CHADEMA yaionya CCM Umeya Dar es Salaam

CHADEMA yaionya CCM Umeya Dar es Salaam

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemteua diwani wa Ubungo, Isaya Charles kugombea nafasi ya Meya wa jiji la Dar es Salaam, na kuitahadharisha CCM hakitakubali kuchezewa rafu katika uchaguzi huo.
-
Aidha, Chadema imemtangaza diwani wa Ubungo, Boniface Jakob kuwa mgombea wa nafasi ya Meya wa Kinondoni na diwani wa kata ya Bonyokwa, Charles Kuyeko kugombea umeya wa Ilala.
-
Uteuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Chadema (Zanzibar), Salim Mwalimu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
-
Majina hayo yaliteuliwa kwa ushirikiano ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema.
-
Mwalimu alisema wanatarajia kuona uchaguzi huo ukifanyika kwa amani na utulivu bila kuwepo na ubadilishwaji wa matokeo, kwa kuwa kuna mbinu chafu zinazofanywa na CCM sasa.
-
Alisema katika Halmashauri za Ilala na Kinondoni Chadema inaongoza kuwa na madiwani wengi lakini cha kushangaza CCM imekuwa haitaki kuyakubali matokeo hayo na kutaka kuyabadilisha.
-
"Kwa mujibu wa taratibu zilivyo ni kwamba Hamashauri yenye madiwani wengi ni kuwa chama hicho huchukua ushindi lakini hawa wenzetu CCM wamekuwa hawataki," alisema.
-
"Mfano mzuri katika Wilaya ya Temeke madiwani ni wengi wa CCM tumekubali huo ushindi kwa kuwa ni kweli wametuzidi.
-
"Kinondoni na Ilala hawataki umeya uchukuliwe na Chadema licha ya kuwa na madiwani wengi na sisi hatuwezi kukubali njama za wazi zinazofanywa na CCM.
"Na hata meya wa jiji lazima atoke Chadema kwa kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam tunaongoza kuwa na madiwani wengi."
-
Mwalimu alisema ameshangazwa na kitendo cha CCM kwenda Zanzibar kuchukua wabunge kwa ajili ya kupigia kura Kinondoni.
-
Alisema kitendo cha wabunge hao kukubali jambo hilo ambalo ni la aibu katika jamii inayowazunguka ni sawa na kuwazalilisha Wazanzibari kuwa hawajasoma.
-
"Unakubalije kubebwa kutoka Zanzibar kuja kupigia kura meya wa Kinondoni! Hivi kabisa mwenyekiti wa chama cha CCM anakubali hii aibu ya wazi wazi isiyohitaji propaganda ya kuleta majeshi Zanzibar" "Hilo jambo tutalipinga kwa nguvu zote."
-
Pia Mwalimu ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuhakikisha inamaliza changamoto zote zilizojitokeza katika viti maalum vya udiwani.
-
"Huko Kelwa tumeshinda viti vya udiwani 13 na CCM wameshinda 11 katika mgawanyo wa viti maalum Chadema wamepatiwa viti vinne na CCM imepatiwa vitano,? alisema.
-
"Hapa tumeitaka NEC itueleze huo mgawanyo umegawanywa vipi" Tumeenda kuwauliza wanatueleza Mkurugenzi hawampati kwenye simu ili athibitishe ni nani mwenye madiwani wengi. Eti mkurugenzi hapatikani na mwezi umeshapita."

CHANZO: NIPASHE
 
Waachane na ujanjaujanja tuna taka haki itendeke
 
Hakika Meya wa UKAWA Dar itakuwa maigizo tu.Chama tawala kitoe mameya wote na wenyeviti wa halimashauri.tunatekeleza sera za Chama kinachotawala tuu
 
Hii aibu unayojitia hapa utambue kwamba inawagusa moja kwa moja wazazi wako .
 
Kama nchi hii ingekuwa na msajili wa vyama anayetimiza wajibu wake akiwa huru, matukio ya uchaguzi wa Zanzibar na hizi figisu za umeya zilitosha kabisa KUFUTA USAJILI WA CCM. Kuna kila dalili kuwa hiki chama ni hatari kwa amani ya nchi kwa kuwa hawakubali kushindwa, hawajui maana ya demokrasia. Maeneo yote CCM iliyopata viti vingi vya udiwani uchaguzi umeenda vizuri kwa vile vyama vingine vimeheshimu maamuzi ya wananchi, CCM haitaki kuheshimu maamuzi ya wananchi. Ikumbukwe kuwa Watu waliwahi kufariki miaka ya nyuma kwa maandamano ya kumpinga meya Arusha
 
Meya wa UKAWA kwa Dar atafanya nini?hilo toeni jibu.sasa chama tawala kinaendelea kasi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemteua diwani wa Ubungo, Isaya Charles kugombea nafasi ya Meya wa jiji la Dar es Salaam, na kuitahadharisha CCM hakitakubali kuchezewa rafu katika uchaguzi huo.
-
Aidha, Chadema imemtangaza diwani wa Ubungo, Boniface Jakob kuwa mgombea wa nafasi ya Meya wa Kinondoni na diwani wa kata ya Bonyokwa, Charles Kuyeko kugombea umeya wa Ilala.
-
Uteuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Chadema (Zanzibar), Salim Mwalimu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
-
Majina hayo yaliteuliwa kwa ushirikiano ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema.
-
Mwalimu alisema wanatarajia kuona uchaguzi huo ukifanyika kwa amani na utulivu bila kuwepo na ubadilishwaji wa matokeo, kwa kuwa kuna mbinu chafu zinazofanywa na CCM sasa.

Alisema katika Halmashauri za Ilala na Kinondoni Chadema inaongoza kuwa na madiwani wengi lakini cha kushangaza CCM imekuwa haitaki kuyakubali matokeo hayo na kutaka kuyabadilisha.
-
"Kwa mujibu wa taratibu zilivyo ni kwamba Hamashauri yenye madiwani wengi ni kuwa chama hicho huchukua ushindi lakini hawa wenzetu CCM wamekuwa hawataki," alisema.
-
"Mfano mzuri katika Wilaya ya Temeke madiwani ni wengi wa CCM tumekubali huo ushindi kwa kuwa ni kweli wametuzidi.
-
"Kinondoni na Ilala hawataki umeya uchukuliwe na Chadema licha ya kuwa na madiwani wengi na sisi hatuwezi kukubali njama za wazi zinazofanywa na CCM.
"Na hata meya wa jiji lazima atoke Chadema kwa kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam tunaongoza kuwa na madiwani wengi."
-
Mwalimu alisema ameshangazwa na kitendo cha CCM kwenda Zanzibar kuchukua wabunge kwa ajili ya kupigia kura Kinondoni.
-
Alisema kitendo cha wabunge hao kukubali jambo hilo ambalo ni la aibu katika jamii inayowazunguka ni sawa na kuwazalilisha Wazanzibari kuwa hawajasoma.
-
"Unakubalije kubebwa kutoka Zanzibar kuja kupigia kura meya wa Kinondoni! Hivi kabisa mwenyekiti wa chama cha CCM anakubali hii aibu ya wazi wazi isiyohitaji propaganda ya kuleta majeshi Zanzibar" "Hilo jambo tutalipinga kwa nguvu zote."
-
Pia Mwalimu ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuhakikisha inamaliza changamoto zote zilizojitokeza katika viti maalum vya udiwani.
-
"Huko Kelwa tumeshinda viti vya udiwani 13 na CCM wameshinda 11 katika mgawanyo wa viti maalum Chadema wamepatiwa viti vinne na CCM imepatiwa vitano,? alisema.
-
"Hapa tumeitaka NEC itueleze huo mgawanyo umegawanywa vipi" Tumeenda kuwauliza wanatueleza Mkurugenzi hawampati kwenye simu ili athibitishe ni nani mwenye madiwani wengi. Eti mkurugenzi hapatikani na mwezi umeshapita."

CHANZO: NIPASHE
Wasije wakatumia nguvu kubwa kuionya CCM kumbe wakapigana bao wao kwa wao;kama kura ni siri ya mpigaji watajuaje kama CUF hawatampigia kura mgombea wa ccm kwa sababu moja au nyingine?Mfano mzuri ni uchaguzi wa juzi,kuna baadhi ya ukawa wanaanza kueleza ukweli kwamba kura za ubunge wamempa ukawa lakini urais wamempa Magufuli,unaposema hawa ni madiwani wangu au hawa ni watu wangu ndipo unapoanza kuchemka,tambua kwamba hakuna mtu mwenye watu wake,watu ni wa mwenyezi mungu na kwa nguvu za mwenyezi huyo huyo unaowaita leo watu wako kesho wanaweza kukubadilikia wakaamini kitu tofauti na unachoamini wewe kwa kufunuliwa.waache kulialia kwani kama kulialia mbona "wakati ule"walilia sana lakini mapenzi ya mungu yalitimia kwa Rais wa wananchi kupatikana?
 
Naona Kuna Mkanganyiko Kwenye Hiyo Habari,diwani Wa Ubungo Imejirudia Mara 2. Nijuzeni Huyo Meya Wa Jiji Anatoka Kata Gani Au Ndio Vijiweni Niliyoiona Jana Fesibuku?.
 
Msem wewe akili huna Kabisa, nadhani unafikiri kwa kutumia ma.... Unasema CUF leo, kwanini usiseme CDM name kama wanajua hilo kwanini wawalete mamluki waje kupiga kura? Jitambue kaka.
 
Waachane na ujanjaujanja tuna taka haki itendeke

Tujitahidin kuwa msaada kwa wasio elewa demokrasia. Hivi ni lazma ukawa au ccm wachaguane? Vp wasiporizka na mteuliwa wataharb kura?
 
Mpigieni kura meya toka ccm kwa manufaa ya jiji.kutoka UKAWA atapwaya sana
 
Tujitahidin kuwa msaada kwa wasio elewa demokrasia. Hivi ni lazma ukawa au ccm wachaguane? Vp wasiporizka na mteuliwa wataharb kura?

Haitakaa itokee kwa siasa za taTZ
 
Back
Top Bottom