SPANERBOY UDZUNGWA
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 622
- 125
Hongera kaka kazi njema kwani elimu ya uraia inatakiwa kuenezwa kwa wingi hasa vijijini. Ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima ifike wakati CCM ipumzike ili hata kama itarudi baadae irudi na mawazo mapya kwani kwa hivi sasa imefilisika kisera na kiutendaji. Hebu jiulize inakuwaje taifa lenye polisi na usalama wa taifa then wakina masogage wanapita airport na unga wa bilion 6.8 na kuenda kukamatiwa sauzi? Hivi kweli kunauwajibikaji hapa si rushwa tu imejaa na imekisiri kwa kiasi kikubwa.
Swali la kujiuliza ni je Taifa letu litakaa liendelee kweli taifa ambalo tunaishi kwa kudra za mwenyezi mungu kwa maana hata kulinda mipaka yetu tumeshindwa. Wageni wanajiingilia tu watakavyo wanaishi kwenye nchi yetu bila vibali wanajifanyia watakavyo na vyombo vya ulizi na usalama vipo vimekaa tu havijui kinachoendelea kazi yao kubwa ni kupambana na wapinzani kwa maslahi ya CCM si kupambana na dawa za kulevya na kulinda usalama wa nchi na wananchi wake kama ilivyopaswa kuwa. Nahisi ipo siku tutakuja tuangamizwe wote ni bora sasa CCM ipumzike ijipange upya kwa kuwa nadhani kwa hali ilivyo sasa hawajui nini uwajibu wao kwa taifa.
Ndovu wanauawa maelfu kwa maelfu, madini yetu yanachotwa na wageni kama mchanga, elimu yetu ni mbovu walishaiua ili wapate kufanya biashara ya shule zao binafsi enzi za mwalimu ukifaulu kwenda shule ya secondari ya umma ulikuwa unaonekana kichwa lakini leo tunaogopa kuwapeleka watoto wetu huko kwa sababu elimu ya umma ilishachimbiwa kaburi na kuzikwa na CCM, Jeshi la polisi na usalama wataifa ambavyo zamani enzi za mwalimu vilisifika na hata watu wakasema tanzania ilikuwa ni nchi inayoongoza kwa upelelezi leo vimekuwa vyombo vya CCM vimeacha kazi ya kulinda raia na mali zao na usalama wa nchi. Leo tanzania imekuwa geti la kupitishia madawa ya kulevya tena hayapiti kwa njia za panya bali yanapita Airport ni aibu kubwa taifa kama tanzania. Sasa taifa letu ni taifa ambalo halina maadili tena hasa kwa viongozi nchi inanuka rushwa kila kona, vitendo vya uonevu na unyanyasaji wa raia pamoja na dhuluma kwa wananchi vimekisiri. Ndio maana tunasema ni heri CCM ikapumzika maanake imelewa madaraka haijitambui tena iko wapi na inaenda wapi.
Hongereni sana mnaoeneza elimu ya demokrasia hatimaye nchi yetu itaokoka kutoka katika makucha ya mkoloni mweusi.
Usahauri kwa vyama vya upizani ni kuwa vijenge kwanza msingi huku chini visikimbilie kwenye nafasi ya uraisi ni ngumu kufika huko kama hujajenga msingi imara huku chini vihakikishe vinaongeza madiwani na kushika uongozi wa hata baadhi ya halmashauri then vionyeshe uwezo wao wa kuongoza na nina imani vitaweza kuwashawishi wananchi walio wengi kuvichagua najua kunaugumu fulani maslani arusha CDM inamadiwani wengi ilipaswa kuongoza manispaa ya arusha lakini CCM haijawa tiari kuwapa mwanya lakini wasikate tamaa naamini kwenye uchakuguzi wa serekali za mitaa mwakani kama watashika maeneo mengi basi itakuwa na impact hata kwenye uchaguzi mkuu 2015 lakini wakichemsha hapo then 2015 tusitarajie miujiza bado CCM itaendelea kushika dola
2010 waliiba kura lakini 2015 tutalinda kura kwahiyo ccm lazima ing,oke hata baba mwanaasha analijua hilo . Baba mwanaasha ataamua kuiingiza nchi kwenye machafuko au ccm itoke madarakani dhamana hii yote ipo mikononi mwake.