Jmushi1,
Unatafuta jibu la swali ambalo tumekwisha kwambia toka mada hii ianze?..
Hakuna system ambayo iko 100% laa sivyo tusingekuwa na vyama vyenmye mirengo tofauti... Swala la Mafisadi nchini ni swala la KIONGOZI mkuu wa nchi ambaye kashindwa kuchukua hatua kisheria kwa sababu mhalifu hapa ni mzazi ama toto wake mwenyewe allomzaa kisiasa..
WE do understand position na uwezo wa JK hadi sasa hivi kwa hiyo tunahityaji kiongozi mwingine mwenye uwezo wa kuwawajibisha wale wote wanaohujumu nchi kwa kuweka sheria kali ambazo zitafuatiwa na utekelezaji wa sheria hizo.
JK kashindwa IKULU na kwa mara ya kwanza maneno ya Mwalimu kuwa IKULU sii kiti cha kuchezea imeanza ku sink in ktk fahamu zetu.. Tunataka kiongozi ambaye kuongoza watu millioni 40 ni ktk uwezo wake. Kuongoza Tanzania akiweka malengo mbele ya Uhuru tuliopigania toka kwa mkoloni na yeyote anayetaka kupotosha malengo hayo ni adui wa Uhuru huo...
Sasa huyu kiongozi awe Chjadema, TLP, CUF ama CCM, hili ndilo swala linalotangulia ktk uchaguzi wa mwaka 2010... na hapo ndipo kura za wananchi zitakapoweza kutambua nani anaaminika zaidi na wananchi ktk kufikia malengo haya..Chadema should concertrate on this rather than Majimbo ambayo ni lugha tofauti na PRIME concern ya wananchi. Muhimu Chadema watambue kwamba KUJENGA UCHUMI ndilo swala kubwa ktk mawazo ya wananchi wakitambua kwamba mbegu zao za kuimarisha uchumi huo zinaliwa na viongozi... Majimbo ni sera inayozungumzia zaidi KUGAWANA mavuno na pengine itaeleweka zaidi kama ni mfumo wa Kila mtu (kanda) na mzigo wake!