Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, ametangaza kuwa chama hicho kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema ni kinyume na sheria na demokrasia. Ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2025, Jijini Dar es Salaam alipowasilisha maazimio ya Kamati Kuu ya chama mbele ya waandishi wa habari.
"Tarehe 03 Juni 2025, Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) imekaa, kupokea na kujadili juu ya taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa umma tarehe 27 Mei 2025 ikiwa ni msingi kutoka kwenye barua aliyoiandika kwa Katibu Mkuu tarehe 12 Mei 2025, katika barua aliyoiandika kwa chama Msajili ameelekeza kwamba chama kijaze nafasi zilizo wazi za viongozi ambao awali walikuwa wameteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la tarehe 22 Januari 2025, sambamba na Wakurugenzi wa chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya Kamati Kuu vilivyofuatia mwezi Februari na tarehe 10 na 11 mwezi Machi 2025"
"Kamati Kuu baada ya kutafakari kwa kina imeamua kwenda Mahakamani kwa vile imeshindwa kuiona nia njema ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika maamuzi yake aliyoelekeza kwenye barua aliyoitoa kama taarifa kwa umma, Kamati Kuu imewaelekeza Wanasheria wa chama kuwa hadi kufikia Alhamisi tarehe 09 Juni 2025 shauri hili liwe limepelekwa Mahakamani"
"Kuhusu taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuzuia ruzuku ya chama (CHADEMA), tunaenda Mahakamani kwa sababu Msajili wa Vyama vya Siasa amechukua jukumu la kuzuia ruzuku ya chama chetu, sasa sheria anayoisimamia Msajili mwenyewe yaani Sheria ya Vyama Siasa, kifungu cha 18(6) kinasema Msajili ana uwezo wa kuzuia ruzuku ya chama kingine chochote cha siasa kinachopokea ruzuku pale tu ambapo kuna kweli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa chama hicho"
"Kwamba labda chama kimefanya matumizi ya hovyo ya fedha na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amekagua na ametoa ripoti, kama vile mnavyosikia ripoti ya CAG inasema serikali imefanya matumizi yasiyokuwa na tija, sasa kwetu sisi (CHADEMA) kama mkaguzi angekuwa amekagua tukapata hati chafu kwa mfano au fedha zimetumika vibaya, au jambo lingine lolote linalofanania na hilo, kwa mujibu wa kifungu hicho cha 18(6) hapo tu ndipo Msajili anapopata mamlaka ya kuzuia ruzuku"
"Utaratibu wa jambo hili unaenda mpaka kwenye utaratibu ikiwemo barua, na hilo linaenda mpaka kwenye Baraza la Wadhamini la chama, kwa sababu chama hiki ni mali ya Baraza la Wadhamini, sasa ili hatua hiyo ifikiwe ni lazima chama kishindwe na Bodi ishindwe, na ripoti maalum za ukaguzi zioneshe kwamba kuna matumizi ya hovyo, sasa tunaenda Mahakamani kuonesha kutokubaliana na jambo hilo"