Ninapenda kwanza kutoa heshima zangu kwa Mheshimiwa Mbowe, aliyekuwa kizuizini, kwa kuonewa na bila kupewa haki yake kama sheria inavyosema.
Nikirudia mada yangu, hivi karibuni tumeona kuwa shughuli zote za hiki chama kikubwa cha upinzani zikihamishwa, kutoka mikoni mwa Ofisi zake za kisheria na mikononi mwa Viongozi wake, na kuhamishiwa kwa wale viongozi waliokimbia nchi kwa usalama wao, na pia kuweka makao makuu ya chama mitandaoni haswa kwenye kipindi cha MARIA SPACE.
Hili jambo linazungumzwa sana na limewabughudhi sana wengi wetu, kwani Chadema ni mali ya watanzania na kina manufaa kwa waliomo na wasiokuwemo, inaumiza kuona Chama kimetekwa Nyara.
Inashangaza sana kuona wale wazee muhimu na wenye busara wa CHADEMA, wamekaa kimya huku wakiona Chama kikiyumbayumba.