Kwa wale mnaoendelea kuaminishwa na propaganda za watawala kuwa CHADEMA kinachukiwa na watu, basi fikirieni upya na jipangeni vizuri kwani moto wa chama unazidi kuwaka na kumulika kila kona. Uchaguzi mdogo wa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Maisaka Kati Jimbo la Babati Mjini mkoa wa Manyara ni kama ifuatavyo
CHADEMA - kura 247
CCM - kura 170
CUF - kura 2
Sasa nyie wafuasi wa Mwigulu mkisaidiwa na Job Ndungai kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa CHADEMA haifai, kwa hilo mmeula wa chuya, jipangeni upya kwani matendo yenu na maamuzi yenu mabaya ya kulinda udharimu wenu Watanzania wa chini kabisa huku mitaani na vitongojini wanaona na wataendelea kuona kama hamtajitambua kwa mbinu zenu chafu na kwa mbinu zenu hizo kila uchaguzi, mtakimbia vituo kabla ya matokeo kutangazwa