ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Nani ataelewa falsafa ya kumkandia Dr Slaa?
Kila mtu anavuna alichopanda...
Nani ataelewa falsafa ya kumkandia Dr Slaa?
Umejitahidi kutoa hongera lkn ni ya kinafiki!
Tabora pia bado wamelala wanahitaji kuamshwa
Hongereni sana Chadema
Hongera Makamba, zimefika kwake wala msijali atakishughulikia hiki chama cha magaidi watanzania wakikwepe kama ukoma.
Hongera Makamba, zimefika kwake wala msijali atakishughulikia hiki chama cha magaidi watanzania wakikwepe kama ukoma.
Ili mradi tu mlalamike....
BAADA ya hila na mbinu haramu kadhaa kuzuia uchaguzi huru na haki, kuminya demokrasia ya sanduku la kura kuchukua mkondo wake, ikiwemo Mtendaji wa Kijiji cha Kwekitui kuharibu uchaguzi kwa kukimbia na sanduku la kura wiki iliyopita, CHADEMA imeibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, kilichoko Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, kwa kura 196 dhidi ya CCM waliopata kura kura 189.
Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika leo, Jumapili, Aprili 7, 2013.
Hongera za kipekee ziwafikie makamanda wa kijijini hapo, Jimbo la Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, chini ya usimamizi wa Kanda ya Kaskazini. Ndiyo waliopigana na kupiganisha 'vita' hiyo.
Kanda ya Kaskazini kwa kweli inaendelea ku-take off vizuri ambapo uchaguzi wa marudio wa vijini na vitongoji huko Lushoto umekuwa na moja ya majaribio na wameonesha uwezo na mfano wa namna decentralization inavyoweza kufanya kazi nzuri kabisa, bila kusubiri Makao Makuu hata kwa vitu ambavyo vingeweza kufanywa na vipaji vingi vilivyoko ngazi za chini ambavyo CHADEMA ilikuwa haijawahi kuvitumia kwa kiwango kikubwa.
We hopefully look forward kwa kanda zingine kuja kwa kasi zaidi. Ushindani huleta ufanisi. Hili ni moja ya jambo la msingi sana katika dhana hii.
Ufanisi huu, hautakuwa kwenye kushinda uchaguzi pekee. Tutarajie kuona mengi to keep the fire burning.
Propaganda za chadema zimeenea sana ila kitaporomoka gafla sana.
Ndio tatizo lenu. Mkipongezwa kosa, msipopongezwa kosa. Lami ikijengwa kosa, isipojengwa kosa. Mshahara ukiongezwa kosa, usipoongezwa kosa. Washutumiwa wakikamatwa kosa wasipokamatwa kosa. Rais akiongea kosa, asipoongea kosa.
Ili mradi tu mlalamike...
Lakini watu kama nyinyi kwenye jamii hamkosekani, TUMESHAWAZOEA...
Hongereni sana Chadema
Sipati picha mtu mzima anatimua mbio na sanduku la kura.....hatareee, hongereni sana makamanda haikuwa kazi rahisi.:rockon: