaidia Nigeria. Hivi sasa jiji la Dar es Salaam karibu litafika Kibaha. Serikali ikihamia Dodoma kutakuwa na idadi kubwa ya watu watakaohama hapa jijini kuifuata Serikali na kupunguza msongamano uliopo.

  Tanzania bado inayo mapori mengi mno yanayosubiri kufyekwa ambako kunaweza kuwa 'vitovu vya elimu' wanavyotaka Chadema. Kwanza wanafunzi wanahitaji sehemu tulivu kwa nini iwe mjini Dodoma ambako tayari kuna vurugu?
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Sasa mkuu huoni kuwa pia wanafunzi wanahitaji huduma muhimu ambazo hazitapatikana huko mapolini nafikiri labda Chadema imeona kuhamia Dodoma italigharimu taifa mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kusaidia secta zingine
   
 6. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Miaka ya Seventies ndio Dodoma ilipatiwa hadhi ya kuwa makao makuu ya serikali, kama ni maendeleo tungeyaona just after ten years, na hii mambo imekaa sana kisiasa make mpaka sasa huwezi kabisa kuona kama Dodoma ni makao makuu ya serikali, we angalia tu miundo mbinu ya hayo makao makuu ya serikali, utafikiri ni kijiji underdevelopment scheme, huwezi jua kabisa hapa ni makao makuu ya serikali, i was in Dodoma for 4yrs in ninties, lakini nimekuwa nikipita hapo several times and i have never noticed any change, yaani badala ya kusonga mbele mimi binafsi naona retro-progressing, it is shame!!

  lazima tunaposema kuwa tunaingia kwenye kitu fulani basi vitendo viwepo, kama ni makao makuu ya serikali mbona mpaka sasa Raisi na serikali yake wapo Dar, sasa Dodoma kuwa makao makuu inatoka wapi--------Nenda Lagos kama utakuta serikali ipo pale, serikali yote ilihamia Abuja baada ya kutangaza kuhamisha makao makuu ya serikali ya Nigeria. Tanzania tunabaki kubwabwaja tu wakati tunajua kuwa sio kweli.

  Open up your scurs man, scrutch your bull if not brain
   
 7. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na Chadema ktk hili in the sense that uhamisho umekua politicised tu. Hakuna uhamisho,all are still in Dar. Yanini kuwarubuni wananchi kwamba tunahama wakati wote tupo hapo hapo mjini? Ni heri kusema ukweli kwamba hatuhami ng'o kuliko kuwadanganya wananchi. Nani hajawahi kuona msululu wa mashangingi to and from Dodoma kila kukicha? Wengine wamepewa mpaka nyumba huko dodoma lakini wapi kila kukicha ni safari tu DSM to Dodoma, Dodoma to Dsm.
  Wakiwa Dom wanasema karibu nitarudi home(eti ndio DSM). Uwongo na wizi mtupu! Heri yenu Chadema mmeliona hili.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kumsikia mtoto wa mkulima akisema ofisi yake itakuwa imehamia Dodoma kabla ya 2010 au nakosea hivi na yeye bado yuko Dar anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa au na yeye hataki kuikosa per diem
   
 9. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huduma muhimu anazohitaji mwanafunzi ni chakula na malazi. Vifaa vingine vinavyohitajika kwa ajili ya masomo yake vinapaswa kutayarishwa na kushughulikiwa na Chuo chenyewe. Isitoshe, huko maporini kutawavuta na wafanyabiashara ndogo ndogo wahamie huko kupeleka huduma ndogo ndogo zitakazohitajika.

  Kila jambo jema lina gharama zake. Kwa maana hiyo ni lazima kuangalia faida zitakazotokana na Serikali kuhamia Dodoma kuliko kuangalia gharama. Fedha nyingi zinapotea kwa matumizi mabovu ya Serikali, ingelikuwa bora Chadema wakaelekeza nguvu zao katika kudhibiti matumizi mabaya ya Serikali kuliko kukomalia matumizi ambayo yana faida kwa nchi kwa ujumla.

  Mtoto wa Mkulima atahamia Dodoma just give him time. Suala la per diem kwake halina nafasi. Angelikuwa anajali mambo hayo ya per diem wala account yake isingelikuwa na Sh. 25 millioni tu!
   
 10. m

  mjukuu2009 Member

  #10
  Feb 8, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndio CHADEMA,wameonyesha kuchoshwa na siasa za CCM zisizokuwa na masilai kitaifa,tokea tuko wadogo tunasikia serikali inaamia Dodoma lakini mpaka sasa nina miaka 30 akuna kilichofanyika,zaidi zaidi ni hawa viongozi wa CCM tuna banana nao B-Bar kila siku,ukiwa umeagiza nyama yako akija yeye anapewa kabla yako ata kama amechelewa,kwenye ATM wanawatukana na kuwafukuzisha kazi ndugu zetu walinzi wa ATM kisa kuwambia wakae pembeni ili kupisha wateja wengine.
  Tunateseka sana na hawa viongozi wa CCM kwani wao wamekuwa ni miungu watu siku hizi,kiongozi yoyote wa CCM atakama ameteuliwa jana anajiona watu wote wana mfaamu kwaiyo anafanya anavyotaka.
  Serikali ya CCM imeshindwa kuiga mfano wa NIGERIA katika kutenganisha mji wa Abuja na Lagos,wangeamia mji mwingine kama Dodoma/Moro mji huo ungeendelea kwa kasi sana ila awataki wanataka kukaa Dar es salaam tu kila kitu Dar es salaam.

   
 11. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 966
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Kinachofanya watu wagune ni kwanini huo mchakato umichukua miaka mingi hivyo kama hiyo azma ipo?Kimsingi naona azma hiyo imeshakufa kwani wengi wawaliohamua huo mpango wameshastaafu, Ikumbukwe Nigeria walituma wataalamu wao kuja kujifunza Tanzania ni jinsi gani wangehamisha makao yao makuu kutoka Lagos kwenda Abuja, Ni garama, ni garama na ni mzigo mkubwa saana kwa serekali, ukipiga mahesabu kipindi cha bunge wizara au taasisi moja inatumia kiasi gani cha pesa inatia huzuni tena saana, Kama hiyo nia ilikuwepo wengekuwa wameshahamia tema siku nyingi kinachotolewa ni visingizio tu, na wasingeruhusu balozi za nje ziendelee kujenga makazi ya kudumu DSM wangeshauri na wao wakajenge dodoma
   
 12. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You've said it "Tanzania tunabaki kubwabwaja tu" na kuendekeza ushabiki badala ya kuangalia mustakabali wa nchi yetu. Kazi yetu ni kubwabwaja tu. It is high time tukaacha kubwabwaja na kuanza utekelezaji wa mambo yaliyo na faida kwa taifa regardless time factor. it is never too late when it comes to something productive.

  Ni kitu rahisi sana kutelekeza huu uhamiaji Dodoma. Kesho Rais Kikwete akiamka usingizini na kusema jamani twendeni tuhamie Dodoma utaona hakuna Waziri wala mfagiaji wa wizara atakayebaki Dar. Kule Dodoma zilishajengwa nyumba za Mawaziri etc etc ndizo wanazoishi wakihudhuria Bunge na yapo majengo ambayo yanaweza kabisa kuwa ofisi bila hata kuingia gharama za kujenga majengo mapya. It can be done, let those concerned play their part.
   
 13. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwenye nyekundu hapo u r quite right. Especially akiwa karudi zake toka Dom utamtambua. Hapo umkute kaona kabinti kamekaa kwa pembeni jamaa ndio litajishaua utafikiri CEO wa kampuni fulani kubwa mjini hapa kumbe wapi,mla hela za walala hoi tu. Wakakae dodoma huko watuachie Dar tupumzike bana!
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu,nimepapenda sana.Keep it up CHADEMA
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,080
  Likes Received: 7,649
  Trophy Points: 280
  What took you guys so long?
   
 16. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #16
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wazo la kwenda Dodoma siyo baya kabisa,ucheleweshwaji wake ni viongozi wenu wanataka kukaa karibu na wafanyabiashara"kaa karibu na pesa ikuzoee",waende Dodoma upesi tumeshoshwa na foleni na ving'ora vyao na wasipohama ndoa yao na wafanyabiashara itakomaa na SFO watawaumbua kila kukicha!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,683
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Hadithi ya kuamia Dodoma ni ya miaka mingi mpaka imenikera.
  Kila mwaka wanatenga pesa za kujenga makao makuu kwa miongo karibu minne sasa na hakuna anayekuwa tayari kuamia Dodoma.
  Mpaka leo kuanzia mkuu wa kaya Dar-es-Salaam ndio makao yao makuu. Wizara zote bado ziko Dar na kila kukicha wanatudanganya kuwa Dodoma ndio makao yao makuu.
  Ni kweli wazo la kwanza la JKN lilikuwa zuri lakini warithi wake hawana nia hiyo bali wamebaki na ngonjera. Sasa si afadhali Chadema wameona tofauti?
  Kwani ni lazima Chadema waone kama sisiemu inavyoona? Big up Chadema!
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,080
  Likes Received: 7,649
  Trophy Points: 280
  Wa-Nigeria walipotaka kuhamisha mji mkuu wao kutoka Lagos kwenda Abuja, walikuja Tanzania kujifunza.Wakakopi makabrasha muhimu yote.

  Wenzetu wamemaliza, sisi tuliowafundisha hatujafanya lolote la muhimu.

  Na hii habari ya kusema wazo la Nyerere lilikuwa zuri siielewi.Wazo zuri wakati halijawa thought out to the end?

  Kuhamisha mji mkuu ni shughuli expensive, kwa nini nchi masikini yenye matatizo lukuki iingie katika project nyingine ya kuhamisha mji? As if hatuna matatizo ya kutosha.

  Nyerere alichemka, hakukuwa na ulazima wa kuhamisha mji. Dar ni mji uliokua organically, there is nothing better than that. Waarabu na hela zao zote wanashindwa ku attract watu kwenda kuishi Dubai kwenye migorofa mitupu, huwezi ku force mji kuhama bila kuwa na plan kabambe.
   
 19. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watanzania wakati mwingine huwa tunajitakia gharama za bure hizo hela na hiyo mipango na huo muda toka 70s wangejenga miundombinu mizuri dar wakaipanua hadi Bagamoyo Kibaha Kisarawe na hizo ofisi za serikali wakazitoa pale katikati peleka bagamoyo huko katikati ya dar iwe biashara tu
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama hii nayo ni sera ya CHADEMA, basi CCM wataendelea kutawala mpaka wachoke maana the alternative ni Utaahira. Walio na busara wanasema 'Kama huna cha kusema ni bora ukafunga domo lako kuliko ukalifungua halafu kila mtu akautambua umbumbu wako'. CHADEMA inakoelekea sasa ni kubaya.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...