Joseph Ludovick
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 383
- 507
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinafuatilia kwa karibu na kinafanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zinazosambazwa mitandaoni kuhusu madai ya kupigwa kwa Mratibu wa Uenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Mh. Sigrada Mligo ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Miongozo yake.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Taarifa ya leo Machi 31, 2025 iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia imeeleza kuwa CHADEMA inafuatilia kwa makini njama za Chama cha Mapinduzi (CCM) za kutumia tukio hili kwa manufaa yao binafsi.
"Tunatoa wito kwa Mh. Sigrada Mligo kuwa makini na mahusiano yake na CCM ili kuepuka kutumiwa kwa malengo yasiyo na nia njema, ambayo yanaweza kuathiri si tu hadhi ya Chama bali na ya kwake pia kama kiongozi na usalama wake binafsi." imesema taarifa hiyo
"Tunaendelea kufuatilia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa kwa kushirikiana na vyombo husika vya ndani na nje ya Chama, na baadae tutatoa kauli rasmi kuhusu suala hili kadri itakavyofaa." imesema
CHADEMA watakuwa wanapanga njama za kumdhuru ili wahamishie lawama kwa CCM. kuweni makini na False Flag. Hii ni style yao tangu zamani.
Pia, Soma