KKKT wananishangaza, huyu kafia guest akiwa mtupu lakini kazikwa na Askofu. Wengine wanafariki wachamungu wananyimwa hata mchungaji!
Jamani KKKT fanyeni hivyo kwa watu wote sio baadhi ya watu tu, hukumu na msamaha ni kwa bwana sio wanadamu. RIP Mollel
Unashangaa nini ndugu au hujui maana ya "NENO"KKKT.? maana yake ni KANISA LA KITU KIDOGO TANZANIA!!
Ukitoa tu Kitu Kidogo hata,kama Marehemu alikuwa Jambazi watamzika,! lakini kama huna kitu Watakususia hadi Msiba! Hao ndio KKKT, bwana!!!!
Miaka ya 2007,Rafiki yangu mmoja akiitwa Lukas Ayubu, aliekuwa akijishugulisha na Biashara ya Kuchinja na kuuza nyama maeneo ya Sanawari,alipigwa Risasi na Majambazi,na Bahati mbaya alifariki njiani tukimuaisha HOSPITAL.Marehemu Katika Uhai wake hakuwahi kuoa wala kuishi na mke,lakini Chakushangaza,KKKT hawa hawa walio mzika huyu Kada wa CCM,waligoma kumzika Marehemu Luka Ayubu, eti kwa kisingizio kuwa alikuwa Haudhurii Kanisani na Michango alikuwa hachangii!!
Ajabu mwaka huo huo alifariki Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Arumeru Magharibi Marehemu LUKAS LOISOLO, na Marehemu alikua ni Muumini wa KKKT! ktk maisha yake alikua ni Mume wa wake wawili! Mabishano yalitokea sana kuhusu je azikwe kwa taratibu za Kanisa au ufuatwe taratibu zinazotumikaga kwa watu wa wengine!!
Lakini mwisho KANISA LA KITU KIDOGO [KKKT] Waliamua kwamba pamoja na kuwa Marehemu Alikuwa amevunja amri ya Saba isemayo Usizini,kwa Kuwa na Mke mwingine tofauti na yule wa NDOA! Lakini kwa kuwa alikuwa mchangiaji mzuri Kanisani basi Wamzike kwa Heshima zote za KANISA! na kweli ilifanyika hivyo!
HIYO NDIO KKKT.Usishangae Marehemu Manyata alijiua kwa kujipiga Risasi baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa Muda mrefu, lakini Alizikwa na Askofu!!
Sasa hivi hatuna tena Makanisa yanayohubiria watu "WOKOVU"zaidi sana wanahubiri,na Kufundisha Somo la Utoaji tu!! Yaani Makanisa yanajali zaidi Pesa na sio "ROHO"za Waumini wao!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!