CHADEMA yamuumbua mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

Unafiki mtupu, watu wanakwenda kujifunza yeye anawawekea kauzibe haoni mjiwa wa MOSHI ulivyo safi? aende akamzuie vasco da gama kutumia fedha za umma kukodi wanamziki wakawaburudishe nyumba ndogo zao huko marekani na uingereza. mbona vasco dagama katumia ndege ya serikali kwenda kumnasua rizmoja huko uchina aliko kamatwa na madawa?

Mkuu hapo kwenye RED ebu anzisha thread juu ya habari hii tuichangie imenigusa sana, kumbe ujio wa wachina kwa wingi Nchi hii kuna siri kubwa nyuma ya pazia.
 
Kaika hili CDM hawasafishiki!

Siyo madiwani wa CDM tu ndio wanahusika; wapo mkurugenzi wa manispaa, watumishi wengine wa manispaa na madiwani wa CCM japo ni wachache. Lakini kuna ubaya gani madiwani kufanya ziara kama kuna fedha na ziara ina tija?
 
Mkuu hapo kwenye RED ebu anzisha thread juu ya habari hii tuichangie imenigusa sana, kumbe ujio wa wachina kwa wingi Nchi hii kuna siri kubwa nyuma ya pazia.
ULIKUWA HUJUI?? Habari ndio hiyo.kila mchuma janga hula na wa kwao.kashikwa na mzigo fedha zetu zinatumika kumnasua.
 
Siyo madiwani wa CDM tu ndio wanahusika; wapo mkurugenzi wa manispaa, watumishi wengine wa manispaa na madiwani wa CCM japo ni wachache. Lakini kuna ubaya gani madiwani kufanya ziara kama kuna fedha na ziara ina tija?
Kama wewe ni CDM wa kweli basi unijibu kama kuna uhalali wa kiongozi wa umma kufuja fedha na kodi za walalahoi.
 
CCM wanafiki sana. Huyo rais wao anayetangatanga dunia nzima na bakuli mkononi na kikundi cha watu 30+ analeta tija gani hapa nchini?

Sana sana anautangazia ulimwengu jinsi Watz tulivyo mafala.

**** ni wewe peke ako usitusemee sisi wengine wala kutuingiza kwny ufala wako,baki nao huko huko
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu kimemjibu mkuu wa mkoa Bwana Gamma katika mkutano ambao haujaonekana mkoani Kilimanjaro baada ya uchaguzi mkuu kwa kueleza kinaga ubaga kuhusu ziara ya madiwani kwenda mafunzoni nchini Rwanda.

Akitoa ufafanuzi hatua kwa hatua huku akishangiliwa na umati wa wananchi meya wa manispaa ya moshi MICHAEL JAFFARY alimtuhumu mkuu wa mkoa kwa unafiki na kufanya mambo aliyotumwa na CCM ili kuiharibu na kuichonganisha na wananchi CHADEMA mkoani huko,alimhakikishia mkuu wa mkoa kuwa hakuna ufisadi kwa kuwa safari yote inajulikana ofisi ya waziri mkuu,mkuu wa mkoa mwenyewe na kuwa haitafutwa na iko palepale.

Akafafanua kuwa hizo ni hasira za kufichuliwa ufisadi mkubwa katika miradi ya mabango ambapo manispaa ilikuwa inapata mil 70 nyingine zinaingia mifukoni mwa mafisadi,baada ya kuwabana sasa hivi mabango yanaingiza 400mil.

Akawataka UVCCM kuandamana kwa ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali yao kwa rais kukaa hoteli za dola 10000 na timu za watu 20 na zaidi.

Amewahakikishia wana Kilimanjaro kuwa CDM haiwezi kuwasaliti na kamwe wasidanganywe na CCM.

Walifanya ziara Japan kwa kodi za walipa kodi wa Japan na sasa imefikia mahali manispaa imeamua kwa makusudi ya maendeleo na usafi wa mji wa Moshi kwenda kujifunza kwa wenzao.

mh jafari naona unakufa na mzigo wako mpaka tone la mwisho la damu,tetea huo ufisadi lakini hii dhambi itkitesa chama kwa muda mrefu sana
 
Unafiki mwingine bwana hivi zile Semina elekezi za ngurudoto na St. Gaspa na safari za JK zilitumia shilingi ngapi na zilikuwa na jita gani kwa watanzania?
 
Meya huyo wa MOSHI ni kilaza ameshndwa kujenga hoja kutetea ni namna gani iwe sawa wao waweze kutumia mamilioni ya fedha kwenda kujifunza usafi?ameshndwa kuonesha michanganuo ya fedha hizo kutuaminisha wananchi tukubali upuuzi huo?ni kwanin wanaCDM wanashndw kujenga hoja wanahalalisha hoja zao kwa ujinga na ubadhirifu wanaofanza CCM?anataka kutuaminisha ufisad wakifanza CDM ni sawa 7bu kaka yao CCM wanafanza mkubw zaid yao?wanacdm co jambo la kushabikia hii ni fedheha kwa chama na watu wanaowaamini.Kweli nimeamini cdm xio kimbilio la wanyonge
 
CDM fikirieni nje ya box! For sure hayo maposho yatawatokea puani! Kwa nini msibadili by-laws katika manispaa ili kuyaondoa?

Is it really necessary kuwatuma madiwani wooooooote! Si waende wachache tu? You guys need to behave otherwise! Ili tofauti tuione bana...
 
Huyo mkuu wa mkoa aseme kuwa alitegemea hiyo safari ifanyweje?kwani hapa njia pekee ni kupunguza watu au kuwaleta wataalamu wa Kigali wakiwa na video napolicises zao za usafi miji waje wafundisha moshi.Ila kama alipiga chini project na hakuwa na mbadala kachemsha.Kwa moshi Mji unaoongoza kwa usafi TZ na wana sheria kali sana, usafi ni issue ya kila siadhani kama kuna diwani ambaye ambaye angekuwa tayari kosa wakati ana jukumu la kurudi simamia usafi katk kata yake.

Njia ya kuwaleta wataalamu au hata kupeleka madiwani wachache nighali zaidi.Kwani hao waliokwenda wangetumia hela karibu robo,na wakirudi walipwe posho kuwafundisha wengine ambao nao wangehitaji posho.Na hata kuleta wataalamu hata watatu tuu ni gharama kuwalipa na pia kuwalipa hao madiwani posho zao.Yoote haya pia haya gurantee mafanikio ya zoezi hilo.

Kwa hiyo idadi ya watu na hiyo hela kama ingetosha kuwapa na osho bado ni matumizi yasiyoogopesha kama mawizarani:

Million 200 si hela kama mnavyodhani.kwa watu wengi hivyo kwenda nje ya nchi.

-hela/watu =>Mil 200/57=3.5087719mil/per person

-mil 3.51 au 3,510,000/= 3,510,000/1600=$2,193.75/pp

-hela kwa siku kwa kila mtu. katika week(assuming 7 days)=> $2,193.75/pp/7=$313.393per person, per day.

Bei ya hotel yenye ubora Kigali ni around $200 per person per night. na inaweza zidi sana.Achilia mbali matumizi mengine,kama stationery,phone,internet, transport etc.Tz yenyewe hotel zinazidi $ 2,000 kwa siku,hata kama kitazidi ni kiasi kidogo ambacho mtu alistahili baki na kitu hata cha kuleta zawadi kwa familia.

Seems ni msukumo wa kisiasa kuliko akili.

Kwani viwango vya per diem vya serikali kuu kwa mtu akiwa nje ya nchi kwa ukanda wa africa mashariki na kati ni zipi?
 
Naomba mwenye otuba hii ya meya naiyomba aniwekee hapa jamani nataka kusikiliza hotuba nyingi sana za viongozi wa cdm kuliko bongo flv
 
Kama ni kwenda kujifunza usafi huko Rwanda, si madiwani wa Moshi wangewapeleka wafagizi wa barabara na wale watunza bustani za Moshi! maana haiingii akilini diwani kwenda kujifunza usafi kisha akirudi atakuwa ofisini kwake tu na watendaji wa moja kwa moja ni wengine! Peeeeople's power kwa hili boiling point ni zaid ya nyuzi joto 100! kuomba samahani unapokosea sio udhaifu ila ni uungwana, madiwani Moshi kuweni waungwana!
 
Meya huyo wa MOSHI ni kilaza ameshndwa kujenga hoja kutetea ni namna gani iwe sawa wao waweze kutumia mamilioni ya fedha kwenda kujifunza usafi?ameshndwa kuonesha michanganuo ya fedha hizo kutuaminisha wananchi tukubali upuuzi huo?ni kwanin wanaCDM wanashndw kujenga hoja wanahalalisha hoja zao kwa ujinga na ubadhirifu wanaofanza CCM?anataka kutuaminisha ufisad wakifanza CDM ni sawa 7bu kaka yao CCM wanafanza mkubw zaid yao?wanacdm co jambo la kushabikia hii ni fedheha kwa chama na watu wanaowaamini.Kweli nimeamini cdm xio kimbilio la wanyonge
Wewe ndio kilaza ulikuepo kwenye mkutano unajua alichosema kwa taarifa tu najua mnachafua Meya kwa sbabu ndio Mbunge mtarajiwa wa moshi mjini kuanzia 2015.Muulize mkuu wa mkoa kw nn anataka amilikishwe eneo la wazi,kw nn ana2mia gari ya serikali kufungua mataw ya ccm?kw nn anasema safari itagharimu milion 200 huku akijua sio kweli?kw nn alivyoandikiwa hyo barua hakujibu badala yake alikimbilia kwenye vyombo vya habari?muulize kwnn ofis ya waziri mkuu isiwe ya kwanza kufuta fungu la mafunzo kw madiwani wote nchi nzima?
 
Kama ni kwenda kujifunza usafi huko Rwanda, si madiwani wa Moshi wangewapeleka wafagizi wa barabara na wale watunza bustani za Moshi! maana haiingii akilini diwani kwenda kujifunza usafi kisha akirudi atakuwa ofisini kwake tu na watendaji wa moja kwa moja ni wengine! Peeeeople's power kwa hili boiling point ni zaid ya nyuzi joto 100! kuomba samahani unapokosea sio udhaifu ila ni uungwana, madiwani Moshi kuweni waungwana!
Unajua maana ya usafi wa mazingira nakuweka mji safi wewe ama unakurupuka tu bila sababu za msingi unajua hyo safar ilipangwa lini?unajua ziara ya mafunzo ni stahili ya madiwan wote nchi nzima na utaratibu upo waz.
 
Kwa hiyo kama ni utaratibu wa kutumia hovyo pesa za walipa kodi wa nchi hii ndio uhalalishwe! kama kawaida ni kama sheria sasa hizi kelele za chadema juu ya matumizi mabaya ya fedha za wananchi ni ya nini si waache maana ni kawaida nchi nzima! Sasa mbona huwa wanapigia kelele safari za kikwete nje ya nchi wao wanajua zilipangwa lini? CDM ni lazima wajipambanue na vyama vingine kwa utendaji wao kama wanataka tuamini kuwa wao ndio Mussa waliotumwa kuja kututoa utumwani Misri!
 
Nimesoma habari kama mara tatu lakini sijaona sehemu ambayo CHADEMA imemuumbua Mkuu wa Mkoa zaidi ya kuona tu kuwa Meya amejiumbua mwenyewe na wenzake waliotaka kufuja pesa za umma...

Huwezi kuona kwa kuwa macho bila ubongo hayafanyi kazi
Akafafanua kuwa hizo ni hasira za kufichuliwa ufisadi mkubwa katika miradi ya mabango ambapo manispaa ilikuwa inapata mil 70 nyingine zinaingia mifukoni mwa mafisadi,baada ya kuwabana sasa hivi mabango yanaingiza 400mil.

Bado huoni?

Sasa kama unaakili, utagundua kwamba, dili la 330m lilipoharibiwa, majombi wamekuwa na hasira na nia ya kutaka kuonesha kuwa hata na wao wanakula. Shida ni kwamba na wa kwao wamo, hiyo moja mbili ni kwamba, haikuwa siri mpaka bonge nyenye aseme amefichua.

Aibu yetu, aibu yenu?
 
Back
Top Bottom