CHADEMA wazidi kujipanga; Wenje Mambo ya Nje

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho. Anajaza nafasi iliyoachwa wazi na John Mnyika aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alisema jana kuwa pamoja na uteuzi huo, Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Hongera Chadema.





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua Mheshimiwa Ezekiah Wenje (Mb) kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa chama; uteuzi huo umeanza tarehe 1 Januari 2012. Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa ameeleza kuwa pamoja na uteuzi huo Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa. Kwa uteuzi huo, Wenje anajaza nafasi iliyokuwa ikitumikiwa na Mheshimiwa John Mnyika (Mb) ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia fursa hii kusisitiza rai iliyotolewa na chama kwa umma, watanzania na wanachama kutambua kwamba katika kusimamia vipaumbele vya kisiasa, kiuchumi na kijamii vya taifa na chama; CHADEMA kimejipanga kutimiza wajibu wa chama mbadala na chama kikuu cha upinzani nchini katika mwaka 2012 kwenye vyombo vya uwakilishi ambavyo chama kina wajumbe wa kuchaguliwa na katika ngazi mbalimbali za chama.

Aidha, pamoja na kutumia mikutano ya maamuzi ya kiserikali na kichama CHADEMA inawajulisha watanzania kwamba chama kitaendelea kutumia pia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha umma wa Watanzania, katika kuwezesha uwajibikaji wa serikali na viongozi wake na kuchochea maendeleo ya watu.

Hivyo, wananchi watarajie CHADEMA kuendelea na ziara katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa mujibu wa ratiba itakayotangazwa na kamati kuu ya chama ambapo kwa mwaka 2012, vipaumbele vikuu ni kuboresha mchakato wa mabadiliko ya katiba ili Tanzania iwe na katiba mpya na bora.

Kipaumbele cha chama katika nyanja ya uchumi ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi na mfumko wa bei na kuongeza uzalishaji. Katika masuala ya jamii ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo au viashiria vya matatizo.

Kurugenzi pia inapenda kusisitiza umuhimu wa serikali kujibu (au kufanyia kazi) hoja za matatizo ya kiuchumi yanayowakabili Watanzania kwa sasa, zilizotolewa na Katibu Mkuu Dkt. Wilbroad Slaa katika tamko la mwelekeo wa CHADEMA kwa mwaka 2012, sambamba na zile zilizotolewa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Kabwe Zitto kuitaka serikali kupunguza matumizi ya kawaida na kuongeza matumizi ya maendeleo, masuala yaliyopendekezwa na CHADEMA katika Bunge la Bajeti, kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni.

Aidha, CHADEMA inaendelea na maandalizi kwa ajili ya ushiriki mzito wa chama katika chaguzi mbalimbali za marudio zilizojitokeza na zitakazoendelea kujitokeza katika ngazi mbalimbali.

Pia, pamoja na kuunganisha umma kuhamasisha demokrasia na maendeleo kwa maslahi ya taifa; mwaka 2012 ni mwaka wa kuanza kwa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya msingi, matawi na kuendelea mpaka uchaguzi wa ngazi ya taifa utakapofanyika mwaka 2013 kwa ili ya kujenga oganizesheni thabiti ya chama nchi nzima.

Kwa upande mwingine; CHADEMA inawatakia Wazanzibar, Watanzania wapenda demokrasia na maendeleo wote, heri katika maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inapaswa kutumika kutafakari kuhusu mwelekeo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, msisitizo ukiwekwa katika kutafakari, kutafiti na kubaini vyanzo hasa vya matatizo yetu kama jamii inayotaka kufikia maendeleo na ustawi ulio bora kwa maisha ya watu wake, badala ya kutafuta visingizio, kushughulikia matokeo ya matatizo hayo.

Imetolewa na:
Tumaini Makene
Afisa Habari CHADEMA
12/01/2012
 
Safi sana Wenje kwa uteuzi huo unafaa sana,kaza buti ukombozi upatikane Tanzania,tupo nyuma yako.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alisema jana kuwa pamoja na uteuzi huo, Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Kwa uteuzi huo, Wenje anajaza nafasi iliyokuwa ikitumikiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa chama hicho kimejipanga kuendelea kutimiza wajibu wa chama hicho kwa Watanzania.

Pia alisema chama hicho kitaendelea kutumia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha Watanzania katika uwajibikaji wa Serikali na viongozi wake na kuchochea maendeleo ya watu.

"Wananchi watarajie Chadema kuendelea na ziara katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa kufuata ratiba itakayotangazwa na Kamati Kuu.

"Kwa mwaka 2012, vipaumbele vikuu ni kuboresha mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili Tanzania iwe na Katiba mpya na bora," alisema Makene.

Alisema kipaumbele cha chama katika nyanja ya uchumi ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha na kuongeza uzalishaji bila kufafanua njia watakazotumia kuongeza uzalishaji huo.

Katika masuala ya jamii, Makene alisema kipaumbele ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo au viashiria vya matatizo bila kuweka iwapo watatumia maandamano na kama yatasaidia kuongeza uzalishaji kama ilivyo katika kipaumbele cha uchumi.
 
Vizuri sana.Wenje anafaa sana.Chama makini na sikivu kwa manufaa ya watanzania
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho. Anajaza nafasi iliyoachwa wazi na John Mnyika aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alisema jana kuwa pamoja na uteuzi huo, Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Hongera Chadema.

Hongera Wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na CCM kwamba mtu ni Mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. CDM ingejitofautisha na CCM kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, Mnyika, Zitto Wenje, Mnyika, Zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.
 
hongera wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na ccm kwamba mtu ni mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. Cdm ingejitofautisha na ccm kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, mnyika, zitto wenje, mnyika, zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.

bora umeliona, utadhani wengine hakuna. Kuna watu wanafanya kazi, lakini hawana nafasi ya kiutendaji nadani ya chama. Hao wangetumika kuimarisha chama. Mifano ni wale wote waliogombea nafasi mbalimbali za ubunge, hao ni mhimu kwani licha ya kuwa viongozi, itawatia moyo wa kujipanga kwa uchaguzi unaofuata.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom