CHADEMA wazua ghasia mazishi ya Mollel

CHADEMA wazua ghasia mazishi ya Mollel

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung'oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za waombolezaji wafuasi wa chama tawala.

Mollel alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM walionekana wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema.

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo msibani na hivyo kuanza kuzing'oa.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, makada wa CCM waliamua kuzirudisha bendera hizo katika eneo la msiba, safari hiyo ya pili wakiamua kuweka vijana wa kuzilinda.

Mamia wajitokeza kumzika Mollel

Mbali na rabsha hizo, jana mamia ya waombolezaji walijitokeza kumzika kada huyo wa CCM.
Waombolezaji hao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigella, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wakazi mbalimbali wa Arusha na mikoa mingine.

Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani kwake saa 2:00 asubuhi ukitokea Hospitali ya Mt. Meru huku jeneza lake likiwa limefunikwa kwa bendera ya CCM na kufuatiwa na shughuli za kutoa heshima za mwisho.

Askofu Mkuu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Solomon Masangya aliendesha ibada maalumu ya mazishi.

Katika salamu zake, Shigella alisema marehemu atakumbukwa kwa mchango mkubwa wa kuwaunganisha vijana ndani ya CCM na kuwataka wengine kufuata nyayo za marehemu.
Alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo alikuwa akiyasimamia wakati wa uhai wake ilikuwa ni amani, haki na mshikamano ndani ya chama na kuwataka wana UVCCM kuenzi mambo hayo.

Kwa upande wake, Mulongo alisema kutokana na utata wa kifo hicho, uchunguzi wa kina unaendelea na kuwataka wananchi kuwa na subira.

Source: Mwananchi
 
Mwandishi amejitahidi kuipamba habari yake kwa maua aina ya CDM lakini wapi! Imegoma kupendeza kwasababu maua aina ya ccm aliyochanganyia hayachangamani!
 
Vituko hivi..., yaani ccm wanapinga kila ambacho CHADEMA wanafanya....,Eti wanasimika na kupandisha bendera za CHADEMA...!???
 
Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung’oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za waombolezaji wafuasi wa chama tawala.

Mollel alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM walionekana wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema.

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo msibani na hivyo kuanza kuzing’oa.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, makada wa CCM waliamua kuzirudisha bendera hizo katika eneo la msiba, safari hiyo ya pili wakiamua kuweka vijana wa kuzilinda.

Mamia wajitokeza kumzika Mollel

Mbali na rabsha hizo, jana mamia ya waombolezaji walijitokeza kumzika kada huyo wa CCM.
Waombolezaji hao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigella, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wakazi mbalimbali wa Arusha na mikoa mingine.

Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani kwake saa 2:00 asubuhi ukitokea Hospitali ya Mt. Meru huku jeneza lake likiwa limefunikwa kwa bendera ya CCM na kufuatiwa na shughuli za kutoa heshima za mwisho.

Askofu Mkuu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Solomon Masangya aliendesha ibada maalumu ya mazishi.

Katika salamu zake, Shigella alisema marehemu atakumbukwa kwa mchango mkubwa wa kuwaunganisha vijana ndani ya CCM na kuwataka wengine kufuata nyayo za marehemu.
Alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo alikuwa akiyasimamia wakati wa uhai wake ilikuwa ni amani, haki na mshikamano ndani ya chama na kuwataka wana UVCCM kuenzi mambo hayo.

Kwa upande wake, Mulongo alisema kutokana na utata wa kifo hicho, uchunguzi wa kina unaendelea na kuwataka wananchi kuwa na subira.

Source: Mwananchi

KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel
 
ukiwa na pesa,hata kama una dhambi za waziwazi kanisa huzifumbia macho!mfano Nyerere alisema George Kahama ni mkatoliki aliyeendelea ndiyo maana ana WAKE 2.
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel

ndugu yangu hata katika dini zetu za siku hizi kuna ubaguzi mkubwa, ukitaka kuona ukiwa mtoto wa kigogo hata kama hujawahi kukanyaga kanisani utafungishwa ndoa na watu mashuhuri wa kanisa. ukufa utazikwa kwa sala kedekede na kutangazwa kila kona na kwanya utapewa kutumbuiza kutoka kanisani.

sasa kufa wewe mwenzangu na mimi utaulizwa ulikuwa unatoa zaka, unahudhuria vigango au jumuia ulikuwa unaenda kanisani? kama huna majibu ya kueleweka hutapata huduma hiyo iwe ndoa au kifo.
hizi ndivyo tunavyoenda.
japo mungu hakusema popote na yoyote kuwa mtu asipofanya hayo asipewe huduma hizo.
kwa sisi wakristo tena yesu alisema warudishwe kondoo zizini na usimuhukumu mwenzako maana hujui ya kwako.
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel

huu ni unafiki mkubwa sana wa viongozi wetu wadini..
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel
kwa kuwa kulikuwa na watu wazito mkuu.Mungu angeangalia mambo kama hayo walala hoi sijui tungekuwa wapi.?
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel

Habari ndio hiyo. Kwani hujui kuwa hata kwenda mbinguni Siku hizi watakwenda matajiri na wenye madaraka? Fedha kaka ndio sabuni ya roho
 
Wafuasi wa CHADEMA, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung'oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za waombolezaji wafuasi wa chama tawala.

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi wanaosadikika kutoka CHADEMA walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo msibani na hivyo kuanza kuzing'oa.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, makada wa CCM waliamua kuzirudisha bendera hizo katika eneo la msiba, safari hiyo ya pili wakiamua kuweka vijana wa kuzilinda.

My Take: Tuache Unazi wa Kijinga kwenye misiba, Sidhani kama bendera zitasaidia kumpumzisha kwa amani marehemu
 
Kwani huyo kiongozi since wa ccm, sasa hao chadema kwenda kung'oa bendera ilikuwa inawahusu nini?
 
Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung'oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za waombolezaji wafuasi wa chama tawala.

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo msibani na hivyo kuanza kuzing'oa.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, makada wa CCM waliamua kuzirudisha bendera hizo katika eneo la msiba, safari hiyo ya pili wakiamua kuweka vijana wa kuzilinda.

My Take: Tuache Unazi wa Kijinga kwenye misiba, Sidhani kama bendera zitasaidia kumpumzisha kwa amani marehemu

Sasa kama CHADEMA waling`oa bendera zao hao UVCCM wanazing`ang`ania zanini?
 
Kwani huyo kiongozi since wa ccm, sasa hao chadema kwenda kung'oa bendera ilikuwa inawahusu nini?

Mkuu pale sio kwenye mkutano wa siasa, ni mahai pa kuwafariji wafiwa na kumuombea marehemu.....iweje wafiwa wanafarijiwa kwa bendera?
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel

.
Huwezi kumtenganisha farisayo na Herode kufanya hivyo ni sawa na kuutenganisha mwili na roho. Ndiposa Bwana Yesu anasema sii wote waniitao Bwana, Bwana watakaourithi ufalme wa milele.
.
 
Mh! RIP kagamba kadogo. Sisi tulikupenda UZINZI ukakupenda zaidi. Kazi ya shetan ilaaniwe.
 
KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!

Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel

Ndio maana watu wa dini nyingine wanalalamika kuwa kanisa ni sehemu ya ccm, ingawa mfumo wa utawala wa ccm na serikali kwa kiasi kikubwa umejawa na watu wa dini hiyo yenye malalamiko!
 
Back
Top Bottom