CHADEMA wawe makini zaidi na hujuma za CCM

luhala

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
412
142
Kadiri 2015 inavyosogea CHADEMA inazidi kusakamwa na tuhuma toka kwa wasioitakia heri kwa tuhuma hizi au zile zikiwemo za ukaskazini, migogoro ya ndani na kuhusishwa na ukristo na hivi karibuni wimbi la wanaojitangaza kuwa watagombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Matukio haya; liliwepo lile la waziri kukitabiria "kifo" chama hiki kabla ya uchaguzi ujao yananiaminisha kuwepo mkono wa serikali katika kutengeneza "migogoro" ndani na nje ya chama hiki. Sasa nakumbuka mazungumzo yangu na mmoja wa viongozi wateule wa JK mara baada ya kuapishwa na kuwateua viongozi wake waandamizi ambapo mimi na jamaa yangu mmoja tulikwenda kumpongeza mmoja wa wateule wake hao ambaye tulisoma nae na kufanya nae kazi kwa miaka kadhaa na alibahatika kuteuliwa tena katika nafasi ya uongozi katika serikali ya awamu ya pili ya JK. Baada ya kutafakari sana nimeamua kuyaweka mazungumzo yetu ili ma-great thinkers watafakari na waone kama kuna relation na yanayojitokeza sasa kwa CHADEMA.

Alikuwa jamaa yangu aliyenifahamisha mapema kabisa kwamba rafiki yetu yule alipata uteuzi tena katika awamu hii na kuniasa twende kumpongeza licha ya msimamo wangu wa kuziunga mkono harakati za CHADEMA. Tulikwenda naa kupokelewa kwa bashasha na baada ya mazungumzo marefu yakiwemo ya kumpongeza yeye binafsi kuteuliwa na mgombea urais wao "kushinda" ghaflaalibadilika na kuanza kufoka ifuatavyo:

"Washenzi hawa wametusumbua sana safari hii, wamemsumbua sana mheshimiwa na nasema hu ndiyo mwisho wao. Hatutawapa fursa nyingine tena ya kutusumbua kama walivyofanya safari hii. Kwani wao CHADEMA ni nani haswa, mbona wenzao NCCR tuliwamaliza kianina? Nakwambia 2015 hakutakuwa na CHADEMA wala huyo mnayemwita Dr. Slaa kwani serikali ina mikono mirefu na tumeshajipanga kuhakikisha kunakuwa hakuna usumbufu tena 2015. Nakwambieni huyo Dr. Slaa na hata Mbowe watausikia ugombea urais kwenye bomba tu na tutahakikisha vyombo vyetu vinawavuruga kabisa na huenda hata wasiwepo ifikapo 2015"

Ni baada ya maneno hayo mwenzangu alianzisha topic nyingine iliyotamalaki huku tukigida bia na kutafuna kuku hadi tulipoagana. Toka wakati huo tunawasiliana kwa simu lakini hatuzungumzii siasa.

Kazi kwenu ma-great thinkers kutafakari kama mihemko inayoitwa "migogoro" ndani ya CHADEMA ina uhusiano na remarks za kiongozi huyu mwandamizi.
 
Huyo rafiki yako kama ni kiongozi basi aliropoka hayo kwa mhemko wa kuteuliwa.
-Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro kama ya NCCR-Mageuzi
-Ofcourse Jitihada za serikali na usalama kuisambaratisha Chadema zipo na zinajulikana ila hawatafanikiwa
-Wanaojaribu kuihujumu Chadema pamoja na msajili wa vyama vya siasa.Wasitegemee kuwa vijana chadema tutavua combati,itakua hatari zaidi

-Mwisho huyo rafiki yako(adui wa kizazi hiki na vijavyo) mpe ujumbe kwamba mbinu zao tunazijua na Chadema haitadhurika wala viongozi wake.
-Na Kwa wale wanaotumika kuhujumu Chadema,be warned!
 
Ahsante kwa taarifa inayojitosheleza. Ni wake-up call kwa wanamageuzi wote. Ni kweli NCCR MAGEUZI ilikufa ghafla tena kwa msambaratiko mkubwa huku viongozi wake wakuu wakihamia CCM akiwepo Masumbuko Lamwai.
 
Hiyo itakuwa kweli kwamba wao wangependa kuipoteza ama kuifuta chadema ktk duru za kisiasa ila mungu yuko pamoja na hawa watz wanyonge,
 
Jambo dogo sana ilo,enzi ya NCCR zilikuwa ni zile enzi ya zidumu fikra za mabalozi wa ccm,CKU HIZI HAO MABALOZI WANAIENEZA M4C kinoma..Hawataweza.
 
Huyo rafiki yako kama ni kiongozi basi aliropoka hayo kwa mhemko wa kuteuliwa.
-Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro kama ya NCCR-Mageuzi
-Ofcourse Jitihada za serikali na usalama kuisambaratisha Chadema zipo na zinajulikana ila hawatafanikiwa
-Wanaojaribu kuihujumu Chadema pamoja na msajili wa vyama vya siasa.Wasitegemee kuwa vijana chadema tutavua combati,itakua hatari zaidi

-Mwisho huyo rafiki yako(adui wa kizazi hiki na vijavyo) mpe ujumbe kwamba mbinu zao tunazijua na Chadema haitadhurika wala viongozi wake.
-Na Kwa wale wanaotumika kuhujumu Chadema,be warned!

"Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro"

Naomba mkuu uendelee kutafakari hayo
maneno yako. Naona kama umejiandikia tu bila kuangalia hali halisi ya CDM kwa sasa na migogoro iliyopo.
 
Tunashukuru sana kwa taarifa hii na siyo ya kuifanyia upuuzi hata kidogo kwani hawa mafisadi kwa kweli wana mawazo yanayoendana na maelezo haya. Ila hakika enzi ya NCCR MAGEUZI naona haitajirudia kamwe,kwani wanainchi wanaona wenyewe yanayojiri maishani mwetu! Mi naweza kusema HATUDANGANYIKI tena!
 
Je taarifa hizi zina ukweli wowote au ni tamthilia ambae mtu yoyote anaweza kuitunga ili apate kuungwa mkono kwa anachokiamini kama unaipenda CDM ungepeleka kwa wahucka sio hapa kwani wanasoma wengi hapa hongera kwa tamthilia nzuri na fupi
 
"Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro"

Naomba mkuu uendelee kutafakari hayo
maneno yako. Naona kama umejiandikia tu bila kuangalia hali halisi ya CDM kwa sasa na migogoro iliyopo.

Rejao,
Hiyo ni sheer fantasy.Naifahamu Chadema mkuu,siandiki kwa kubahatisha.

Migogoro ikiwepo Chadema ukaona kimya basi ujue migogoro hiyo ni healthy na inatakiwa iwepo kwenye taasisi yoyote imara.Ikifikia level ya kuhatarisha interest za chama inashughulikiwa fairly and squarely
 
Huyo rafiki yako kama ni kiongozi basi aliropoka hayo kwa mhemko wa kuteuliwa.
-Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro kama ya NCCR-Mageuzi
-Ofcourse Jitihada za serikali na usalama kuisambaratisha Chadema zipo na zinajulikana ila hawatafanikiwa
-Wanaojaribu kuihujumu Chadema pamoja na msajili wa vyama vya siasa.Wasitegemee kuwa vijana chadema tutavua combati,itakua hatari zaidi

-Mwisho huyo rafiki yako(adui wa kizazi hiki na vijavyo) mpe ujumbe kwamba mbinu zao tunazijua na Chadema haitadhurika wala viongozi wake.
-Na Kwa wale wanaotumika kuhujumu Chadema,be warned!

BIG UP. CCM WANAWEWESEKA, WAKAE WAKIJUA CHADEMA C MBOWE. ZITO WALA SLAA, M4C C MBOWE WALA SLAA, HII KITU IKO NYOYONI MWA WATU, NYOYONI MWA VIJANA WAZALENDO NA C WA UVCCM WAZANDIKI, WALA RUSHWA KM BABA ZAO, HATARI NA WAROHO KM FISI, NAAMINI TUTASHINDA KWAN TUMEANZA NA MUNGU NA NDO TUTAMALIZA NAE, WALA RUSHWA NA MAFISADI CCM ALWAYS WAKO NA SHETANI MBWA AWa
 
rejao umenukuu kimakosa,ben kasema chadema imevuka migogoro kama ya nccr na si imevuka migogoro.
kuwa makini na hoja za ma gt tofautio na hapo hatukuelewi.
 
ni kosa kubwa sana kuingia kwenye uchaguzi bila chadema kwani hiki ndio chama pekee kilchotuliza mzuka wa vijana kuinyakua ikulu kwa njia ya maandamano.nasema ni kosa kubwa sana kwani kufuta chama haimaanishi umeufuta upinzani dhidi ya serikali.chadema ikiingia kwenye mgogoro kabla ya 2015 tutarajie vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Mkuu,
Hapa ndipo wanapokosea.Mimi ni mmojawapo
 
Upepo wa mabadiliko huu, hauwezi kuzuiwa kwa chochote! Unapiga kotekote, unawezaje kuzuia mafuriko?
 
ww hujui chadema chama cha kidini kikabila unaona wanavyomhujumu zito kisa iz muslam and not from north
 
Huyo rafiki yako kama ni kiongozi basi aliropoka hayo kwa mhemko wa kuteuliwa.
-Chadema ni chama kikubwa sasa na tumeshavuka level ya Migogoro kama ya NCCR-Mageuzi
-Ofcourse Jitihada za serikali na usalama kuisambaratisha Chadema zipo na zinajulikana ila hawatafanikiwa
-Wanaojaribu kuihujumu Chadema pamoja na msajili wa vyama vya siasa.Wasitegemee kuwa vijana chadema tutavua combati,itakua hatari zaidi

-Mwisho huyo rafiki yako(adui wa kizazi hiki na vijavyo) mpe ujumbe kwamba mbinu zao tunazijua na Chadema haitadhurika wala viongozi wake.
-Na Kwa wale wanaotumika kuhujumu Chadema,be warned!

View attachment 69478 labda CAROLITE ndio itumikayo kuwhujumu kama atumiayo huyo aliyekuwa mke mtu....ambaye amesababisha mumewe wa awali kuogopa kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali na BABU
 
chadema wamepita mapito mengi ya kusakamwa na serikali ya ccm kikubwa wanainchi wa kipindi wameelewa au wanajua adui wao ni nani ndio maana serikali ya ccm itakuja na propaganda mbaya kwa chadema mwisho wa siku zinapuzwa badala yake hupata wafuasi wengi na ungwaji mkono mkubwa.
 
Back
Top Bottom