CHADEMA yamuumbua mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yamuumbua mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, Sep 22, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuonyesha ukomavu wa hali ya juu kimemjibu mkuu wa mkoa Bwana Gamma katika mkutano ambao haujaonekana mkoani Kilimanjaro baada ya uchaguzi mkuu kwa kueleza kinaga ubaga kuhusu ziara ya madiwani kwenda mafunzoni nchini Rwanda.

  Akitoa ufafanuzi hatua kwa hatua huku akishangiliwa na umati wa wananchi meya wa manispaa ya moshi MICHAEL JAFFARY alimtuhumu mkuu wa mkoa kwa unafiki na kufanya mambo aliyotumwa na CCM ili kuiharibu na kuichonganisha na wananchi CHADEMA mkoani huko,alimhakikishia mkuu wa mkoa kuwa hakuna ufisadi kwa kuwa safari yote inajulikana ofisi ya waziri mkuu,mkuu wa mkoa mwenyewe na kuwa haitafutwa na iko palepale.

  Akafafanua kuwa hizo ni hasira za kufichuliwa ufisadi mkubwa katika miradi ya mabango ambapo manispaa ilikuwa inapata mil 70 nyingine zinaingia mifukoni mwa mafisadi,baada ya kuwabana sasa hivi mabango yanaingiza 400mil.

  Akawataka UVCCM kuandamana kwa ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali yao kwa rais kukaa hoteli za dola 10000 na timu za watu 20 na zaidi.

  Amewahakikishia wana Kilimanjaro kuwa CDM haiwezi kuwasaliti na kamwe wasidanganywe na CCM.

  Walifanya ziara Japan kwa kodi za walipa kodi wa Japan na sasa imefikia mahali manispaa imeamua kwa makusudi ya maendeleo na usafi wa mji wa Moshi kwenda kujifunza kwa wenzao.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM wanafiki sana. Huyo rais wao anayetangatanga dunia nzima na bakuli mkononi na kikundi cha watu 30+ analeta tija gani hapa nchini?

  Sana sana anautangazia ulimwengu jinsi Watz tulivyo mafala.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Umenena mkuu. Huyo rais wao kama kweli anaitakia mema nchi yetu angefanya jambo la tija iweapo angekwenda Uswisi akapiga kambi kule hadi mamlaka za kibenki za nchi hiyo zimpe majina ya mafisadi vigogo katika serikali yake waliowekewa mabilioni ya hela katika benki za huko.

  Ninachofahamu yeye mwenyewe anaweweseka kuhusu majina yaliyomo katika orodha hiyo.
   
 4. M

  Magesi JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika CHADEMA 2natisha kamanda James olle Millya amewafurahisha wananchi kwa hotuba yake iliyowaingia barabara.Kasoro iliyokuepo ni kitendo cha kadi zilizokua zinauzwa sh.1500 kuisha pia kamanda GODBLES LEMA hakuweza kuhudhuria kama ilivyopangwa kwn ameenda kushiriki katika kumuaga aliyekua baba wa mbunge wa Singida mashariki kamanda Tundu Lisu
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Eti mkuu wa mkoa anasema hela zikanunue madawati,hajaziona za rada,dowans,meremetasafari za rais,magari ya kifahari nk.
   
 6. commited

  commited JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  yap, nami nimefarijika sana hayo maelezo ya makamanda kupitia moshi-fm
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  RC huyo na yule wa Arusha wanafanana sana. Kama Pinda alivyosema wako ki-CCM zaidi na kwa kazi maalum. Kazi zao kubwa ni kwa ajili ya kuihujumu CHADEMA na kuumiza wananchi wa mikoa husika, yote mawili sambamba.

  Hawajui kufanya hivyo kunaiimarisha zaidi na hapo hapo CCM kuzidi kuchukiwa na wananchi. Wote pamoja na kikwete ni viongozi vipofu wanaoongoza chama kipofu - CCM

  Njama zao hazitafaulu na ukombozi utatimia mbele ya macho yao.
   
 8. MBWA HARUKI

  MBWA HARUKI Senior Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LILE LIMKUU LA MKOA LENYEWE LIMEKULA MPAKA HALIWEZI HATA KUTEMBEA KWA SASA, LINATIA HASARA SERIKALI MAANA HATA SHANGINGI ANALOTUMIA LAZIMA LITAKUWA LINAKULA MAFUTA ZAIDI MAANA LIMEBEBA MZIGO MKUBWA KULIKO UWEZO WAKE! amebakia kuzinduaFIESTA tu kwake, hivi ndio vitu vya maana!
  ni huyo mwenye tracksuti nyeusi
   
 9. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadhani huo ulikuwa ni mkutano wa pili kufanyika. Kiukweli mkuu wa mkoa alichofanya ni propaganda lakini nadhani matokeo yake ameshayapata.
   
 10. TOFU

  TOFU JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 532
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Ccm kamata ...!
  Kamata.....!!!
  Weka chini.....!!
  Shindiliah Shindiliah Shindiliah Shindiliah Shindiliah Shindiliaaasaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah
  Mpaka ipotelee..
   
 11. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu madiwani wa CHADEMA Moshi, kwa hiyo kama huyo Rais wa CCM anatangatanga hovyo kwa kufuja hela za wananchi na sisi CDM ndo tutangetange na kula hela za wananchi bila sababu? Hivi kweli tunahitaji madiwani wote kwenda Rwanda kujifunza usafi? hatuoni aibu? Tuache masihara jamani na tufanye mambo yenye msingi. Bora mngesema hata mnatumia hizo hela kukusanya nguvu ya wananchi wajitolee kufanyia usafi jiji la Moshi walau kwa siku mbili then muwanunulie chakula wale.

  Kila mtu anajua usafi, tusidanganyane kwamba tunaenda kujifunza Rwanda. Mtoto akijinyea na wewe mtu mzima ukajinyea wakati unajua kabisa sio sahihi, sisi watu wazima wenzio tutakushangaa sana.

  CHADEMA msiingie kwenye mkumbo wa CCM wa kufuja hela za wananchi bila sababu.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wanaenda kujifunza kufagia? viwanda vingine noma.
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nimesoma habari kama mara tatu lakini sijaona sehemu ambayo CHADEMA imemuumbua Mkuu wa Mkoa zaidi ya kuona tu kuwa Meya amejiumbua mwenyewe na wenzake waliotaka kufuja pesa za umma...
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,917
  Likes Received: 2,346
  Trophy Points: 280
  Kaika hili CDM hawasafishiki!
   
 15. darison andrew

  darison andrew Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli itakuweka hurun mtusaidie tunakufa kwa umasikini wa mmmmmm!!!![​IMG]
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu-wa-mkoa.jpg

  Wanakula nini hawa?
   
 17. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mleta uzi nadhani kuna mistari umeisahau kwenye hii single yako. naomba uiweke ili heading ilete maana la sivyo utakuwa mdaku kama Shigongo ambaye huwa anaweka heading kuuuubwa ila ukisoma ni ***** tu
   
 18. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hawa mapro wa CDM wana hasira zao kwani nani asiyejua Madiwani wanavyoshindana kula hela za Minara ya mawailiano hapo mjini na ugomvi wa Memorial sasa L. Gama wa nini tena? Yy katembelea kiwanda cha Ngozi huku makamanda eti wanamnanga haya kaeni na Mikoa yenu
   
 19. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Unafiki mtupu, watu wanakwenda kujifunza yeye anawawekea kauzibe haoni mjiwa wa MOSHI ulivyo safi? aende akamzuie vasco da gama kutumia fedha za umma kukodi wanamziki wakawaburudishe nyumba ndogo zao huko marekani na uingereza. mbona vasco dagama katumia ndege ya serikali kwenda kumnasua rizmoja huko uchina aliko kamatwa na madawa?
   
 20. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Tatizo hapa ni Katiba ya nchi jinsi gani wananchi wanaweza wabana wawakilishi wao wasiwe wabadhirifu! Kama wananchi wanakubaliana na hizi cost na wahusika wamefuata taratibu kwanini RC analeta siasa? Kuna kitu kinaitwa retreat,je huyu mkuu wa mkoa anaelewa maana yake? Moja ya makosa makubwa alifanya Mwl. Nyerere ni kwa akili ndogo kwenda kuongoza akili kubwa.. Lazima nchi itakwama! Mtu mwenye akili za kitumwa ataongozaje mtu mchapa kazi na mwenye kutaka maendeleo?!
   
Loading...