CHADEMA yaizika CCM Ukonga

CHADEMA yaizika CCM Ukonga

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Operesheni ya Chadema ni Msingi na vuguvugu la Movement for Change jimboni Ukonga imeonekana kukisimika vyema chama hicho jimboni humo.

Wanachama wa Chadema jimboni Ukonga hawasiti kuupongeza uongozi wa jimbo hilo chini ya Mwenyekiti Thomas Nyahende maarufu kama Mwita Maranya kwa kazi kubwa waliyofanya tangu waingie madarakani.

Jimbo la Ukonga lenye ubovu mkubwa wa barabara limekuwa ngome kuu ya CCM kwa miaka mingi.

Hata hivyo katika uchaguzi uliofanyika wa Serikali za Mitaa wiki iliyopita Chadema wamejipatia ushindi mkubwa katika mitaa 10 huku washirika wao CUF chini ya mwavuli wa Ukawa wakijipatia mitaa 2.

Kikubwa zaidi ni kwa chama hicho kuweza kujipatia mitaa miwili muhimu.Mitaa hiyo ni ule anaokaa Meya wa Ilala Jerry Silaa wa Guluka Kwalala Gongolamboto na Mtaa wa Kivule unaoaminika kuwa na wakazi wengi zaidi kuliko mtaa wowote DSM.Kwa mfano katika mtaa huo wa Kivule mshindi alikuwa ni Afisa wa Chadema makao makuu Kamanda Mwita Mwikabe Waitara aliyepata ushindi wa kimbunga wa kura 1262 huku CCM wakiambulia kura 663

Kabla ya uchaguzi huu upinzani kwa ujumla walikuwa wanaongoza mitaa 2 tu kwa jimbo zima.

Jumapili wiki hii kutakuwa na marudio ya uchaguzi kwa mitaa 23 ambayo haikufanya uchaguzi wiki iliyopita.

Katika mahojiano na wanachama na baadhi ya viongozi wa misingi wamepongeza uongozi bora wa Mwita Maranya unaoshirikisha viongozi wote wa ngazi za chini na uwajibikaji uliotukuka.

Pia wanachama wameutaka uongozi wa Jimbo kutokubweteka kwa matokeo haya mazuri bali waendelee kukijenga chama bila kuchoka ili mwakani waweze kupata mbunge na madiwani wengi kwa lengo la kuongoza Manispaa ili walau wasimamie fedha za wananchi na hatimaye barabara za Ukonga zijengwe.
 
Last edited by a moderator:
Kazi ya Maranya ni kazi iliyo tukuka chama cha mchwa kinatapatapa tu
 
Huyo kamanda wa Sinza,hatufai ,why kapoteza kata nzima?!Awajibishwe,huo ni uzembe,mie mtaani kwangu japo nimehamia muda mfupi,na sina cheo chamani,nimepiga mzigo nikiwashirikisha madogo wakanielewa na tukashinda Mwenyekiti na wajumbe wote?
 
Kamanda yupi mkuu Idimulwa? Mtaje kabisa maana Sinza kuna makamanda wengi kwa nafasi mbalimbali
 
Last edited by a moderator:
Chadmea kumekucha. Tuwakimbize hawa mafisadi.
 
Chadema kumekucha. Tuwakimbize hawa mafisadi.
 
Huyo kamanda wa Sinza,hatufai ,why kapoteza kata nzima?!Awajibishwe,huo ni uzembe,mie mtaani kwangu japo nimehamia muda mfupi,na sina cheo chamani,nimepiga mzigo nikiwashirikisha madogo wakanielewa na tukashinda Mwenyekiti na wajumbe wote?

Labda ni kibaraka wa wakubwa
 
safi sana cdm ukonga .

Kilio kikubwa cha wananchi wa Ukonga ni ubovu wa barabara zake zote kuu za kuingia ndani ya Jimbo hilo mfano barabara ya Kivule,Kitunda,Moshi Bar,Majohe nk.

Inaponyesha mvua barabara zote hazipitiki na nauli ya daladala inafikia sh 1000 kituo hadi kituo.

Madiwani wote wa Jimbo la Ukonga ni CCM ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kupigania kujengwa kwa barabara hizi lakini wote wanapigania matumbo yao tu.

Wananchi wanaamini kwa kuchagua madiwani wengi wa Chadema mwakani kutasaidia ujenzi wa barabara hizi
 
Nawaomba makamanda msilale...kimbizini majizi mpaka october mwakani ili kieleweke.....
 
Chadema kumekucha. Tuwakimbize hawa mafisadi.

Ubovu wa barabara za Ukonga umewaunganisha wananchi wote bila kujali Itikadi zao kupigana sambamba na Chadema
 
Labda ni kibaraka wa wakubwa

May be,nimechukia sana,mtaa niliokuwa naishi kabla ya huu niliohamia muda mfupi tumeshinda na ule wa zamani tena uko mkoa mwingine nimepiga kampeni kwa simu madogo wakaelewa cdm pia ikashinda!why kwa diwani???!
 
Nawaomba makamanda msilale...kimbizini majizi mpaka october mwakani ili kieleweke.....

Na ndivyo wananchi wa Ukonga wanautaka uongozi wa Kamanda Mwita Maranya kukaza kamba mara mbili ili kutokomeza kabisa CCM Ukonga.
 
Last edited by a moderator:
May be,nimechukia sana,mtaa niliokuwa naishi kabla ya huu niliohamia muda mfupi tumeshinda na rule wa zamani tena uko mkoa mwingine nimepiga kampeni kwa simu madogo wakaelewa cdm pia ikashinda!why kwa diwani???!

Kazi nzuri sana Kamanda Idimulwa
 
Last edited by a moderator:
Operesheni ya Chadema ni Msingi na vuguvugu la Movement for Change jimboni Ukonga imeonekana kukisimika vyema chama hicho jimboni humo.

Wanachama wa Chadema jimboni Ukonga hawasiti kuupongeza uongozi wa jimbo hilo chini ya Mwenyekiti Thomas Nyahende maarufu kama Mwita Maranya kwa kazi kubwa waliyofanya tangu waingie madarakani.

Jimbo la Ukonga lenye ubovu mkubwa wa barabara limekuwa ngome kuu ya CCM kwa miaka mingi.

Hata hivyo katika uchaguzi uliofanyika wa Serikali za Mitaa wiki iliyopita Chadema wamejipatia ushindi mkubwa katika mitaa 10 huku washirika wao CUF chini ya mwavuli wa Ukawa wakijipatia mitaa 2.

Kikubwa zaidi ni kwa chama hicho kuweza kujipatia mitaa miwili muhimu.Mitaa hiyo ni ule anaokaa Meya wa Ilala Jerry Silaa wa Guluka Kwalala Gongolamboto na Mtaa wa Kivule unaoaminika kuwa na wakazi wengi zaidi kuliko mtaa wowote DSM.Kwa mfano katika mtaa huo wa Kivule mshindi alikuwa ni Afisa wa Chadema makao makuu Kamanda Mwita Mwikabe Waitara aliyepata ushindi wa kimbunga wa kura 1262 huku CCM wakiambulia kura 663

Kabla ya uchaguzi huu upinzani kwa ujumla walikuwa wanaongoza mitaa 2 tu kwa jimbo zima.

Jumapili wiki hii kutakuwa na marudio ya uchaguzi kwa mitaa 23 ambayo haikufanya uchaguzi wiki iliyopita.

Katika mahojiano na wanachama na baadhi ya viongozi wa misingi wamepongeza uongozi bora wa Mwita Maranya unaoshirikisha viongozi wote wa ngazi za chini na uwajibikaji uliotukuka.

Pia wanachama wameutaka uongozi wa Jimbo kutokubweteka kwa matokeo haya mazuri bali waendelee kukijenga chama bila kuchoka ili mwakani waweze kupata mbunge na madiwani wengi kwa lengo la kuongoza Manispaa ili walau wasimamie fedha za wananchi na hatimaye barabara za Ukonga zijengwe.

Mbona huyu mama afisa uhusiano wa manispaa ya ilala ameitaja kivule kuwa uchaguzi unarudiwa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom