CHADEMA wazidi kujipanga; Wenje Mambo ya Nje

Ni kweli,pia kwa level ya chama sasa Multi-track Diplomacy (kuna kitabu kilichoandikwa na Ambassador John W. McDonald) ni muhimu na kuzingatia kanuni zake katika utendaji wa kurugenzi ya mambo ya nje kwa chama kinachosubiri muda mchache kuchukua dola .Ndiyo maana ukiangalia uchaguzi wa kenya 2007,ODM walikuwa wamejiandaa sana kwa hili na Zambia Patriotic Front.

Ukiangalia Congo-Kinshasa hawa jamaa wa upinzani walishindwa katika hili ndiyo maana hata chama tawala kikawa na uwezo wa kufanya ghiliba kama ilivyoelezwa katika ripoti ya waangalizi wa uchaguzi.Tshisekedi na chama chake walijikita kwenye millitary zaidi na kusahau kanuni ya kinyonga kwenye msingi wa diplomasia 'Hatua za kidiplomasia zina militarism kama background'.Chama tawala kilijua zaidi ya upinzani kujipanga ndani lakini walikuwa hawajaandaa kuwashawishi jumuiya ya kimataifa na kuweka mechanism za kuungwa mkono hata kama watawafanyia ufedhuli/uchakachuaji.

Kama unapenda kusoma vitabu jaribu kutafuta hivi vitabu (Stone, Diane. (2004) 'Private Authority, Scholarly Legitimacy and Political Credibility pia kuna virtabu hivi 'Think Tanks and Informal Diplomacy', by Timothy J. Sinclair '

Ben twend mbele turudi nyuma unaonekana ulikuwa umejiandaa vya kutosha kupewa hayo madaraka ama mengine sawa na hayo! Unaonekana unaongelea kwenye corridor za UN pale New York City ambapo watu huwa wanapigana vikumbo kuhakikisha diplomasia zinafanya kazi kwa kuwaghilibu wengine kidiplomasia! Mkuu unaonekana umezama kwenye Diplomasia ya Kimataifa. Tatizo ni kwamba kuna siasa za vyama vyetu ambazo hazitaki diplomasia bali mtulinga. Ukiwa mwanadiplomasia unaonekana mwoga ukiwa wa mtulinga bila hoja unaonekana shujaa!
 
Hongera Wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na CCM kwamba mtu ni Mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. CDM ingejitofautisha na CCM kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, Mnyika, Zitto Wenje, Mnyika, Zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.
Hawana watu wengine ndo maana unawaona hao hao akina zito, mnyika, wenje. Wenje hana jipya nafasi hiyo angeiweza vizuri John Mrema
 
Ben twend mbele turudi nyuma unaonekana ulikuwa umejiandaa vya kutosha kupewa hayo madaraka ama mengine sawa na hayo! Unaonekana unaongelea kwenye corridor za UN pale New York City ambapo watu huwa wanapigana vikumbo kuhakikisha diplomasia zinafanya kazi kwa kuwaghilibu wengine kidiplomasia! Mkuu unaonekana umezama kwenye Diplomasia ya Kimataifa. Tatizo ni kwamba kuna siasa za vyama vyetu ambazo hazitaki diplomasia bali mtulinga. Ukiwa mwanadiplomasia unaonekana mwoga ukiwa wa mtulinga bila hoja unaonekana shujaa!

Kimbunga,

Hahahaha....Asante kamanda!

Hapana mkuu,ukiangalia dhana ya "muti-track Diplomacy" inavyotoa muongozo inafit sana katika vyama au asasi za kiraia hasa zile zinazokabiliana na vyama dhalimu kama CCM ambayo iko tayari hata kutumia raslimali za taifa ili kupata uungwaji mkono kwa jumuiya ya kimataifa.Safari hii vyama kama CCM ni lazima vishindwe katika hili

Kuhusu suala la maandalizi:Ni kwamba nimetumia muongozo wa tuliyofundishwa na tuliyo-apply katika mazingira ya kazi na kuleta ufanisi.Kwa wanafunzi wa mwaka wa pili wa Masters hilo nililoongea siyo geni hata kwa wanafunzi wa bachelor ni lazima walipewa intro. kwenye multi-track diplomacy.( soma kitabu kilichoandikwa na Louise Diamond,Ph.D .The Institutionalization of Polarization ,Recognizing Healing as the Key to Transformation,pia soma Maintaining Flexibility in the Face of the Unknown)

Kwa siasa zetu watu wakipiga mitulinga (millitary background) basi ni lazima kuwe na Diplomacy kama front object.
 
bora umeliona, utadhani wengine hakuna. Kuna watu wanafanya kazi, lakini hawana nafasi ya kiutendaji nadani ya chama. Hao wangetumika kuimarisha chama. Mifano ni wale wote waliogombea nafasi mbalimbali za ubunge, hao ni mhimu kwani licha ya kuwa viongozi, itawatia moyo wa kujipanga kwa uchaguzi unaofuata.
mwenye nacho anaongezewa mkuu
 
Nilishatanguliza pongezi kwa Wenje.Kwa Chadema sasa ni wakati wa kuishauri na kuishinikiza serikali kuhusu mabadiliko kwenye sera yetu ya Mambo ya Nje.Sera ya mambo ya nje tuliyo nayo ni shallow mno

Balozi zetu nje zimegeuka kijiwe cha watoto wa vigogo na maofisa wastaafu serikalini au wale waliokataliwa na wananchi (kama hisani au kitengo cha kujifutia machozi) bila kuzingatia taaluma.Career Diplomats hapa Tanzania hawapewi majukumu hayo,hii ni changamoto kubwa kwa wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa.Mlioko nje ya nchi mnaelewa hali halisi kwenye balozi zetu

Diplomasia ya uchumi bado tunaitafsiri na kuitekeleza vibaya.Tunaichanganya na diplomasia ya kuomba na kushukuru.Haya ni mambo yaliyopitwa na wakati.Our embassies abroad especially in Europe, America and Asia are to focus more on investment policy to our domestic agenda. We now tie our foreign policy to our domestic agenda. Our interaction with foreign dignitaries should be investment-driven and less of politics

Ni lazima sasa tuwe na sera zinazolenga bara fulani na pia tuwe na special zones.Tuwe na sera zilizotafsiriwa vyema katika utekelezaji.Ushawishi wa Tanzania katika nyanja za kimataifa umeshuka sana ingawa tunao wanadiplomasia wenye rekodi iliyotukuka.Tunao akina Dr.Salim Ahmed Salim,Ambassador Mwapachu,Mahiga na wengine.Tuweke sera itakayotafsiriwa katika faida za kiuchumi ili pamoja na sera nyingine murua tuwe na ushawishi katika bara la Afrika(ingawa najua nguvu ya kiuchumi inachangia katika ushawishi).

Our foreign policy must be defined in terms of the goals our nation need to officially seek to attain abroad, the culture and values that bring about those objectives and the instruments necessary to pursue the goals while taking into account other nation's prevailing foreign policies that may be established against our national interest. The essential tripods of our foreign policy strategy must be linked together such that they add value to our nation. Unfortunately for Tanzania, our foreign policy is static, unprogressive and is not benevolent to most Tanzanians.

Ukiangalia hata balozi zetu nje zinavyoshughulikia maswala yenye maslahi kwa taifa na wananchi wake,utagundua wanafanya kiujanja ujanja na mara nyingi Interest za taifa na wananchi hazitiliwi maanani ukilinganisha na balozi za nchi nyingine.Perhaps, it is not surprising why a citizen of one nation is patriotic while a citizen of another work against the interest of his nation; why a citizen of one nation exhibits political fervor while citizen of another nation shows political apathy; and why a citizen of one nation is very passionate about his country while the citizen of the other looks for every available moment to make caustic statement about his country.

Tanzania's foreign policies have historically exhibited stagnancy, political favoritism, sometimes involve political cronyism, clueless diplomats who have no idea of their functional responsibilities which is to represent Tanzania well in times of joyous ceremonies, defending the nation in hostile environment from a hosting nation, protesting citizens' human right abuses in the countries where such human right abuses take place, chastising nations that flout citizen's human rights and feverishly defending Tanzania's national interests.

Pia tuhakikishe tunaishinikiza serikali inatoa misimamo kwa uwazi kwenye mambo ya kimataifa na yenye maslahi kwa taifa letu.Covertly,ni muda wa kuunda sera inayoendana na wimbi la mabadiliko duniani hasa kipindi hiki ambacho China anaibuka kama taifa lenye nguvu duniani

Kwa upande wa maslahi ya chama hasa muda huu tunaojiandaa kuchukua Dola 2015,kuna mambo mengi ya kuweka sawa kidiplomasia .haitakuwa jambo jema kama nitayaandika hapa kwa sasa.Ila tu tujiandae kikamilifu

Duhh! kweli hii ni five star Master's in International Relations.Ila Chadema mtatuletea balaa.Mnaanza kupanga watu wa propaganda na kuwaaminisha mabalozi kwamba mmechakachuliwa 2015.Ben ninavyokujua hii ndiyo kazi yako haswa.propagandah.Ila huwa navutiwa na uchambuzi wako pamoja na kwamba najua wewe huna tofauti na Odinga ,naona tangu siku ile hujapost humu au ndiyo maombolezo yenyewe?

 
Duhh! kweli hii ni five star Master's in International Relations.Ila Chadema mtatuletea balaa.Mnaanza kupanga watu wa propaganda na kuwaaminisha mabalozi kwamba mmechakachuliwa 2015.Ben ninavyokujua hii ndiyo kazi yako haswa.propagandah.Ila huwa navutiwa na uchambuzi wako pamoja na kwamba najua wewe huna tofauti na Odinga ,naona tangu siku ile hujapost humu au ndiyo maombolezo yenyewe?


Ben Ulipost hapa ukaandika na sikuiona post tuliyojibizana jumamosi jioni"


Nuclear,

Kama huna cha kuchangia ni bora ukae kimya.Watu tuko kwenyemaombolezo bado na kwa post yako hii naona umepata fursa kwa kutojua ya kuonyesha jinsi ulivyo na inhumanity katika matatizo ya kawaida ya kibinadamu.nilitarajia kwa kiwango chako cha taaluma ungeweza kutuma post ambayo ni makini zaidi kuliko hii bila kukwaza watu/kikundi chochote katikajamii fulani.Umenidissapoint sana,na ni fedheha kujihusisha au kusema unanifahamu katika muktadha wa kitaaluma .Mtu makini anaweza kujiuliza kama assesment/endorsement ya mtu kama Nuclear inaambatana na contents za aina hii kwenye post,iweje Ben Saanane aonekane makini?

Kwa hiyo nimegundua ni janja yako ya kunichafua na kutekeleza lengo/malengo yenu maovu dhidi yangu kwa sababu mnazozijua ninyi na kundi lenu ndani ya chama chenu mnachokijua.Ni jambo la kushangaza sana nanyi ati leo mna termerity ya kuongelea masuala ya international relations wakati ninyi mkiwa kwenye nchi za watu mlikuwa mnajiita South Africans kitu ambacho kwangu niliona ni upuuzi mtupu mtu kukana asili yako.

Mlipokuwa mnashirikiana na wakenya kuvuruga uchaguzi hamkujua kwamba mambo yatawageukia.matokeo yake bado mna maumivu hadi sasa.Let us move forward,tuijenge Tanzania hata kama tuko ndani ya vyama vyenye itikadi tofauti.Kama una alternative way ya ku-redefine foreign policy yetu ilete hapa ijadiliwe.tusiwasaliti wale ma-profesa wetu waliyokuwa wanatufundisha

Najua nimesomeshwa na serikali ya Tanzania kwa gharama ya walipa kodi,lakini pamoja na wewe kusomeshwa na wazazi au taasisi yoyote hakutuzuii kulisaidia taifa letu,hakunizuii kuwa mwanachama wa chama cha siasa.Mengine uliyoandika in-box nitayajibu accordingly lakini matusi nitakuachia mwenyewe.That's too low for me !

NB: Kama unavutiwa na uchambuzi wangu basi rudi kwenye mjadala husika"
 
Duhh! kweli hii ni five star Master's in International Relations.Ila Chadema mtatuletea balaa.Mnaanza kupanga watu wa propaganda na kuwaaminisha mabalozi kwamba mmechakachuliwa 2015.Ben ninavyokujua hii ndiyo kazi yako haswa.propagandah.Ila huwa navutiwa na uchambuzi wako pamoja na kwamba najua wewe huna tofauti na Odinga ,naona tangu siku ile hujapost humu au ndiyo maombolezo yenyewe?


Nuclear1,

Balaa hailetwi na chama cha upinzani.Kwa taarifa yako historia ya vyama tawala Afrika haiwapi CCM nafasi ya kuwa chama kilichoshindwa uchaguzi na kikaondoka kwa Heshima.Nenda Ivory-Coast,Zimbabwe,Kenya na kwingineko.Wajifunze kutoka Ghana na Zambia.Ni kweli sijapost huku tangu J'mosi.Nilijiwekea azma ya kutopost kitu chochote kisichohusiana na maombolezo ya kamnada na Rafiki yangu Regia mtema hadi siku 7 ziishe.Kwa hayo mengine tafadhali acha upotoshaji.
 
Back
Top Bottom