Nimesoma maelezo yote hapo ya huyo msemaji wa jeshi, hakuna mahali popote amejibu hoja ya msingi ya CHADEMA kuhusu mchezo mchafu unaoendelea katika kambi za majeshi kwa askari wote kuamriwa kupeleka taarifa za vitambulisho vyao vya kupiga kura.
Huyo msemaji ametoa vitisho vitupu badala ya kujibu hoja. Jeshi sio vitisho bali jeshi ni kanuni, sheria na Utaratibu. Ni ujinga na ushamba mkubwa kwa karne hii na dunia ya sasa kuwa na jeshi linaloamini kutishia watu badala ya kujenga urafiki na mahusiano mema na raia na taasisi.
Kwa namna IGP na huyu msemaji wa Jeshi la JWTZ walivyoshindwa kutoa majibu ya msingi katika hoja nzito zilizotolewa kwao, inaashiria kabisa wamepanic sana hususani baada ya hicho kichafu walichokuwa wanakificha sasa kimeanza kuwa hadharani.