inaona aibu! Wako bize kushawishi waliokuwa viongoz wa chadema na juhuisha uanachama wao temporary!
Vijana wa lumumba watakuja mda si mrefu kukwambia chadema imekufa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na ushindi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa katika mtaa wa King'azi B, Kata ya Kwembe, jijini Dar es Salaam.
Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, George Lupia, alisema Chadema kimeshinda nafasi zote hizo dhidi ya wapinzani wake CCM na hivyo kuwa viongozi wa mtaa huo.
Msimamizi huyo alisema kuwa mgombea wa Chadema, Donath Mtemekele, alishinda kwa kupata kura 585 huku wa CCM, Daud Ngaliba, akipata kura 376 na kwamba kura 18 ziliharibika.
Chanzo:EATV radio
Hii kata ndiyo kile kimtaa ambacho marehemu HOLACE KOLIMBA,aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi alikuwa anaishi. Pia Marehemu Williamu Mpiluka ,aliyekuwa mbunge wa Mufindi(CCM) alikuwa anaishi hapo. Nina huhakika familia zao mpaka sasa zinaishi hapo. Pia huku anaishi MANYERERE , pia Shule ya Mama Tibaijuka Babro JOHA girls ndiyo ilipo. Ongera ChademaSio vijana tuu, inashangaza hata wakubwa wao wanaendelea kuwaaminisha watu kuwa Chadema/UKAWA eti ni wafu. Sasa kila uchaguzi wa marudio ukifanyika wanashindwa na bado wanasema hivyo hivyo mpaka inatia mashaka kama kweli mwenyekiti wao alipotoa tahadhari kuwa wajiandae kisaikolojia kama walimwelewa.
Hili ni jambo muhimu sana kuhakikisha kuwa wanaelewa. Hasa Katibu wao mwenezi Nape, naona atafutiwe kabisa Mshauri Nasaha aanze kumpa tuisheni ili aelewe.
Chama kinachoelekea kaburini bado kinaendelea kufanya vitu vyake na kukigaragaza chama chenye uhai mkubwa wa miaka 200 ijayo! Kweli Mungu ni mkubwa.
😛eace: 😛eace: 😛eace:
Haya matokeo ndiyo yale ya mbezi au ni tofauti?
-nauluza tu makamanda.
Chama kinachoelekea kaburini bado kinaendelea kufanya vitu vyake na kukigaragaza chama chenye uhai mkubwa wa miaka 200 ijayo! Kweli Mungu ni mkubwa.
😛eace: 😛eace: 😛eace: