CHADEMA yaicharaza CCM Bumbuli, Tanga

CHADEMA yaicharaza CCM Bumbuli, Tanga

Ndio tatizo lenu. Mkipongezwa kosa, msipopongezwa kosa. Lami ikijengwa kosa, isipojengwa kosa. Mshahara ukiongezwa kosa, usipoongezwa kosa. Washutumiwa wakikamatwa kosa wasipokamatwa kosa. Rais akiongea kosa, asipoongea kosa.

Ili mradi tu mlalamike...

Lakini watu kama nyinyi kwenye jamii hamkosekani, TUMESHAWAZOEA...

Wasikuzingue, ila Pongezi kwa ndogo ndogo na kofia kwani ziliwasaidia makamanda walau kununua maji na msosi ikiwa ni pamoja na kujikinga na jua wakati wa uchaguzi. Tunaomba moyo huo uendelee
 
Halafu kumbe hizi ripoti ni za uongo mbona mleta habari unawahadaa wenzako? Wacha kuwapa matumaini kisha uchaguzi mkuu mkishindwa mnaanza kulalama.
 
Safi sana Makamanda wa Bumbuli Lushoto Tanga kwa kazi nzuri Lol ama kweli Chadema inapendwa hadi Bumbuli basi mpaka sasa Maccm hayana chao,Huraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Chadema
 
Kwa taarifa yako, CUF yako haikuweza kusimamisha mgombea hata angalau kijiji kimoja! Kipute kilikuwa ni ccm Vs CDM!

Tunataka vyama vya siasa viwili tu ccm na chadema ktk nchi yetu. Ccm ameshindwa kazi hivo 2015 tunampa chadema. Akishindwa tunampa ccm tena, akishindwa tunawapa chadema tena. Hakika baada ya miaka 20 tanzania itakuwa inakuwa developed country.
 
Mh naibu waziiri JM upepo huo unakuja unaezua hadi masufuria jikoni
 
Ndio tatizo lenu. Mkipongezwa kosa, msipopongezwa kosa. Lami ikijengwa kosa, isipojengwa kosa. Mshahara ukiongezwa kosa, usipoongezwa kosa. Washutumiwa wakikamatwa kosa wasipokamatwa kosa. Rais akiongea kosa, asipoongea kosa.

Ili mradi tu mlalamike...

Lakini watu kama nyinyi kwenye jamii hamkosekani, TUMESHAWAZOEA...

Hawa hawakujulishwa movie ya Lwakatare? Namna gani CCM, mbona movie imeanza kupoteza soko mara hii tu. Ongezeni ma-movie kibao, labda yatafanikiwa kugeuza mkondo wa uelekeo wa upepo.
 
Hapa ndipo unapoweza kuona uthamani wa kupiga kura,maana ni tofauti ya kura saba tu, hongereni wote mlioipigia kura chadema, hongera kwa kuvunja propaganda za udini na ugaidi wa chama cha zamani
 
BAADA ya hila na mbinu haramu kadhaa kuzuia uchaguzi huru na haki, kuminya demokrasia ya sanduku la kura kuchukua mkondo wake, ikiwemo Mtendaji wa Kijiji cha Kwekitui kuharibu uchaguzi kwa kukimbia na sanduku la kura wiki iliyopita, CHADEMA imeibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, kilichoko Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, kwa kura 196 dhidi ya CCM waliopata kura kura 189.

Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika leo, Jumapili, Aprili 7, 2013.

Hongera za kipekee ziwafikie makamanda wa kijijini hapo, Jimbo la Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, chini ya usimamizi wa Kanda ya Kaskazini. Ndiyo waliopigana na kupiganisha 'vita' hiyo.

Kanda ya Kaskazini kwa kweli inaendelea ku-take off vizuri ambapo uchaguzi wa marudio wa vijini na vitongoji huko Lushoto umekuwa na moja ya majaribio na wameonesha uwezo na mfano wa namna decentralization inavyoweza kufanya kazi nzuri kabisa, bila kusubiri Makao Makuu hata kwa vitu ambavyo vingeweza kufanywa na vipaji vingi vilivyoko ngazi za chini ambavyo CHADEMA ilikuwa haijawahi kuvitumia kwa kiwango kikubwa.

We hopefully look forward kwa kanda zingine kuja kwa kasi zaidi. Ushindani huleta ufanisi. Hili ni moja ya jambo la msingi sana katika dhana hii.

Ufanisi huu, hautakuwa kwenye kushinda uchaguzi pekee. Tutarajie kuona mengi to keep the fire burning.

Ndugu Tumaini Makene-

Salamu. Natumaini huu uzi ni muhimu kwako kwa sababu tu jimbo la Bumbuli ni la Mh. January Makamba. Kabla ya kukupa hongera kwa ushindi wa chama chako, ningependa kujua mafanikio hasa ni nini. Rejea uchaguzi wa kata za mgwashi (Bumbuli) na Tamota (Ushoto) ili kuweza kujipima kwamba kweli wananchi wa Lushoto na Bumbuli wamezikubali siasa zenu za kutokujifahamu. Naamini hapa Tuonaongelea ushindi wa mwenyekiti wa kijiji kimoja. Tusitazame mti mmoja wakati msitu bado mnene.

Nakutakia kazi njema na kutumiwa vyema.

Wako katika kuonyesha ukilaza wa Chadema.

Selemani.
 
Du!

Bora wamepata wa kuwasemea. Maana ni kama vile kabaki Prof. Lipumba peke yake. Vipi ile mliyokopi na kupaste, wakaanzia Arusha iliishia wapi vile. Au jamaa wale wa Lumbumba walihamishia mawazo kwenye mkakati mwingine, wa kupandikiza mamluki BAVICHA na kutengeneza movies.

Mkuu Jabulani, ni ama uko kule au hapa, hakuna option ya tatu kwa siasa za nchi hii tunapoelekea kung'oa mzizi wa fitna.
Daah, operesheni mchakamchaka sio mchezo, kwa kweli imetushinda. Lakini jamani, huku Bara hebu tuachieni Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Temeke. Pale Tarime tutawaachia kwani hata huyo wa CCM alipata asilimia 40, lakini alishinda kwa kuwa tuligawanya kura zetu na ninyi. Halafu namshauri Waitara agombee Ukonga, mitaa ya Kitunda na Kivule jamaa wanamkubali sana, labda kwa kuwa kuna mapoti wengi. kule Tarime muachieni Heche, na sisi hatutamsimamisha Mwera wala mwingine (kumbuka sisi huwa hatugombei sehemu tuliyoshika nafasi ya tatu uchaguzi uliopita)
 
BAADA ya hila na mbinu haramu kadhaa kuzuia uchaguzi huru na haki, kuminya demokrasia ya sanduku la kura kuchukua mkondo wake, ikiwemo Mtendaji wa Kijiji cha Kwekitui kuharibu uchaguzi kwa kukimbia na sanduku la kura wiki iliyopita, CHADEMA imeibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, kilichoko Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, kwa kura 196 dhidi ya CCM waliopata kura kura 189.

Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika leo, Jumapili, Aprili 7, 2013.

Hongera za kipekee ziwafikie makamanda wa kijijini hapo, Jimbo la Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, chini ya usimamizi wa Kanda ya Kaskazini. Ndiyo waliopigana na kupiganisha 'vita' hiyo.

We hopefully look forward kwa kanda zingine kuja kwa kasi zaidi. Ushindani huleta ufanisi. Hili ni moja ya jambo la msingi sana katika dhana hii.

Ufanisi huu, hautakuwa kwenye kushinda uchaguzi pekee. Tutarajie kuona mengi to keep the fire burning.

Hongereni Chadema,kama sijakosea kuna chaguzi ndogo ndogo nyingi ambazo ziko pending?. Nia ya wananchi wengi ni kuendelea kuichagua CDM ili indicator hiyo ya mabadiliko iwaonyeshe CCM kuwa propaganda zao si cho chote si lolote,
 
Back
Top Bottom