Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) muda huu kinafanya mkutano na waandishi wa habari wenye lengo la kuanika taarifa ya CAG juu ya ukaguzi uliofanywa kwa baadhi ya vyama vya siasa.
Mkurugenzi wa fedha Kamanda Antony Komu ndio mzungumzaji mkuu wa press hiyo na anaeleza maswala kadhaa kuhusu ripoti hiyo.
- yanayo jiri
Ndugu wana habari mtakumbuka kuwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya vya siasa na kama ilivyo fanyiwa marekebisho na sheria na 7 ya mwaka 2009 CAG alipewa mamlaka ya kukagua hesabu za vyama vya siasa.
- Mtakumbuka kuwa CAG alitoa ripoti bungeni kwa kusema si vyama vyote vimekaguliwa huku akijua kuwa sheria ina mtaka kukagua vyama vyote ili kutimiza takwa la kisheria.
- Sisi CHADEMA tumeamua kufanya mambo yetu kwa uwazi na hatuna cha kuficha ndio maana tumewaita hapa ili mfikishe ujumbe huu kwa watanzania na wapenda mabadiliko wajue nini CHADEMA kina simamia na kwa nini tumeonyesha kwa vitendo kwa kuweka hesabu zetu hadharani.
- Sisi tume kuwa vinara na mara zote tume simama mstari wa mbele kutaka vyama vikaguliwe (Tukiwemo sisi) ili penye changamoto au dosari zirekebishwe na fedha za walipa kodi zisipotee bure. Tumesimamia msingi huo tukiamini tunaweza kujenga taasisi bora na imara kama ilivyo CHADEMA leo.
- Tuna imani msajili wa vyama vya siasa atachapisha ripoti za vyama vyote kama sheria inavyo mtaka kwa ajili ya rejea ya umma unaolipa fedha hizo.
- Tunajua na tulisema mwaka 2005 CCM ilitumia fedha zilizo kwapuliwa kwenye akaunti ya EPA katika kampeni zake, na hadi leo tuna uhakika mpaka tuna waita na kuanika ripoti yetu kwenu CCM hawaja kaguliwa.
- Anaeleza kwa kwa uundani kilichoko kwenye ripoti hiyo, huku akiwaahidi kuwapatia nakala ya press kwa ajili ya kuwajulisha watanzania kilicho jiri kwenye ripoti hiyo.
- baada ya kumaliza kuelezea maeneo kadhaa yaliyo kwenye ripoti, waandishi wamekabidhiwa nakala ya press conference hiyo kwa ajili ya vyombo vyao nia ikiwa kuwa na taarifa sahihi kutoka ndani ya chama.
- Waandishi wanapewa fursa ya kuuliza maswali.
Ananyoosha muandishi mmoja na kwa kuonyesha ameshiba kwa yale yaliyo elezwa anaulizwa swali kuhusiana na kauli ya chama kuhusu mtuhumiwa wa ugaidi aliye uwawa kwa kupigwa risasi na Polisi.
Muandishi mwingine anauliza kauli ya chama kuhusiana na mkanganyiko wa kauli za Mwanasheria mkuu na raisi kuhusiana na kura ya maoni ya katiba pendekezwa.
Majibu.
Waandishi wana shukuriwa kwa kuelewa kilicho elezwa huku wakisisitizwa kwenda kuuliza kwa nini mpaka leo CCM wamegoma kukaguliwa na CaG aeleze, na watanzania wajulishwe kwa nini hawataki kukaguliwa huku CAG akishindwa kuweka wazi sababu za kushindwa kukidhi takwa la kisheria kukagua chama kikubwa chenye kumiliki kwa hila majengo na viwanja vingi kama ccm.
- kuhusu kuuwawa kwa anayeitwa gaidi, CHADEMA tulisha sema kuwa polisi wana husika na walihusika na milipuko mbalimbali ya mabomu kwenye mikutano yetu ya Arusha, walicho kifanya kwa kumpiga risasi na kumuua mtuhumiwa yule tafsiri yake ni kupoteza ushahidi juu yao maana dhamira haikuonyesha kuwa walitaka kupata taarifa muhimu kutoka kwake kwani mtuhimiwa hakuwa na silaha alikuwa na pingu na bado wamempiga tumboni huku taarifa za awali wakidai walimpiga kwenye makalio.
Anaeleza namna mtuhumiwa alivyo safirishwa usiku na gari moja ya polisi wakati watuhumiwa wote wa ugaidi wa CHADEMA walio wahi kutuhumiwa walikuwa wanasafirishwa chini ya ulinzi mkali wa polisi walio sheheni silaha za kivita na wakati mwingine wakisafirishwa mpaka kwa ndege za jeshi kama la polisi kama ilivyo tokea kwa Mh Mbowe walipo mvamia nyumbani kwake, Henry Kilewo na wenzake pamoja na Lwekatare.
Polisi wanatakiwa kueleza sababu za kumuua mtuhumiwa muhimu wa matukio ya ulipuaji mabomu yaliyo poteza maisha ya watu wasio na hatia. Na kuhusu hilo chama hakita kuwa kimya mpaka haki ipatikane.
- Kuhusu kauli tata kati ya JK na mwanasheria mkuu, wananchi wanatakiwa kuona ni namna gani sasa ombwe la uongozi na viongozi wa serikali ya ccm wasivyo pamoja kutokana na kila mtu kusema lake kwenye maswala mazito ya taifa. Rais anato kauli zake na mwanasheria mkuu naye anatoa kauli zake.
Chadema kinataka kuona daftari la wapiga kura linaboreshwa kabla ya zoezi la kupiga kura ya katiba pendekezwa iliyo patikana kinyume na matakwa ya wengi ili kutoa haki na fursa kwa makundi mengi yaliyo nyimwa fursa hiyo kutokana na sheria kukiukwa kuanzia kwenye chaguzi zilizo pita mpaka sasa.
Na hili tunataka na jaji Lubuva asimamie kauli yake aliyo wahi kuitoa mbele ya vyombo vya habari.
Walau hayo ndio nimeweza kuyaweka hapa kwa muda huu.
Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke.