CHADEMA yaigaragaza CCM

CHADEMA yaigaragaza CCM

Martin Mayala

Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
20
Reaction score
28
Kwa wale mnaoendelea kuaminishwa na propaganda za watawala kuwa CHADEMA kinachukiwa na watu, basi fikirieni upya na jipangeni vizuri kwani moto wa chama unazidi kuwaka na kumulika kila kona. Uchaguzi mdogo wa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Maisaka Kati Jimbo la Babati Mjini mkoa wa Manyara ni kama ifuatavyo

CHADEMA - kura 247
CCM - kura 170
CUF - kura 2

Sasa nyie wafuasi wa Mwigulu mkisaidiwa na Job Ndungai kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa CHADEMA haifai, kwa hilo mmeula wa chuya, jipangeni upya kwani matendo yenu na maamuzi yenu mabaya ya kulinda udharimu wenu Watanzania wa chini kabisa huku mitaani na vitongojini wanaona na wataendelea kuona kama hamtajitambua kwa mbinu zenu chafu na kwa mbinu zenu hizo kila uchaguzi, mtakimbia vituo kabla ya matokeo kutangazwa
 
Hongereni sana kwa ushindi huo mkubwa! Tukaze buti hatimaye nchi itakombolewa tu!!!
 
Sio rahisi mtapaki kuwa wapinzani wazuri tu mpaka mwisho wa dunia
 
Kwa mwendo huu 2015 majimbo ya Babati mjini na vijijini wanaCCM tuanze kuhesabu maumivu.

Kuna kila dalili CCM tutazidi kuendelea kulizwa kanda ya kaskazini na kanda ya Ziwa kila siku.
 
CHADEMA YATOSHA.
Ni kama maji utayaoga au kuyanywa!
 
Nasubiri "misukule" iingie hapa mtaskia.. viva people's power..
 
mnastahili kushinda na wale wanastahili kushindwa
 
M4C ni noma maana CCM huwa wanashinda bila kupingwa dawa ni kila kijiji CHADEMA KUWA na wagombea hongereni sana makamanda
 
hongeleni saaaana chadema mjipange sanasana vijijini watu uelewa wa mabadiliko bado sana.
 
Nimepata faraja kidogo .Kama sio msiba 🙁 ningefanya kasherehe..Mapambano yanaendelea..
 
Back
Top Bottom