CHADEMA watoana macho Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA watoana macho Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dume la Mende, Jun 21, 2011.

 1. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeingia kwenye mgogoro baada ya baadhi ya wabunge kupandwa na hasira dhidi ya wenzao wanaoendesha kampeni ya kutaka posho za vikao kwa wabunge ziondolewe.Mkwaruzano huo iliibuka ndani ya kikao cha wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

  Kikao hicho kiliitishwa na kambi hiyyo kwa lengo la kuweka msimamo wa kupinga posho za vikao kwa wabunge, lakini kikageuka uwanja wa vita uliozusha vurumai kubwa kiasi cha kushindwa kufikia muafaka.

  Baada ya kikao hicho kufunguliwa, John Mnyika (Ubungo-Chadema) aliwasilisha hoja hiyo ya kutaka wabunge wa upinzani kuweka msimamo wa pamoja wa kupinga posho hizo ili mkakati huo ulioanzia kwenye Bunge hilo la Bajeti, uweze kufanikiwa.

  Akifikiri ataungwa mkono, Mnyika aliwataka wabunge kuonyesha moyo huo wa kishujaa kwa kutosaini kitabu cha mahudhurio bungeni, lakini wawepo ndani ya vikao.

  Kauli hiyo ya Mnyika ilikuwa sawa na kumwaga petroli kwenye moto unaowaka ambapo wabunge watatu wa Chadema (majina tunayahifadhi kwa sasa) walikuja juu na kupinga vikali hoja hiyo.

  Upinzani huo mkali uliotolewa na wabunge hao ulidhihirisha kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyesema kuwa ingawa baadhi ya wabunge wa chama hicho wanajionyesha kimbelembele kusisitiza mpango huo, wengine wa chama hicho pia wanaumia kimoyomoyo, lakini hawasemi.

  Suala la kukataa posho bungeni lilianzishwa na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema) akisema zinaenda kinyume na mpango wa Taifa wa kupambana na umasikini kwa kuondoa posho zisizo na tija.

  Zitto akionekana kuwa na ushupavu mkubwa ilifikia mahali akaamua kutosaini mahudhurio Bungeni ili jina lake lisiorodheshwe miongoni mwa watakaolipwa licha ya Spika, Anne Makinda kutishia kuwa kitendo hicho kinaweza kumfukuzisha bungeni.

  Mkakati wa Mnyika ulikuwa ni wabunge wote wa upinzani kuwa na mshikamano katika hilo jambo ambalo sasa limeonekena kuwa ni nyongo kiasi cha wengine kutaka kuwararua wenzao wakisema ni msimamo usio na maana.

  Source:
  Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza

  Jamaa wanaweza wakaandamana fasta kupingana wao kwa wao Teh teh
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Narudia kusema wanaokimbilia bungeni hawana msaada wowote na wananchi zaidi ya kujineemesha wenyewe. Hivi si tunawajua wafanyabiashara wakubwa wa upinzani? mbona wao hawathubutu kusema mishahara yao iende kusaidia wapiga kura majimboni mwao kwa kuwa wao wapo kuwatumikia wananchi na wanatosheka na wanachokipata kwenye biashara zao? si tuna mawakili maarufu wanaosimamia makesi makubwa na wanalipwa vizuri? mbona hawapo tayari ku sacrifice mishahara yao ili ilipie watoto mayatima kwenye majimbo yao ada za shule? mil 7 zinaweza kulipia watoto wangapi wa shule za kata?

  Ifike wakati tutambue wanasiasa wapo kwenye siasa kwa manufaa yao na kutafuta protections na sio kwa ajili ya kukutumikia wewe! wachache wana dhamira hizo lakini kipato ni masikini na hawana biashara yoyote ndio maana wanapigania hizo posho.
   
 3. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimekusoma mkuu
   
 4. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Hii habari iko kishabiki zaidi, source not disclosed.

  Rating 0.4/10.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mbona sioni macho yaliyotoka kusaini au kutosaini ndiyo kutoana macho.
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wanaoishabikia cdm habari hii wataipotezea kwa kuwa inawataka wafunguke macho ilhali wao wamefumba na wapo usingizini. Mimi binafsi siamini mabadiliko kwa kutumia siasa ingekuwa ukiwa ccm hukai kwenye foleni barabarani basi ningeingia ccm leo na ingekuwa ukishabikia cdm hukatiwi umeme basi sasa hivi ningefanya juhudi za kuingia chamani. Ukweli utabaki uwe ccm, cdm, ltp hata jahazi asilia machungu ya mgao na foleni utayapata tu!
   
 7. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Yaani waliona Mnyika akiwakilisha hoja ya kupinga POSHO, ila hawakuona hata mbunge mmoja aliyetaka kumtoa macho?

  Hii habari naona ilifaa iandikwe miezi kadhaa mwaka nyuma wakati Sheick Yahya akiwa bado hai.

  Naona sasa kunazaliwa mwingine na hatakuwa mtoto wake maana mwanae yupo Chadema.
   
 9. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Wametoana macho. Hilo ni gazeti la serikali la habarileo. Hata wakipingana hakuna tatizo ila wananchi tunataka suala la posho la litazamwe upya. Kama wana ujasiri wajitokeze kwa majina yao halisi ili 2015 tuwaengue kwenye kura za maoni kwa kuwa wameshindwa kuendana na ilani na msimamo wa Chama. Mwenyekiti na Kiongozi, Naibu, Mnadhimu na Katibu wao wapo mstari wa mbele kupinga posho kwa hiyo huo ndio msimamo wa Chama
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  Watae hao wabunge
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  wanainchi tunachotaka posho ziondolewe
   
 12. z

  zamlock JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  fufununu kuhusu habari hii wengine tumeipata toka majuzi na nimikakati ya ccm na serikali kutaka kuwachafua chadema lakini nacho jua wabunge wa chadema wanakubaliana vizur sana na wanamaelewano kwa sababu lao moja nikushika dola na ccm wasije zania huu ni muda wa kuwadanganya watu hizo zama zimeshapitwa na wakati watafute mbinu ingine lakini siyo hiyo ya uchonganishi
   
 13. A

  Abdalla Khamis Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam, kwakweli hakuna marefu yasiyo na ncha na penye haki uongo hujiengua.Methali na msemo huu umekuja baada kuuona mkanganyiko mkubwa wa kauli za CHADEMA zinazotolewa na viongozi wao Mahasimu .Kauli zinazotolewa na viongozi hao zinapelekea kuyaengua mahubiri ya uongo yanaohubiriwa na viongozi hao wadhalimu.
  Mikutano na maandamo haramu yanayoendeshwa na chama hicho chenye viongozi na wafuasi wenye tabia za kizulu za kupenda vita;imejikita katika kuhubiri mapambano dhidi ya Rushwa,ufisadi maisha magumu na hivi karibuni kuna sakata la posho za wabunge huko Dodoma.kujikanganya kwa chama hicho hasimu, kumedhihirika baada ya chama hicho kwenda tofauti na yale yanohubiriwa.
  Bila shaka sote ni mashahidi kuwa chama kimekuwa kikihubiri mapambano dhidiya rushwa na ufisadi, wakati huohuo katibu mkuu wa chama hicho,Padri Slaa akikifanyia ufisadi chama chake kwa kukishiniza kumlipa ml.7.5 huku akipinga ml.7 zinzopokelewa na wabunge akinadi kuwa huko ni kuifilisi Nchi
  .Evi jamani tuache kwanzwa suala ushabiki hapa,kupi kuifilisi Nchi kati ya kupokea ml.7.5 na ml.7? ambapo zote hizo ni fedha za wananchi wetu tunaojinadi kuwa tunawaonea huruma.Hivyobasi, hapa ndipo CHADEMA inapojikanganya katika kauli zake na hatimaye kutarajia anguko kubwa la chama hicho pale waloghiribiwa akili watakapouona unga wa Rutuba.
  Aidha mkanganyiko mwingine unajipambanua pale chama hicho kilipopanga mkakati wa kupinga posho za wabunge kikidai kuwa kupokea posho hizo ni sawa na kuwadumbukiza wananchi shimoni,huku mwenyekiti wa chama hicho,Freeman Mbowe, akiwa msitari wa mbele kusaini fomu za mahudhurio ambapo kwa pamoja hujumuishwa na kupewa posho wakati wa kusaini kama alivyo kaririwa Spika wa bunge hilo lililoingiliwa na wana muziki wanaovesika watoapo hoja.Huu ni mkanganyiko mwingine wa chama hicho ambapo viongozi wake wanajikanganya kwa yale wanayohubiri na yale wanayotenda na hii ni ishara ya kuanguka kwa chama hicho katika siku za usoni.Maana wahenga walisema kuwa"jahazi linapopoteza mwelekeo kinachofuata ni kuyumba na kuzama,ndivyo ilvyo kwa CHADEMA ya sasa.Je nyie wanamagwanda hamuoni mkanganyiko huo? unaobainisha unafiki wa viongo wenu.Kwanini mmekuwa viziwi,vipofu na mabubu kiasi hicho. Tafakarini ndugu zangu.
  Nimalizie kwa kusema kuwa "NO ONE CAN MAKE YOU BETTER WITHOUT YOUR OWN EFFORTS".
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Official response toka CDM kuhusu posho ilishatolewa mara nyingi kwanza na Mh Mbowe, katibu wa CDM bungeni (Mnyika). Na wameelza vizuri mantiki ya hoja yao pamoja na hela zitakazo okolewa na mapendekezo ya wapi ziende (i.e kuboresha mishahara ya wafanyakazi wote sio wachache).
  Pia soma budget ya kambi rasmi ya upinzani inaeleza hili la posho.

  Hii habari ya 'ndani' ya kikao cha CDM ni umbeya na fedheha kwa watanzania na ndio maana hujaandika jina la gazeti, but I can tell ni gazeti la Mt wa Lumumba. Mmefikisha hii nchi hapa kwa sababu ya umbeya na failed leadership. Badala ya kukaaa na kujadili mambo ya msingi mmeamua kuwa busy kuchunguza nini kinaongelewa kwenye vikao vya watu. Shameless bunch!
   
 15. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Cheki kwenye red! Yaani hii ndio demokrasia,na hapa naona mpango wao umefanikiwa iwapo watatu tu kati ya 40 na ushehe ndio waliopinga.Ni kweli huwezi kuanzisha wazo watu wote wakarikubali asilimia mia,lazima watokee wa kutofautiana na wewe,lakini pia lazima watokee wa wa kukurekebisha kidogo.

  Wazo lao ni zuri,na nikisoma vyombo vya habari,wanachokataa wabunge wa chadema ni kitu kidogo tu...katika malipo ya mbunge. ni km % 5 ya malipo yote.Hii haiwezi kukufanya utofautiane na wenzio,labda upo kupinga kila idea!
   
 16. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Join Date : 13th June 2011
  Posts : 12
  Thanks 0
  Thanked 0 Times in 0 Posts
  Rep Power : 0
   
 17. S

  Stany JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hayo ndo uliyotumwa na Nape/nepi? Umekosea njia.
   
 18. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hoja nyingine bana!
  sio kua umeongea uongo kwa asilimi mia ila kwa asilimia zisizopungua 90.
  uliona wapi nchi inayoendeshwa bila siasa??
  ziwe za kiimla, kidemokrasia au vyovyote ila nchi lazima iwe na siasa.
  siasa ni injini ya maendeleo ya nchi, ndizo ziznazoibua mipango, kukosoa serikali, kuikemea,
  kuishauri. siasa ndio chanzo cha sera, ndizo zinazopitisha maamuzi, na mengine mengi.
  mengi katui ya haya yakiwa yanafanyikia bungeni ambako kunawabunge ambao hua ni wanasiasa.

  Ni kweli kua wabunge hua wana maslahi yao, hyo ipo wazi.lakini pia wanajukum la kulinda maslah ya uma.
  sasa ukwa hoja yako unataka kusema kua unakubali kua hata wabvunge wasipofanya lolote kwa
  miaka yaote wanayokaa bungeni kwa maufaa ya watu wao ni sawtu??
  Serikali iliyo madarakani ifanye lolote na wabuge wanyamazietu?? hata kama halina tija kwa uma??
  hoja kaa ya zito ipo wazi hta kwa mtoto mdogo kuani ya manufaa kwa watanzania wote, unataka ipuuziwe
  kwa kua wabunge wanainterest zao??
  Suala la wabunge kupinganawao kwa wao, ni kawaida kwa sababu asicaly kila mtu anamawzo yake,
  hisia zake n.k
  sio kua wote ni waopinzania basi wote watakubaliana katika kila kitu,
  tunachaoangalia ni hoja inaukweli kiasi gani.
   
 19. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunakuwa viziwi dhidi ya upumbavu wa CCM
  Tunakuwa vipofu dhidi ya upumbavu wa CCM
  Tunakuwa mabubu dhidi ya upumbavu wa CCM

  Tutaendelea kuwa hivyo, kuanzia sisi wenyewe na vizazi vyetu mpaka ukombozi utakapofika.
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Wewe Madaya inawezekana ni NEPi na thread yako ya juzi iili backfire naona leo umejikongoja ukaja na utumbo mwingine humu. Inakuwaje unauliza swali kwa wasiohusika si uende pale ukumbi wa Bunge ukamwuulize Mbowe akufafanulie?

  Suala la posho bado halijakwisha na hakuna mbunge wa CDM aliye backdown mpaka sasa. Wewe akili yako naona inafanya kazi kwa rivasi kwa sababu sioni kujikanganya kwa CDM hapa labda wewe ndo umeamka na matongotongo machoni ukaingia bila kunawa uso humu.

  Freeman Mbowe sasa hivi saa 5:16 anaongelea suala la posho bungeni na kama uko kwenye TV msikilize acha upuuzi.
   
Loading...