CHADEMA yaanika unyama wa kundi la Green Guard ya CCM

Haya yote yanafanyika sasa ama kwa kutaka red brigade ihalalishwe ama green guard ifutwe pia

Walikuwa wapi kutoa huu ushahidi kwa umma tokea kipindi chote hicho wanasubiria sasa ili kutoa tamko?

Miezi miwili iliyopita haya yalikuwa hayazungumzwi!

Siasa.. Ni uongozi wenye kuleta tija sio kupiga domo tu.. Kama wanasiasa wengi wa tz na africa kwa ujumla.
 
Kwa ushahidi wote huu na ukizingatia cdm ina mawakil nguli,kuna haja gani ya kukaa na kulalamika kila kukicha? Ipelekeni serikali mahakamni mara moja
 
kwani ni uongo mkuu? hiyo ndiyo janja ya CHADEMA hivi sasa baada ya kukosa sera kwa wananchi wameona watekeleze uhalifu na kukimbilia makujwaani na kwenye vyombo vya habari kuwa ni ccm na serikali. Huku mitaani siri zimeshavuja tena kutoka kwa viongozi wenu wa matawi.

Mara nyingine muwe mnaona aibu mnaposema maneno kama watu msiokuwa na akili. Hivi tukisema tumtambue aliyeishiwa sera ni nani, cdm au magamba? Hata ungemuuliza mwendawazimu angekujibu kuwa CCM wameishiwa sera na sasa mnatetea ugali wenu kwa kung'oa kucha na meno bila ganzi, kuua, kumwagia tindikali na matendo mengi ya kishetwani! Mngekuwa na sera mngekimbiwa na wanachama wenu na kushindwa kwenye chaguzi mbali mbali? Tumewachoka hamna jipya mnaloweza kulifanya, pisheni tuwape wengine, miaka 51 ya kutuletea hasara inawatosha!
 
The Red Brigades terrorize Italy


On this day in 1974, Italian prosecutor Mario Sossi is kidnapped by the Red Brigades. It was the first time that the left-wing terrorist group had directly struck the Italian government, marking the beginning of tensions that lasted for 10 years.


The Red Brigades were founded by college student Renato Curcio in 1969 to battle "against the imperialist state of the multinationals." At first, the fledgling organization restricted its activities to small acts of vandalism and arson. However, in 1972, they abducted business executive Idalgo Macchiarini, releasing him a short time later with a sign that said, "Hit one to educate 100. Power to the armed populace." The Red Brigades kidnapped several other executives in the years following.


The kidnapping of Mario Sossi marked the first time that the Red Brigades demanded a ransom: They insisted on the release of eight imprisoned members. After fellow prosecutor Francesco Coco agreed to the demand, Sossi was released. However, Coco reneged on the deal and infuriated the Red Brigades.


Over the next several years, the terrorist group kidnapped 26 wealthy men and women to fund their criminal enterprises, extorting as much as $2 million for one abduction. They also got revenge on Coco, killing him in 1976. That same year, 49 members were prosecuted in Turin, prompting several retaliatory shootings against government officials.


In 1978, the ante was upped even further after some of the Red Brigades' leaders were arrested. Aldo Moro, a former Italian prime minister, was kidnapped on March 16, 1978, and five bodyguards were killed in the attack. For 55 days, the terrorists made various demands while taunting Moro's family with fake death announcements. On May 9, after their demands were refused, Moro's body was found in the trunk of a red car in the middle of Rome. He had been shot 11 times in the chest. The Red Brigades killed seven more politicians in the next week, terrorizing the whole country of Italy.


Sixty-three persons ended up being charged with involvement in Moro's murder. Prospero Gallinari, the actual shooter, and 22 others were convicted and sentenced to life imprisonment. The Red Brigades were finally crushed in the early 1980s when over 400 members were jailed.
endeelea kujitoa akili bt soon mtarejea katika uhalisia wenu!!
 
Mboba CCM mna jazba hivi?Anyway hivi kwanini hamtaki Serikali tatu?Mnahofia nini au mnahofia kupigwa bao kirahisi katika Uchaguzi wa Urais wa Zanzibar na Maalim Seif na Dr Slaa kwa upande wa Tanganyika.Amini nakwambia hata mfanyaje CCM lazima itoke madarakani 2015.That's a vow!

Kamanda jazba nizitoe wapi? Hapa burudani tupu!! nyie fungeni ndoa hata na mama zenu hamna mtakachoambulia!
 
Nilishakuonya usijadili threads zangu.

Na nilishasema sitabishana na -------- hata siku moja.

Ninasikitika hata kukujibu kwa sababu huna thamani yoyote ya kujibiwa.

Wewe ------ una thread au unautumbo?? Hivi na wewe unajiona una thamani?? shukuru sana JF unapata hata nafasi kujibishana na waungwana; jifundishe kilimo vinguinevyo 2015 baada uchaguzi ni kuoelewa tu mjini bila kazi shughuli!!
 
WAKATI taasisi ya Kijerumani ikitoa ripoti iliyoainisha ‘madudu’ mengi yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanika matukio yote mabaya yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitumia kikundi cha vijana wake wa Green Guard.


Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, amekitaja kikundi cha Green Guard kuwa cha hatari kutokana na kuhusika na matukio mengi ya kigaidi.


Mnyika amesema matukio hayo yana baraka zote za CCM na serikali kutokana na ukweli kwamba kikundi hicho hakiguswi wala kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola, pamoja na kuhusishwa kwa ushahidi mwingi na matukio mengi.


“Hawa wameshiriki matendo mabaya ya utekaji, upigaji, kujeruhi na yapo ya vifo. Lakini kwa sababu kinafanya haya kwa baraka za CCM na serikali yake, hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya yeyote.


“Tumetoa taarifa nyingi tu na zenye ushahidi wa waziwazi wa kuhusika kwa kikundi hicho, ambacho sasa kinasimamiwa na Mwigulu Nchemba, lakini polisi hao hao wanaotusakama leo kwa vile tumeamua kusema ukweli, hawajachukua hatua zozote dhidi ya yeyote yule,” alisema Mnyika.


Aliongeza kuwa CHADEMA imesema sana kuhusu ukatili huo, lakini katika hali ya kusikitisha viongozi wa siasa wanaojitokeza kulaani hatua ya chama hicho kuamua kutoa mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake, wamegeuka mabubu kuikemea CCM na serikali yake.


Malalamiko hayo ya CHADEMA yanafanana pia na yale yaliyotolewa juzi katika ripoti ya Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani linalojihusisha na utafiti wa masuala ya siasa nchini.


Shirika hilo katika ripoti yake ambayo inadaiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, imeshutumu vikali matukio hayo, huku ikisukuma lawama kwa vyombo vya dola kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na ukatili huo.


Pia shirika hilo limetahadharisha kuwepo kwa uwezekano mkubwa zaidi wa vitendo vya kikatili kwa viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wakosoaji wa serikali kadiri chaguzi zinavyokaribia.


Ripoti hiyo iliyoandikwa na Danja Bergman na Stefan Reith, iliyotolewa tangu mwezi uliopita, inazungumzia matukio mbalimbali yaliyolikumba taifa kwa siku za karibuni, yakiwemo ya mabomu yaliyolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA na Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha.


Hata hivyo, wachunguzi hao wana maoni kuwa ongezeko la matumizi ya mabavu kutoka kwa vyombo vya dola dhidi ya maandamano halali na ukosoaji, ni dalili tu ya mambo makubwa zaidi yanayoweza kutokea katika kipindi cha miaka miwili ijayo, ambayo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.


Ripoti hiyo pia inasema katika hali hiyo, kwa kadiri ya hali ilivyo kila aina ya vitisho, udanganyifu na matumizi ya mabavu vitakuwa vikibadilishwa badilishwa na kutokea katika sura tofauti ikiwemo vurugu ili kupotosha umma, huku watuhumiwa wakishindwa kutambuliwa, na wale wanaotambuliwa watafichwa au kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na mamlaka husika.


Ripoti hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kuwa hata pale vyombo vya dola vinapohusishwa na mauaji, kwa ushahidi wa wazi, watuhumiwa wamekuwa wakilindwa na kuendelea kutesa mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, badala yake wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakishitakiwa kwa kesi mbalimbali za kubambikiza, zikiwemo uchochezi, ugaidi na kuhamasisha chuki kati ya wananchi na serikali yao.


CHADEMA imeorodhesha matukio yanayodaiwa kutendwa na vijana wa CCM kama ifuatavyo:


Juni 16 na Julai 14 katika uchaguzi wa kata nne za Arusha vurugu nyingi ziliripotiwa zikiwahusu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kuteka, kujeruhi na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kusimamia shughuli za ulinzi katika chama hicho kikongwe nchini.

Vijana CHADEMA watekwa


Mkuu wa Wilaya (DC) ya Bunda, Joshua Mirumbe, aliyekaimu nafasi hiyo pia Wilaya ya Serengeti alituhumiwa kuwateka vijana kadhaa wafuasi wa CHADEMA akitumia magari STK 8430, T 286 BFB, T 245 BFE, yanayomilikiwa na CCM pamoja na gari T 352 AHD, T 573 BEW akisaidiwa na askari magereza na kuwapeleka kwenye jengo moja la chama tawala.


Taarifa zaidi zinasema kuwa mkuu wa wilaya huyo alitaka kuwatumia polisi, lakini Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo alimkatalia, hali iliyomlazimu kwenda kuwachukua askari magereza kwa ajili ya kutekeleza operesheni hiyo iliyodumu usiku kucha kabla ya kuwapeleka vijana hao polisi baada ya kubanwa na CHADEMA.


Katika Kata ya Iyela, gari la CCM lenye namba T 704 BEU, likiwa na watu wawili wanaotambulika kwa majina ya Moris na Nosy, waliwateka vijana wa CHADEMA ambapo mmoja wao Meshack Bernad alichomwa kisu.


Pikipiki yapigwa moto


Pikipiki ya CHADEMA ilichomwa moto na vijana wa CCM (Green Guard) na Katibu wa CHADEMA wilaya ndugu, Lucas Daniel amepigwa na kuumizwa, huku mwenyekiti wa jimbo hilo, Kibam Ally Mohamedi akijeruhiwa na katibu Mwenezi Severine Matanila kukatwa vidole.


Risasi za moto


Watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliwafyatulia risasi za moto viongozi na makada wa CHADEMA katika uwanja wa mpira wa Shule ya Msingi Sengerema wakati wafuasi wa CCM na CHADEMA walipokutana kufuatilia hali ya mambo katika vituo vya kupigia kura Kata ya Nyampulukano.


Katika tukio hilo, milio ya risasi zaidi ya nne ilisikika kutokea upande wa pili wa CCM, ambapo magari matatu yalilizunguka gari moja la CHADEMA Kanda ya Magharibi likiwa na kiongozi wa Kikosi cha Movement for Change (M4C), Kanda ya Ziwa Magharibi, Alfonce Mawazo, Hussina Amri na makada kadhaa.


Green Guard waitwa Janjaweed Zanzibar


Kundi hilo lililoasisiwa mwaka 2005 limewahi kuvitingisha visiwa vya Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005.
Wakati wa kampeni za uchaguzi huo vijana wa kundi hilo walipelekwa visiwani humo kwa lengo la kudhibiti nguvu za Chama cha Wananchi (CUF) kwa kuwapiga na kuwatesa viongozi na wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani humo.


Kutokana na vitendo vyake vya vurugu na ghasia za kupiga na kutesa watu, kundi hilo lilipachikwa jina la Janjaweed, likilinganishwa na wanamgambo wa Kiarabu waliotekeleza mauaji ya zaidi ya watu 300,000 huko Darfur, nchini Sudan.


Wabunge wa CHADEMA wakiona cha moto


Juni 17, mwaka huu, vijana wa Green Guard walimshambulia na kumuumiza vibaya mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.


Machi, 2012, wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza, Highness Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemuli wa Ukerewe walivamiwa na kushambuliwa vikali kwa mapanga na nondo na vijana wa Green Guard wa CCM wakiongozwa na mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Ahmed Mkilindi.


Shambulio hilo lilitokea wakati wabunge hao wakiratibu kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kirumba, mkoani humo, ambapo CHADEMA kilishinda.


Wamteka kada


Septemba 28, 2011, Green Guard walimshambulia kada wa CHADEMA Odero Odero wakati mwenyekiti huyo akielekea kwenye kampeni za uchaguzi wa udiwani huko Engototo ambao ulitarajiwa kufanyika Oktoba 2, 2011.


Kada huyo alitekwa na mwenzake aitwae Maganga ambaye alifanikiwa kutoroka na kwenda kutoa taarifa polisi ambao walianza msako wa kumtafuta Odero na kumkuta akiwa ametelekezwa katika pori moja huko Engototo akiwa hoi kwa kipigo huku watekaji wakiwa wameondoka na nyaraka zote alizokuwa nazo.


Wamvunja mbavu mwanachama


Mei 22, 2009, vijana wa Green Guard walimshushia kipigo na kumvunja mbavu mwanachama wa CHADEMA katika Jimbo la Busanda, mkoani Geita. Polisi hawakuchukua hatua zozote dhidi ya kundi hilo la kihalifu.


Washambulia wananchi


Oktoba 25, 2012, vijana wa Green Guard waliwashambulia na kuwaumiza vibaya wananchi wa Daraja Mbili, mkoani Arusha, baada ya kuonyesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA.


Wavamia hoteli


Septemba 24, 2011, vijana wa Green Guard waliokuwa wakipatiwa mafunzo haramu ya kijeshi na kigaidi katika makambi maalumu mkoani Singida, walivamia hoteli waliyofikia viongozi wakuu wa CHADEMA wilayani Igunga wakiwa na gari aina ya Toyota Landcruiser VX mbili mali ya CCM wakitaka kuchoma moto magari mawili ya matangazo (PA).


Jaribio hilo lilishindwa baada ya kudhibitiwa na walinzi wa CHADEMA na kufanikiwa kuwakamata na kisha kuwapeleka polisi, lakini katika mazingira ya kushangaza, vijana hao waliachiwa huru bila kufikishwa mahakamani.


Washambulia mwandishi


Septemba 25, 2011, vijana wa Green Guard walimshambulia kwa ngumi na mateke mwandishi wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Mussa Mkama aliyekwenda katika hoteli waliyofikia viongozi wa CCM ili kuzungumza na mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya (CCM).


Walimshambuliwa kwa maelekezo ya Mwigulu Nchemba, kutokana na mwandishi huyo kuandika habari ya kushikwa ugoni kwa kiongozi huyo wa CCM ambaye katika kampeni za uchaguzi mdogo wilayani Igunga alikuwa meneja wa kampeni za chama chake.


Mwandishi Tanzania Daima anusurika kuchinjwa


Oktoba 4, 2011, mwandishi wa gazeti hili George Maziku aliyekuwa wilayani Igunga kuripoti uchaguzi mdogo wa ubunge, alinusurika kuchinjwa na vijana wa Green Guard wa CCM akifuatilia vurugu zilizofanywa na vijana hao wakitaka kuwadhuru wafuasi wa CHADEMA huku wakiwa wamebeba silaha za jadi, yakiwemo mapanga, visu, nondo, marungu, na majembe.


Maziku alijikuta akiwa amezingirwa na vijana hao ambao hawakutaka kuandikwa maovu yao, wakiwa tayari kumtoa uhai.


Aliokolewa na kiongozi mmoja wa CCM aliyekuwa katika hoteli ya viongozi wa CCM, na kumtoa kwa nguvu kwenye mikono ya Green Guard waliokuwa tayari kumcharanga mapanga na visu.


Tindikali
Septemba 11, 2011, mmoja wa vijana wa Green Guard alikamatwa na kiasi kikubwa cha tindikali na polisi. Ndiyo siku aliyomwagiwa tindikali Mussa Tesha.


Kada wa CHADEMA auawa

Oktoba, 2011, Green Guard walimteka, wakampiga na kumtesa, na kisha kumuua kada wa CHADEMA Mbwana Masudi mkazi wa Dar es Salaam ambaye alipelekwa na chama chake wilayani Igunga kuwa wakala katika uchaguzi mdogo wa ubunge.


Mashambulizi kituo cha polisi
Kiteto (2007) waliwashambulia wafuasi wa CHADEMA ndani ya kituo cha polisi.


Wakata mapanga
Tarime (2008) wanatuhumiwa kuwakata mapanga wanachama wa CHADEMA, na wakafanya tena hivyo Busanda na Biharamulo (2009)


Kambi za mafunzo
Kambi ya vijana iliyofanyika Kijiji cha Ughaugha, mwaka 2005, kabla ya Uchaguzi Mkuu, vijana zaidi ya 200 walikaa wiki sita, chini ya Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Singida Mjini.


Kata ya Unyambwa, katika Shule ya Msingi Ipungi, Kijiji cha Kisasida, chini ya Katibu wa UVCCM wa Singida Mjini, Musa Sunja, kijana kutoka Kata ya Mwankoko na walikaa wiki mbili wakipata mafunzo yaliyoitwa ya ukakamavu.


Kambi iliyoundwa mkoani Mbeya baada ya Mwigulu kufika mkoani humo, iliyokuwa na vijana 376, katika Shule ya Sekondari ya Ivumwe, Kata ya Mwakibete, na walifanya vitendo vya utekaji, kauli iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.


Kambi nyingine kubwa ni ile ya Ulemo, iliyofanyika kwa ajili ya kuhusika na fujo katika uchaguzi mdogo wa Igunga na mmoja wa washiriki amekiri chini ya kiapo mafunzo waliyokuwa wanafanya
 
Back
Top Bottom