Elections 2010 Chadema watumie rangi nyeupe pe kwenye mikutano yao!

CHADEMA walipokuwa wakiizindua bendera yao mpya walifafanua wazi kuwa "RANGI NYEKUNDU inamaanisha kuwathamini mashujaa wetu waliokubali kumwaga damu kwa ukombozi wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar)"

Ni usahaulifu wa hali ya juu kama mtu atasema Tanzania ilipata UHURU bila kumwaga damu. Wakati unapozungumzia vita vya ukombozi(kuelekea uhuru), utataja majimaji, mapambano ya Mkwawa, Mirambo, Mangi etc dhidi ya wajerumani na waingereza.

waacheni CAHDEMA watumie rangi wanayoipenda maadamu ipo katika rangi za bendera yao na zina maana kamilifu.

Nina wasiwasi kuwa ipo siku moja katika shughuli za kiserikali nikivaa T-shirt yenye rangi nyeusi matasema ni kama naleta uchuro kana kwamba tuko msibani, mwingine akivaa njano watasema huyu analeta U-yanga-yanga, mwingine kijani naye analeta U-CCM na bluu u-NCCR.

Ni mitazamo yetu tu.
 
Mkuu I second this.

Ukweli ni kuwa rangi inleta mvuto sana katika kusanyiko la watu. I suggest CHADEMA to take thins into consideration; rangi nyekundu huwa ni nzuri san pia kwenye makusanyiko; ubaya wake, CCM wanaweza kubadili maana na kusema wanataka kumwaga damu hawa!!

I think pure white is ideal!!:becky:

Vipi (ikiwa tutaishi katika uoga huohuo) kama wakisema wanavaa rangi ya sanda au mashuka ya hospitali?
 
mwanakijiji umeongea ..................yaani picha ya dk Slaa na magwanda unaweza kujiuliza kama kuna kamanda mpya wa polisi kachaguliwa huna habari!

appearance ya mgombea ni muhimu sana kuwashawishi wapiga kura wasiokuwa na uelewa wa siasa ambao naamini wako wengi sana tanzania.
 
Pure white or the party's coulor but white to dominate and if possible dicard red altogether. CCM wameshaanza kuhubiri mambo ya vurugu kwenye nchi za jirani so any reddish in their colours could jeopardize their position especially in the rural areas where the level of reasoning is low.

I also agree that yale magwanda do not present CHADEMA very well, they do not look nice!
Katika vitu vyote magwanda ndiyo yananihamasisha kuliko kitu kingine chochote!
 
Mimi hayo magwanda nimeshahoji uvaaji wake vya kutosha. Sijui lilikuwa ni wazo la nani tu...
 
Mwanakijiji umeongea ..................yaani picha ya Dk Slaa na magwanda unaweza kujiuliza kama kuna kamanda mpya wa polisi kachaguliwa huna habari!
Appearance ya mgombea ni muhimu sana kuwashawishi wapiga kura wasiokuwa na uelewa wa siasa ambao naamini wako wengi sana tanzania.

Ukitaka kumdhalilisha mtu waweza tumia lugha yoyote hata hii ya kusingizia mfanano na kamanda wa POLISI.
Hivi katka umri ulionao huwezi tofautisha rangi ya kitambaa cha POLISI na kitambaa cha gwanda la CHADEMA?
Je pia huwezi tofautisha hata mshono wake?

Kaazi kwelikweli.
 
Vipi (ikiwa tutaishi katika uoga huohuo) kama wakisema wanavaa rangi ya sanda au mashuka ya hospitali?

mtu yeyote atakayefikiria kuwa wamevaarangi ya "sanda au mashuka ya hospitali" basi atakuwa ana matatizo makubwa zaidi kichwani... think about it.
 
Nakubaliana na hoja yako Mwanakijiji.Rangi moja inaleta uniformity na hamasa kwani mnapokuwa kwenye kikao au mkutano wowote ule mnakuwa mnapendeza sana na kuonekana wengi.Ni wzo zuri ila kwa sasa utekelezaji wake ni mgumu labda kwa siku za usoni.Hivi sasa watu tumekolea na kombati,mimi hivi sasa ninazo 7,za sketi,gauni na suruali na ninazipenda sana kwani zinakupa confidence ya aina yake.Nitajaribu kuwa mfano wa kutengeneza sare nyeupe pe kwa watu wa jimboni kwangu na kuona kama inanoga ila kwangu dongo jekundu hilo sijui kama watazipenda nahisi zitanidodea.

Kilombero For Change(K4C).
 
Duuh!! Kumbe na wewe unatinga hizo kombati sio? Si mchezo.....
 
Nakubaliana na hoja yako Mwanakijiji.Rangi moja inaleta uniformity na hamasa kwani mnapokuwa kwenye kikao au mkutano wowote ule mnakuwa mnapendeza sana na kuonekana wengi.Ni wzo zuri ila kwa sasa utekelezaji wake ni mgumu labda kwa siku za usoni.Hivi sasa watu tumekolea na kombati,mimi hivi sasa ninazo 7,za sketi,gauni na suruali na ninazipenda sana kwani zinakupa confidence ya aina yake.Nitajaribu kuwa mfano wa kutengeneza sare nyeupe pe kwa watu wa jimboni kwangu na kuona kama inanoga ila kwangu dongo jekundu hilo sijui kama watazipenda nahisi zitanidodea.

Kilombero For Change(K4C).

nimekupata sasa wale wananchi wetu kule Kilombero na wenyewe wanayo hayo makombati?
 
Mambo ya uniform haya, japo yanaonyesha umoja (kama mnavyodai), lakini kwa upande wa pili yanaonyesha ubaguzi.

Mimi si shabiki wa uniform mikutanoni. Nillizichukia za CCM toka zamani. Nazichukia pia na za Chadema. Watu wakusanyike mikutanoni wakiwa wamevaa wanavyoweza, na inavyokubalika katika jamii.
 
Hivi kuna mwenye picha ya Nyerere RIP aliyovaa kijani au njano rangi za CCM please atuwekee.

Kwangu sale(uniform) ndicho kitu muhimu zaidi ya rangi ya sale. Lakini kama suala ni rangi, nyeupe naitoa kwenye short listing yangu kwa sababu ya usafi wake.

Mimi nafikiri waendelee na hiyo hiyo nyekundu kwa pindi hiki na waitangaze rasmi kwenye mikutano yao ya kampeni badala ya kutegemea kuwa watu watagundua wenyewe sale ni ipi, ikiwezekana watumie rangi zote Red and Blue. Kuhusu magwanda mi naona yanawafit sana makamanda wala hayaleti utengano wowote.
 
Back
Top Bottom