CHADEMA wazidi kujipanga; Wenje Mambo ya Nje

mabadiliko ya Wenje na Mnyika ni kuongeza mshikamano zaidi.nafikiri mambo yataenda kwa ufanisi zaidi na majungu mwisho! Akina Saasita Watapumua sasa!!
 
ana maana uchagani, umasani, umburu, ujaluoni, usukumani, ukuryan- wote wanapatikana kaskazini mwa tanzania

Kwa hiyo, wanaoteuliwa watoke wapi? Watu wengine kila kukicha ni kujaribu kufikiria ukabila tu badala kufikiria kupunguza changamoto za maisha.
 
Hongera Wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na CCM kwamba mtu ni Mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. CDM ingejitofautisha na CCM kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, Mnyika, Zitto Wenje, Mnyika, Zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.

Nikweli, CDM inabidi wajitofautishe na ccm kwa kuwanagalia vijana ambao ni makini. By the way nampongeza wenje.
 
mi nadhani wangewatumia wale walioshinda ubunge lakini kwa hila za CCM wakapigwa chini. Karagwe yupo mmoja, kasulu magharibu yupo mmoja, kigoma mjini yupo mmoja, kahama yupo mmoja, shinyanga yupo mmoja. unaweza kuwataja wengine kama unawakumbuka. Hata ylue kashindye wa Igunga kwa bi fatuma.

Kuwapo uongozi wa chama, kutawajenga zaidi, halafu kwa kuwa walikuwa wamekubalika, hata wakiita mikutano ya hadahra wataitikiwa kwa nguvu kubwa kwani tayari wana wapenzi wengi, ni hii ndo itakuwa fursa pekee kwao kujitangaza, na kutangaza sera za chama kwa wananchi katika maeneo yao
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua Mheshimiwa Ezekiah Wenje (Mb) kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa chama; uteuzi huo umeanza tarehe 1 Januari 2012. Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa ameeleza kuwa pamoja na uteuzi huo Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa. Kwa uteuzi huo, Wenje anajaza nafasi iliyokuwa ikitumikiwa na Mheshimiwa John Mnyika (Mb) ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia fursa hii kusisitiza rai iliyotolewa na chama kwa umma, watanzania na wanachama kutambua kwamba katika kusimamia vipaumbele vya kisiasa, kiuchumi na kijamii vya taifa na chama; CHADEMA kimejipanga kutimiza wajibu wa chama mbadala na chama kikuu cha upinzani nchini katika mwaka 2012 kwenye vyombo vya uwakilishi ambavyo chama kina wajumbe wa kuchaguliwa na katika ngazi mbalimbali za chama.

Aidha, pamoja na kutumia mikutano ya maamuzi ya kiserikali na kichama CHADEMA inawajulisha watanzania kwamba chama kitaendelea kutumia pia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha umma wa Watanzania, katika kuwezesha uwajibikaji wa serikali na viongozi wake na kuchochea maendeleo ya watu.

Hivyo, wananchi watarajie CHADEMA kuendelea na ziara katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa mujibu wa ratiba itakayotangazwa na kamati kuu ya chama ambapo kwa mwaka 2012, vipaumbele vikuu ni kuboresha mchakato wa mabadiliko ya katiba ili Tanzania iwe na katiba mpya na bora.

Kipaumbele cha chama katika nyanja ya uchumi ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi na mfumko wa bei na kuongeza uzalishaji. Katika masuala ya jamii ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo au viashiria vya matatizo.

Kurugenzi pia inapenda kusisitiza umuhimu wa serikali kujibu (au kufanyia kazi) hoja za matatizo ya kiuchumi yanayowakabili Watanzania kwa sasa, zilizotolewa na Katibu Mkuu Dkt. Wilbroad Slaa katika tamko la mwelekeo wa CHADEMA kwa mwaka 2012, sambamba na zile zilizotolewa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Kabwe Zitto kuitaka serikali kupunguza matumizi ya kawaida na kuongeza matumizi ya maendeleo, masuala yaliyopendekezwa na CHADEMA katika Bunge la Bajeti, kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni.

Aidha, CHADEMA inaendelea na maandalizi kwa ajili ya ushiriki mzito wa chama katika chaguzi mbalimbali za marudio zilizojitokeza na zitakazoendelea kujitokeza katika ngazi mbalimbali.

Pia, pamoja na kuunganisha umma kuhamasisha demokrasia na maendeleo kwa maslahi ya taifa; mwaka 2012 ni mwaka wa kuanza kwa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya msingi, matawi na kuendelea mpaka uchaguzi wa ngazi ya taifa utakapofanyika mwaka 2013 kwa ili ya kujenga oganizesheni thabiti ya chama nchi nzima.

Kwa upande mwingine;
CHADEMA inawatakia Wazanzibar, Watanzania wapenda demokrasia na maendeleo wote, heri katika maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inapaswa kutumika kutafakari kuhusu mwelekeo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, msisitizo ukiwekwa katika kutafakari, kutafiti na kubaini vyanzo hasa vya matatizo yetu kama jamii inayotaka kufikia maendeleo na ustawi ulio bora kwa maisha ya watu wake, badala ya kutafuta visingizio, kushughulikia matokeo ya matatizo hayo.

Imetolewa na:

Tumaini Makene
Afisa Habari CHADEMA
12/01/2012
 
Kuna watu wengi sana ambao wangeweza ku-focus kwenye hiyo kazi.
Dr.Slaa hapa you're wrong.
Mtu mmoja kazi miamoja,hapo hapo mna mlaumu kikwete kumteua
Mbunge kuwa mkuu wa mkoa kweli?
 
mi nadhani wangewatumia wale walioshinda ubunge lakini kwa hila za CCM wakapigwa chini. Karagwe yupo mmoja, kasulu magharibu yupo mmoja, kigoma mjini yupo mmoja, kahama yupo mmoja, shinyanga yupo mmoja. unaweza kuwataja wengine kama unawakumbuka. Hata ylue kashindye wa Igunga kwa bi fatuma.

Kuwapo uongozi wa chama, kutawajenga zaidi, halafu kwa kuwa walikuwa wamekubalika, hata wakiita mikutano ya hadahra wataitikiwa kwa nguvu kubwa kwani tayari wana wapenzi wengi, ni hii ndo itakuwa fursa pekee kwao kujitangaza, na kutangaza sera za chama kwa wananchi katika maeneo yao

Hata yule mwalimu wa Igunga inamaana hafai?
Au hadi angekuwa mbunge kwanza?

Hata kina wenje,Mnyika,Zitto nao ni wanafiki tu.
We utakubali vipi kuwa naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,
Wewe huyo huyo naibu katibu mkuu wa chadema,wewe huyo huyo waziri kivuli.
The same goes to wenje,mnyika,...najua mnachungulia humu,.....jueni nyinyi ni waroho wa madaraka.

Mwalimu wa watu Igunga mlinadi kweli kwamba anaweza kazi,kapoteza ajira yake.
Yes,najua hamlipani,...lakini mpeni nafasi kama hiyo azoee uongozi basi.LOL WAROHO NYIE
 
Kuna kijana aliye gombea mara mbili ubunge kule Busanda,he is smart.
Hadi awe mbunge ndo mumuone?
 
Ben wa saanane,...
mambo kama hayo ya uhusiano wa kimataifa yanamfaa sana.
Nae hadi awe mbunge?
Mbona hamkuzi vipaji nyie chadema?
Slaa au kuna rushwa kwenye kuteuana?
AAAAAH DR.SLAAAAAA
 
Hongera Mh: Wenje kwa uteuzi huo. Kumbuka cheo ni dhamana na uwajibikaji katika upendo, akili na nidhamu.
 
Kuna watu wengi sana ambao wangeweza ku-focus kwenye hiyo kazi.
Dr.Slaa hapa you're wrong.
Mtu mmoja kazi miamoja,hapo hapo mna mlaumu kikwete kumteua
Mbunge kuwa mkuu wa mkoa kweli?

Viongozi wa CHADEMA walishasema muda mrefu, wabunge wao wakiteuliwa nafasi za chama huwa hawalipwi. Hivyo unaweza ukawa pia ni mkakati wa kupunguza matumizi ya chama. Wenje kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Mbunge napongeza uamuzi wa chama kumteua kwa kuwa atakuwa ana uzito kwenye mikutano ya kimataifa na pia anaweza kukutana kirahisi na mabalozi. Nashauri chama sasa kiteue afisa wa mambo ya nje kijana ambaye atafanya kazi kila siku ofisini. Naona wamezingatia ushauri huo kwa upande wa Mnyika wamemteulia afisa habari, nimeona hapa jina lake kuwa ni Tumaini Makene, nakumbuka huyu kamanda aliwahi kuwa mwanandishi wa habari. Wateue kijana mwenye utaalamu wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ili amsadie Wenje kiutendaji. Huyo afisa ndiye alipwe na chama miongoni mwa vijana wahitimu wa vyuo.

Serayamajimbo
 
Mnaboa,be innovative please.
Tumechoka kusikia majina yale yale kila siku.
 
Hauwezi kukwepa gharama kwenye siasa.
Wao wenyewe chadema huwa wanashawishi vijana kwa kuwaambia kwamba
gharama ya ukombozi ni kubwa sana.
Yes,kama ni kubwa basi wamteue mtu atakae shika wadhifa wa mambo ya nje na
mshahara wake wapunguze 3M toka kwa Dr.Slaa wampe.
Simple,siasa ni gharama,tugawane umaskini katika ku-manage gharama hizo.

Huwezi sema tatizo ni gharama ndo uchague magalacha kuongoza chama wakati
kuna watu wa maana kabisa.Ubunge tu huko nyamagana una mpelekesha,bado mna muongeza
mambo ya nje kweli?
 
Halima Mdee, Leticia Nyerere, Esther Matiko na Regia Mtema wote hawafai kweli? Au ile sera ya CCM ya Spika kwenu haifai? Dr Slaa, huku nje wabaya wako wanasema teuzi zako zimekaa kikatoliki sana ambako Ma-Cardinals, ArchBishops, Bishops na Padres wote ni wanaume!
 
Hongera Wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na CCM kwamba mtu ni Mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. CDM ingejitofautisha na CCM kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, Mnyika, Zitto Wenje, Mnyika, Zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.
Kimbunga ndugu yangu,hoja yako naona ni nzito na muhimu sana. Ila nadhani sababu ya kufanya hivyo kwa sasa ni kuwa vyeo hivyo ndani ya chama vikitumikiwa na wabunge watakuwa hawalipwi na Chama kwani wanamishahara ya ubunge kwa sasa,na ukiajiri mtu mwingine atahitaji mshahara na CDM sio kama CCM hakina vyanzo vya kutosha vya mapato. Kwa sasa wacha vijana wabunge wajitolee kufanya kazi hizo ila iwe kwa ufanisi
 
kuna kijana aliye gombea mara mbili ubunge kule busanda,he is smart.
Hadi awe mbunge ndo mumuone?

ujinga mwingine huu. Ni kweli mwanasiasa anachosema kweli huwa ni jina lake tu, japokuwa wengine wametudanganya. Lakini kwa usafi wa roho na akili, ni wale wale akina mbatia, seif, kikwete, na wengine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom