CHADEMA yambeba Odinga

CHADEMA yambeba Odinga

Acha Ujinga mkuu na acha kuwa kama wale wanao Chora Zombi, kwa hiyo vyama kama REPBLICAN Cha USA ni chama cha Kidini, Conservative, kwa kifupi viko vingi sana na orodha ni ndefu sana na nilisha wahi kuileta humu day one, so hata ODM ni chama cha Kidini? Na unajua ukiachilia IDU muungani mwingine unaitwa nini? ambao una vyama kama Democratic na kazalika,

IDU memorandum yake inasema wazi wazi kuwa ni muungano wa vyama vyenye kushabikia ukristo kitu ambacho ndicho Republican Party ya USA wanachofanya. Kwa hiyo kama CDM nao wanashabikia ukristo, basi inabidi waliseme hilo wazi na kuwa wanafuata matakwa ya IDU hata kama ni hatari kwa taifa.


Kuhusu kusapoti hiyo iko wazi kabisa, na inaruhusiwa kabisa na kila mtu anajua hilo, na hata CCM hawawezi ongea chochote maana wanajua na Mkuu kisicho ruhusiwa ni Nchi kusapoti Mgombea fulani wa chama fulani kwenye Uchaguzi, kufanya hivyo ni kujatafutia matatizo na hata kuvunjika kwa uhusiana pale ambapo mlio kuwa mnamtarajia hakushinda na kashinda mpinzani wake,

Kwa Vyama hakuna kitu kama hicho make Vyama na Setikali ni Vitu viwili tofauti kabisa

Kwa hiyo chama cha Ahmedinajad wa Iran kikiwapa CCM mamilioni kwa ajili ya uchaguzi 2015, wewe huoni kuwa watakuwa wanaiingilia demokrasia yetu?
 
Chadema yambeba Odinga

JUMATATU, MACHI 04, 2013 06:21 NA ARODIA PETER, NAIROBI

chadema.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo

*Kilimtumia magari, wasanii kuzunguka nchi nzima

WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.

Chadema ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja.

Mbali ya kutuma magari hayo, Chadema walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide’.


Habari kamili: Chadema yambeba Odinga


Hivi huu ni mchezo mzuri kwa CHADEMA na Tanzania kwa ujumla kujiingiza katika siasa za mataifa mengine? Je kuna faida gani na hasara zipi za vitendo kama hivi? Ni nani anayefaidika na uingiliaji huu, CDM, Odinga au viongozi wa CDM? Je hii haihatarishi usalama wa mataifa yetu yote kwa kushabikia <50% ya waKenya?
[/QUOTEI

ID yako tu tosha..
 
Mnapojenga hoja hapa, jaribuni kuangalia pia athari zake.
Kwa hiyo mnataka kutuaminisha kuwa CHADEMA inafanya kile ambacho CCM walikifanya kwa Malawi?.

Kama hivyo ndivyo, Sasa kipi ni tofauti ya CHADEMA na CCM kama vyote vinafanya vivyo hivyo kwa maana kwamba hata madudu ya CCM nao CHADEMA kikiingia madarakani kina ruhusa kuyafanya pia kwa vile CCM kiliyafanya.

Si suala la kwamba ccm wamefanya ama hawajafanya, muhimu ni kuangalia kama ushirikiano huo una athari gani kwa chama chetu ama nchi yetu. Vyama vya siasa duniani kote vinashirikiana katika nyanja mbalimbali kadri ya mahitaji ya kila chama na nchi husika.

Lakini najua ninyi mliolishwa nyamafu na ccm huwa mkiona jambo limefanywa na Chadema hamuachi kutokwa na mapovu. Kila jambo linalofanywa na Chadema huwezi kulifananisha na jinsi ccm wanavyolifanya ama kutaka kuigeuza ccm kuwa ndio msahafu huo ni ufinyu wa fikra.

Na kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na ccm si kwakuwa ni ccm bali kwakuwa ndivyo mfumo wa maisha ulivyo ama mfumo wa kijamii unavyotaka na si suala la ccm. Ukweli ni kwamba ccm hawajawahi kuasisi kitu chochote ambacho kimeweza kutumiwa kama mfano huko duniani kwahiyo jaribuni kupanua akili yenu kutooona kila kitu kwa miwani ya ccm.
 
Kuhudhuria na kusaidia kwenye kampeni ni vitu viwili tofauti kabisa. Kuhudhuria hakumaanishi kuwa active kwenye maswala ya huyo aliyewaalika zaidi ya kuwa mtazamaji. Kujihusisha kwenye maswala ya kampeni ni kuvuka mipaka ya kuwa mtazamaji na kuwa ni muhusika hai. Katika macho ya mahusiano ya kimataifa na dipromasia, hili ni kosa.
Nilikujibu kutokana na counter argument yako kwa kubwajinga pale uliposema,



CCM walifanya makosa makubwa kufanya hivyo hasa ikizingatiwa kuwa ni chama ambacho kilikuwa kinaongoza serikali. Hii pia haiwapi CHADEMA tiketi ya kufanya madudu ya waliyofanya CCM.
Tunasubiri kuona CCM wakipiga kelele kuhusu hili na mwanasheria mkuu awafungulie mashitaka CHADEMA.
 
Kweli kabisa mkuu, tena baada ya hizo kampeni Komba akapewa zawadi ya shule. Kuna Shule hipo kule mbweni inaitwa Bakili Muluzi Sec. inamilikiwa na huyu komba...

sasa hili jamaa na njaa zake limeingia ccm ukubwani 2005 na kwanza kubwabwaja tu bila kujua hapo nyuma hilo chama lake mfu lishafanya hivo,. Iacheni chadema ifanye mambo yake kama haivunji sheria
 
Ni jambo la hatari sana chama cha siasa au hata mwanasiasa binafsi kutoka nchi "A" Kuingilia na kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye masuala ya kisiasa ya nchi "B". Jambo hili nihatari bila kujali chama au mwanasiasa anayefanya mchezo huo.Kama CCM walikosea huko nyuma; basi hiyo haiwezi kuwa sababu ya msingi kwa CHADEMA kufanya kosa hilo hilo.
 
Kwa hiyo Islamic Coalition Party ya Iran ikiwatumia CCM helcopta 20 na pesa $100,000,000 ili washinde uchaguzi 2015 wewe utajisikiaje?


Wewe mbona ni mugumu sana kuelewa? kwa nini unashindwa kukubali baada ya kugundua kuwa uliweka hii post yako pasipokuwa na utafiti na watu wanaojua wameshakujibu kuwa hiki ni kitu ambacho kinakubalika kimataifa!

Wewe umebaki na na mambo ya uisilamu tu, hivi ni kwanini mifano yako yote inalenga huko? Au ndo udini unakusumbua mwenzetu!
Jibu ni kwamba kama CCM wana uhusiano na vyama hivyo basi wako huru kupokea lakini!
 
Mkuu ili Uhuru Kenyata aendelee kulinda mali za familia, fikilia athari za Kenyata kingdom kuporomoka!!!Thirty six thousand hekters of land, from coast Mombasa to Nakuru, to mention a few!!!!!
 
Tunashukuru kwa darasa, JF utajifunza mengi labda kama hutaki kujua!!!
 
Kama habari hii ni ya kweli, CDM wamefanya kitu cha kipuuzi na kipumbavu.
unashangaa?chadema ndo zao hizo,yaani wameshaweka mia kwa mia kuwa odinga anashinda.VIPI AKISHINDA UHURU?si ndio mambo ya aibu hayo.

Juzi hapa wanampa kawambwa siku 14,aache kazi au la kitawaka.siku zimeisha nasikilizia watafanyaje .
 
Mkuu na waziri Makufuli nasikia alikuwa huko akihamasisha wapiga kura, basi na yeye sasa amegeuka CHADEMA???
 
unashangaa?chadema ndo zao hizo,yaani wameshaweka mia kwa mia kuwa odinga anashinda.VIPI AKISHINDA UHURU?si ndio mambo ya aibu hayo.

Juzi hapa wanampa kawambwa siku 14,aache kazi au la kitawaka.siku zimeisha nasikilizia watafanyaje .
Wewe umefurahi watoto woote nchi nzima SIXTY % kufeli, kwa hiyo CHADEMA ni mazumbukuku??? Unataka waziri aendelee kutuletea matahira kwenye system ya nchi yetu, na kwa nini asijiudhuru????

 
Siku hizi ulinganishwaji wa mambo si mtu anafanya nini, na wala si siasa tena, zinalinganishwa dini, eti je Islamic coalition? Je Christian union? Utadhani kuna mahubiri ya injili au kusilimishana hapa, nakerwa si kidogo!!
 
Wewe mbona ni mugumu sana kuelewa? kwa nini unashindwa kukubali baada ya kugundua kuwa uliweka hii post yako pasipokuwa na utafiti na watu wanaojua wameshakujibu kuwa hiki ni kitu ambacho kinakubalika kimataifa!

Wewe umebaki na na mambo ya uisilamu tu, hivi ni kwanini mifano yako yote inalenga huko? Au ndo udini unakusumbua mwenzetu!
Jibu ni kwamba kama CCM wana uhusiano na vyama hivyo basi wako huru kupokea lakini!
kwahiyo mtu akitaja iran tu tayari amekua mdini?.

Kama hivyo ndo unavyofikiri,itabidi urudi standard one.
 
Wewe umefurahi watoto woote nchi nzima SIXTY % kufeli, kwa hiyo CHADEMA ni mazumbukuku??? Unataka waziri aendelee kutuletea matahira kwenye system ya nchi yetu, na kwa nini asijiudhuru????

kwahiyo hao kufeli kasababisha shukuru?kama ndiyo HOW?.
 
Wewe mbona ni mugumu sana kuelewa? kwa nini unashindwa kukubali baada ya kugundua kuwa uliweka hii post yako pasipokuwa na utafiti na watu wanaojua wameshakujibu kuwa hiki ni kitu ambacho kinakubalika kimataifa!

Wewe umebaki na na mambo ya uisilamu tu, hivi ni kwanini mifano yako yote inalenga huko? Au ndo udini unakusumbua mwenzetu!
Jibu ni kwamba kama CCM wana uhusiano na vyama hivyo basi wako huru kupokea lakini!

Taifa lipi hilo linalokubali kuingiliwa kwenye chaguzi zake?
 
Mnanikumbusha tulivyomsimika Rais wa Comoro.
Mbona tumesaidia kwa Kabila chini ya Banyamulenge tukamtoa Mobutu.
Mbona misaada ni Kawaida jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom