CHADEMA yakerwa na tamko la Kamati Kuu ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yakerwa na tamko la Kamati Kuu ya CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Nov 24, 2011.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
  KURUGENZI YA HABARI NA UENEZI –MAKAO MAKUU
  TAMKO KWA UMMA WA WATANZANIA

  YAH: KAMATI KUU YA CCM KUMWAGIZA RAIS KIKWETE AKUTANE NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

  Kurugenzi ya Habari na Uenezi imeshangazwa na tamko lililotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye kuwa "Kamati Kuu ya CCM imemwagiza Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akutane na vyama vyote vya siasa badala ya CHADEMA peke yake" aliendelea Kusema kuwa …… "Pamoja na kukubali akutane na CHADEMA, tumetahadharisha kuwa lazima kushirikisha wajumbe wengine kutoka kwenye vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe CHADEMA pekee".

  Awali ya yote tunapenda kusisitiza kuwa maridhiano ya kitaifa juu ya mchakato wa kuweza kufikia kupata katiba mpya ni suala ambalo ni la muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu na haswa kama muafaka huo utafikiwa kwa nia njema ya kujenga na kuimarisha mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini, rangi, kabila ama itikadi za vyama vyao.

  Tamko la Kamati Kuu ya CCM linaonyesha muendelezo wa matamko ambayo wamekuwa wakiyatoa kila mara wanapokutana, mathalani kikao kilichopita kiliiagiza serikali kuwa bei ya mafuta ya taa lazima ishuke, kitu ambacho mpaka leo hakijafanyiwa kazi na hii inaonyesha jinsi ambavyo Kamati kuu hiyo isivyokuwa na msimamo juu ya maamuzi yake na maagizo yake inayotoa kwa viongozi wa kiserikali.

  Tamko hili, limetushangaza kwani limeonyesha wazi kuwa kuna hofu miongoni mwa viongozi na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuwa sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa kushirikiana na wale wa CUF haina muafaka wa kitaifa na hivyo wanamwagiza Rais kukutana na makundi mengine ili kupata maoni kabla ya kuisaini sheria hiyo.

  CHADEMA tuliandika barua kwa Rais naye alikubali kukutana nasi, kitendo cha Kamati Kuu ya CCM kutoa tamko hili ni dhahiri kuwa kamati kuu ya CCM imejitwalia madaraka ya kuwa wasemaji wa vyama vingine vyenye uwakilishi Bungeni ambao mpaka leo hatujawasikia wakitoa tamko juu ya suala hilo. Tunajiuliza hivi Kamati Kuu ya CCM leo imekuwa ndio wasemaji wa vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA?

  Pili, Vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA NA NCCR-Mageuzi waliopinga muswada huu, vyama vingine mathalani CUF, CCM na TLP wao waliunga mkono kupitishwa kwa muswada huu, sasa Kamati Kuu ya CCM inataka wakakutane na Rais ili kujadili kitu gani? Wakati walikuwa ni sehemu ya maamuzi ambayo CHADEMA na wadau mbalimbali wanayalalamikia na ndio maana tukataka kuwasilisha malalamiko yetu kwa Rais.

  Tunapenda kuikumbusha Kamati Kuu ya CCM kuwa CHADEMA iliomba kukutana na Rais wa Nchi na sio kama Mwenyekiti wa chama, iwapo Rais atakubaliana na agizo hili la Kamati Kuu ya CCM itakuwa dhahiri kuwa ni muendelezo wa ushahidi kuwa viongozi wa Kiserikali wamekuwa wakitimiza majukumu yao kutokana na shinikizo la Chama hata kwenye masuala ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kama suala hili la Katiba lilivyo.

  Mwisho, Tungependa kumshauri Rais kuwa pamoja na kukutana na CHADEMA atenge muda ili aweze kukutana na makundi mengine mbalimbali ya kijamii yenye maoni na malalamiko kabla ya kusaini sheria iliyopitishwa na Bunge kwa maslahi ya taifa letu na ili kuweza kuleta utengamano wa kitaifa .
  Imetolewa na

  ……………………
  Erasto Tumbo
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
  24 Novemba 2011.

   
 2. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Peoles power daima! well crafted!
   
 3. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  aaaaaah!ccm we, nitakimiss sana hiki chama kikifa.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa wako makini sana mweee
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  peeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeepleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeesssssssssssssssssss poooooooooooweeeeeeeeeeer,

  CDM wana akili sana, hawa jamaa wa CCM ni vilaza nadhani ndiyo maana wanatoa rasilimali za waTZ burbure maaana hawaelewi ni wazito wa akili,
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Na hapo ndo cdm inapojipambanua kama chama makini na chenye maono ya mbali ktk kuiletea nchi hii maendeleo.
   
 7. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Huu ni ushaidi dhahiri kuwa kamati ya ccm haimuamini mweneykiti wake, wana wasiwasi asipopata wapiga chapuo kutoka kwa wafuasi na vibaraka wao walijificha kwenye vyama vingine vya upinzani, anaweza kuzidiwa hoja na hivyo kuwasariti.

  Si mmeona hata alipoitisha mkutano wa kile anachosema kuzungumza na wazee wa dar si ni wana ccm tu?! wanajua wazi kuwa mawazo thabiti kutoka upande wa nje ya ccm yana nguvu sana na hivyo kutaka nguvu ya pamoja kupingana nayo.
   
 8. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  well written, bravo bravo bravo ! Sasa pata bahati ya kukutana na writings za CCM utatoka nanmmaswali mengi kuliko majibu.
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hii ya CCM kukurupuka ni sawa na kumuona jamaa anaelekea Ubungo ukamfuata wakati wewe ulikuwa huna mpango wa kwenda huko.

  Chadema ina sababu zake wanapinga mswada kusainiwa, sasa CCM na CUF watakwenda na hoja gani, kama hoja yao ni kuupinga mswada sawa waende makao makuu ya Chadema waone ni kwa namna gani wataunganisha hoja lakini kama wana hoja tofauti na Chadema waombe siku nyingine wakutane na rais hawakatazwi.

  Hii ni sawa na fujo za kisiasa, ni sawa na kusikia BAKWATA wanataka kumuona raisi nayo Jumuiya ya Kikirsto Tanzania CCT wakaomba waingie gari moja.
   
 10. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Naaaam..
   
 11. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  walikolalia..............ndio chadema wameamkia huko!!

  anatakiwa raisi peke yake kama alivyoongea na wanaojiita wazee wa dsm ndo akaongee na cdm

  ila asipotoa excuse ya alshabab, atatafuta wasemaji wakuu yeye atakaa kucheka tu
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huo ni msimamo makini wa CDM kutokubali kuchanganywa na CCM maana wao walisha kubali na kupitisha hiyo rasimu, sasa papara za nini wasubiri waone mziki wa CDM pindi wakikutana na Rais wa nchi!!!!!
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  CDM mmepigwa bao la kisigino. Naona mmeishiwa nguvu kabisa. Hapo ndio mjuie CCM kuna vichwa vinafanya kazi!
   
 14. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Nawaomba Cdm wawashirikishe wabunge wa nccr siyo chama at least mwakilishi mmoja wale waliopinga mswaada. Maana chama kama chama hawasomeki mpaka leo Mbatia kashikwa na kigugumizi mpaka leo.
   
 15. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  hahahahahaha! yaani matamko ya CCM utafikiri ya mwendawazimu.
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kwa nini asiwe msemaji wa hivyo vyama wakati ni vyake? utamtenganisha Mrema na CCM? Utamtenganisha Cheyo na CCM? Utamtenganisha Hamad Rashid na wenzie na CCM? Lazima awasemee ili kuwakumbusha wajibu wao kwa mjibu wa CCM
   
 17. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  kuna hofu miongoni mwa viongozi na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuwa sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa kushirikiana na wale wa CUF haina muafaka wa kitaifa na hivyo wanamwagiza Rais kukutana na makundi mengine ili kupata maoni kabla ya kuisaini sheria hiyo.

   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCM kuna vichwa hatari, jamaa hakutegemea kupigwa bao la kisigino. Mpira umeisha na sasa wanatafuta ushindi wa mezani wa kuonana na JK ikulu, huu ni ushindi wa mezani. Ushindi wa dkk 90 wameshindwa bungeni!
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja, kwani nao walipinga kupitishwa kwa muswaada huo, some time wale unaoendana nao kimawazo, usiendelee kuwatenga
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mkuu embu jaribu kuweka na hiyo sentesi yako kwa kidhungu tuone inakuwaje.
  kama ni mimi ningesema ''this is ward english school, hehehehehehe! which ward did you learn? hohoho, hahahahahaha, kumbe na mimi nimo. dah! aisee kingereza ni issue.
   
Loading...