CHADEMA yakana vikumbo vya urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yakana vikumbo vya urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jan 10, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kwa sasa hakiwezi kuanza mbio za kusaka urais. Badala yake, kinatumia muda huu kujikita kutatua matatizo ya jamii yanayozidi kuongezeka.

  Pia, Chadema kinasema kumewapo na taarifa zinazosambazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, zikiwa na nia ya kuonyesha kuwa kuna mbio za kuwania urais ndani ya chama.

  Taarifa ya chama hicho iliyotolewa jana, inasema kuna baadhi ya watu wanapewa nafasi kubwa kugombea nafasi hiyo, kiasi kwamba sasa ndani ya Chadema ni mvutano wa kuwania urais.

  "Chama kinapenda kutoa taarifa sahihi kwa wanachama, wapenzi, washabiki wake na Watanzania wote kwa ujumla, juu ya suala hili ambalo linaweza kuiweka Chadema katika mizania moja na vyama vingine," inasema sehemu ya taarifa hiyo. Kinasema kimekuwa kikifanishwa na viongozi wa vyama vingine ambao wamekuwa wakilifanya suala la kugombea urais kuwa linaongozwa na kuamriwa kwa utashi binafsi wa mtu, uchu na tamaa ya cheo.

  Miongoni mwa mambo ambayo yanazungumziwa kwenye taarifa hiyo, ni kwamba Serikali imekuwa ikiishia kushughulika na dalili au matokeo yanayojitokeza, hivyo kukosa majibu ya kudumu na kuishia kutoa lawama kwa wakosoaji wake.

  Taarifa hiyo inasema katika chama chao, kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma kwa ajili ya maendeleo ya watu siyo mbio za kusaka vyeo.

  "Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya Chadema, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Inasema hivi sasa ndani ya Chadema hakuna cha ‘kupamba moto' kwa ajili ya kuwania urais, wala hakiwezi kuwapo.

  Chadema imesema suala muhimu ni namna ya kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayokabili jamii pana ya Watanzania, kisha kutafuta majibu au suluhisho ya kudumu, kwa kushirikiana na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao.

  CHANZO: Mwananchi

  =================
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hakika kitengo cha Mnyika sasa kipo kazini.Thats what we like
   
 3. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nikacho takiwa kila uongo ukitolewa ujibiwe kwa haraka,
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Wana JF,

  Itakuwa vizuri zaidi tukajikita katika kujadili mchakato wa katiba.Tujadili maudhui ya katiba mpya ili tupate katiba bora kabisa ili tufike kwenye demokrasia ya kweli na tujenge Tanzania tuitakayo miaka 50 ijayo kuanzia sasa

  Kwa wanachadema,tujadili namna bora ya kutunga sera mbadala na tufikirie zaidi kujiimarisha kama timu ili ifikapo 2015 tuingie kwenye uchaguzi mkuu tukiwa hatuna mgogoro wala makundi.Tukiimarishe chama chetu,tunayo fursa ya kuendelea kusaidiana na viongozi wetu wa ngazi zote na tuweke miundombinu itakayotupatia viongozi bora watakaotupeleka 2015.Wakati wenzetu wanagawanyika basi tutumie fursa hii kujiimarisha ila kwa tahadhari ya hali ya juu ili tusije tukaingia kwenye mtego wa kutegemea udhaifu wao tu

  Tuweke mikakati mizito,tuzibe mianya yote na udhaifu uliokuwepo uchaguzi uliopita.Tunayo dhamira moja,naamini chama chetu kitatoa mgombea bora 2015 bado.Kitu cha msingi tuepuke ubinafsi tualenge kwenye maslahi mapana ya chama na taifa letu kwa ujumla.Uchaguzi wowote au uteuzi ndani ya chama chetu ni lazima tuuweke kwenye mizani ya 2015,ni uchaguzi wa Transitional team.

  Ni wakati muafaka kwa wanachama na viongozi kupima aina ya kauli tunazotoa vinywani mwetu,sio muda wa kutoa reckless statements.Tuwekeze na tuimarishe kitengo chetu cha research.Ni muda wa uwajibikaji zaidi na kila mmoja awe evaluated kupitia results zinazoonekana

  Kuna mgombea/wagombea wa chama tawala wanajitahidi kujitenga na udhaifu wa serikali iliyopo ili kujenga aura ya messiah ajaye.Watanzania tusidanganyike. Wanajitahidi kujifanya wanaguswa na matatizo ya vijana ili kuteka kundi la vijana ambao ndio mtaji mkubwa wa vyama na wagombea urais 2015. Tuitumie taasisi ya BAVICHA katika hili na kitengo cha research.Tusiingie kwenye mtego wa majungu kama wenzetu.Pia katibu mkuu na secretariat wanajituma tuwaongezee nguvu

  Tujipange kikamilifu kwani uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana,naamini CHADEMA itaweka historia.Tupanue mtandao,tuimarishe safu ya uongozi na kuhakikisha umoja na mshikamano ndani ya chama,tufanye tafiti za kutosha tuandae ilani ambayo itakuwa the best na itakayo sustain transition kwa kuzingatia waathirika wakubwa na walengwa ambao ni kundi kubwa la vijana katika aspect zote

  Ni ufafanuzi mzuri
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Good!! Hilo ndilo jawabu sahihi kwa wachongaji!
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  This is what i understand, haya ya Mwananchi na mwandishi wao sijui walipatia wapi.

  sometimes vyombo vya habari viwe makini sana, nashawishika kuwa mauaji ya kimbari yalichangiwa na aina hii ya uandishi wa habari eti Na mwandishi wetu.

  Ukisoma content na title wala havikuwa na hadhi ya gazeti la Mwananchi. Labda waliishiwa habari?
   
 7. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #7
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]
  TAARIFA KWA UMMA[/FONT]

  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]MAHITAJI YA UMMA NA SIFA ZA KIONGOZI, KUAMUA MGOMBEA URAIS, SI UTASHI WA WATU/MTU BINAFSI[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]KUMEKUWEPO taarifa zinazosambazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, zikiwa na nia ya kuonesha kuwa kuna mbio za kuwania urais ndani ya chama na kuwa kuna baadhi ya watu wanapewa nafasi kubwa kugombea nafasi hiyo, kiasi kwamba sasa ndani ya CHADEMA "hapatoshi" kwa ajili ya kuwania urais.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Chama kinapenda kutoa taarifa sahihi kwa wanachama, wapenzi, washabiki wake na Watanzania wote kwa ujumla, juu ya suala hili ambalo linaweza kuiweka CHADEMA katika mizania moja vyama vingine au kuwafananisha viongozi wa chama hiki na viongozi wa vyama vingine ambao wamekuwa wakilifanya suala la kugombea nafasi ya urais kuwa linaongozwa na kuamriwa kwa utashi binafsi wa mtu, ukiongozwa na uchu na tamaa ya nafasi ya vyeo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa sasa ndani ya CHADEMA kitu hicho cha ‘kupamba moto' kwa ajili ya kuwania urais hakipo na wala hakiwezi kuwepo. Hasa kwa sasa ambapo chama kimejikita kuzidi kujijenga kwa kutimiza wajibu wake, kama serikali mbadala inayosubiri kupata ridhaa ya wananchi kuongoza nchi.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa muda huu, kwa CHADEMA suala muhimu ni namna ya kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii pana ya Watanzania na kisha kutafuta majawabu au masuluhisho ya kudumu, kwa kushirikiana na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao, kwa ajili ya maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda muhimu, chama kinasimamia na hakiwezi kutolewa kwenye mstari kwa watu kukimbilia urais.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa CHADEMA, siku zote suala la urais linategemea na kufuata mahitaji mapana ya Watanzania, kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa, utashi au uchu wa watu/mtu binafsi. Na katika kufikia hatma ya mahitaji/ maslahi mapana ya wananchi, chama hiki siku zote huamua kwa kufuata na kuzingatia katiba, kanuni na taratibu zake, si vinginevyo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Ni uwezo na umakini wa kuzingatia mahitaji ya chama na maslahi mapana ya umma katika kuamua masuala mazito kwa mstakabali wa taifa, huku kikifuata katiba yake, kanuni na taratibu, ndiyo umekipambanua CHADEMA kuendelea kuwa chama makini, kinachoaminiwa kwa dhati na Watanzania, na kiupekee kuwa kinastahili kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mahitaji ya chama na ya Watanzania ndiyo yaliyotumika kupata wagombea urais wa CHADEMA katika chaguzi kuu mbili, mwaka 2005 na 2010. kwa kuzingatia mtazamo huo, mara zote hizo mbili, wagombea waliombwa, wala hawakuongozwa na uchu au tamaa ya madaraka. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Hali itakuwa hivyo hivyo wakati ukiwadia wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015, kamwe utashi, uchu au maslahi binafsi ya mtu hayawezi kupata/kupewa nafasi ndani ya CHADEMA.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Kwa CHADEMA, urais si cheo, ni dhamana ya utumishi kwa umma, suala ambalo linazingatia masuala muhimu, ambayo ni mahitaji ya wananchi (nchi) na kisha sifa za mtu husika kuwa kiongozi wa nafasi hiyo. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Kwa sasa CHADEMA na viongozi wake makini hawawezi kuanza mbio za kusaka urais, badala yake, muda wa sasa unatumika kujikita katika kushughulikia na kutafuta ufumbuzi wa vyanzo vya matatizo ya jamii yanayozidi kuongezeka, huku serikali ikiishia kushughulika na dalili/matokeo, hivyo kukosa majawabu ya kudumu na kuishia kutoa lawama kwa wakosoaji wake. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Daima, CHADEMA na viongozi wake makini, kitaendelea kuweka mbele kwanza kabla ya kitu kingine chochote, mapambano dhidi ya vyanzo vya matatizo kama vile umaskini (ugumu wa maisha), rushwa na ufisadi mwingine lukuki unaozidi kutafuna na kuangamiza taifa na watu wake, hali inayowafanya Watanzania kuwa katika mtanziko na mkwamo mkubwa kimaendeleo, miaka 50 baada ya uhuru, huku wakiwa ndani ya taifa lenye baraka tele za utajiri wa rasilimali na kila aina ya nyenzo muhimu inayohitajika kwa maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda ya muhimu kwa sasa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Imetolewa leo, Januari 8, 2012, Dar es Salaam[/FONT]
  [FONT=&amp]Kurugenzi ya Habari na Uenezi, Makao Makuu ya CHADEMA Taifa [/FONT]
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Haya ndiyo mawazo tunayohitaji kwa upande wa chama makini!!
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  That is a good move.

  Makene hivi ndivyo kurugenzi ya habari inavyopaswa kufanya kazi. Upuuzi wowote utakakuwa na lengo la kuwatoa watanzania kwenye agenda kuu ya kupambana na umaskini muupinge mapema kwa taarifa rasmi kama hii.

  Katika hili Makene tutawaunga mkono.
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana,Kitengo cha habari na uenezi.Well done

  Mods:poleni na kazi ! Ingekuwa vyema kama threads hizi zenye mtiririko unaofananan zikaunganishwa ili kutoa flow nzuri ya information and counter information
   
 11. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Iko vizuri ni vema kuweka utaratibu bora mapema ili huko mbele ya safari chama kisiwe genge la wasaka vyeo.
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Asante kwa ufafanuzi. Hayo mambo ya urais kupamba moto waachieni CCm.
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Maumivu ya kichwa huanza taratibuuu!! CDM, mnaongelea urais kitu ambacho kwenu ni ndoto!!! Labda jaribuni kuanzisha cheo cha rais wa CDM, instead of mwenyekiti! Urais wa JMT hamuuwezi!!!
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rejao,
  Chadema wanaota ndoto za mchana aisee! labda Rais kivuli.
   
 15. K

  KAMBAJECK Member

  #15
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Big up J. J Mnyika
   
 16. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Tunawasubiri waanze kugombana...lazima kizaliwe chama kipya cha siasa out of CDM!!
   
 17. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  inawezekana mwananchi linatumika kuvuruga chadema,..ila hawa CDM wako makini sana ndo maana galasa kama shibuda wameliacha lakini hawalipi ushirikiano.
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Humu JF wameishaanza kugombana mpaka wengine wanawambia wenzao wametumwa kuchafua chama.

  Chadema wanakimbilia mambo ya urais wakati kuna wabunge wengi watawapoteza.

  Wanatakiwa wajipange kwenye udiwani sio urais.
   
 19. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii press release ukiisoma kwa makini inakinzana na baadhi ya matakwa ya vigogo wa Chadema, so ni ya kujikosha. Tusisahau Zitto alishatangaza jimboni kwake kwamba 2015 atatupa kete kwenye Uraisi, nasubiria kwa hamu, TUENDELEE TU KUSHANGAAAAAAAAAA!
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Funguka zaidi kipo kazini kivipi?
   
Loading...