CHADEMA watoana macho Bungeni

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeingia kwenye mgogoro baada ya baadhi ya wabunge kupandwa na hasira dhidi ya wenzao wanaoendesha kampeni ya kutaka posho za vikao kwa wabunge ziondolewe.Mkwaruzano huo iliibuka ndani ya kikao cha wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.Kikao hicho kiliitishwa na kambi hiyyo kwa lengo la kuweka msimamo wa kupinga posho za vikao kwa wabunge, lakini kikageuka uwanja wa vita uliozusha vurumai kubwa kiasi cha kushindwa kufikia muafaka.Baada ya kikao hicho kufunguliwa, John Mnyika (Ubungo-Chadema) aliwasilisha hoja hiyo ya kutaka wabunge wa upinzani kuweka msimamo wa pamoja wa kupinga posho hizo ili mkakati huo ulioanzia kwenye Bunge hilo la Bajeti, uweze kufanikiwa.Akifikiri ataungwa mkono, Mnyika aliwataka wabunge kuonyesha moyo huo wa kishujaa kwa kutosaini kitabu cha mahudhurio bungeni, lakini wawepo ndani ya vikao.Kauli hiyo ya Mnyika ilikuwa sawa na kumwaga petroli kwenye moto unaowaka ambapo wabunge watatu wa Chadema (majina tunayahifadhi kwa sasa) walikuja juu na kupinga vikali hoja hiyo.Upinzani huo mkali uliotolewa na wabunge hao ulidhihirisha kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyesema kuwa ingawa baadhi ya wabunge wa chama hicho wanajionyesha kimbelembele kusisitiza mpango huo, wengine wa chama hicho pia wanaumia kimoyomoyo, lakini hawasemi.Suala la kukataa posho bungeni lilianzishwa na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema) akisema zinaenda kinyume na mpango wa Taifa wa kupambana na umasikini kwa kuondoa posho zisizo na tija.Zitto akionekana kuwa na ushupavu mkubwa ilifikia mahali akaamua kutosaini mahudhurio Bungeni ili jina lake lisiorodheshwe miongoni mwa watakaolipwa licha ya Spika, Anne Makinda kutishia kuwa kitendo hicho kinaweza kumfukuzisha bungeni.Mkakati wa Mnyika ulikuwa ni wabunge wote wa upinzani kuwa na mshikamano katika hilo jambo ambalo sasa limeonekena kuwa ni nyongo kiasi cha wengine kutaka kuwararua wenzao wakisema ni msimamo usio na maana.Source: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongozaJamaa wanaweza wakaandamana fasta kupingana wao kwa wao Teh teh
Wote bado wana macho yao, wewe mwongo wa aina ya magamba
 
Tunakuwa viziwi dhidi ya upumbavu wa CCM
Tunakuwa vipofu dhidi ya upumbavu wa CCM
Tunakuwa mabubu dhidi ya upumbavu wa CCM

Tutaendelea kuwa hivyo, kuanzia sisi wenyewe na vizazi vyetu mpaka ukombozi utakapofika.

Suala la posho ni gumu kidogo mimi ningemuuliza zitto juu ya mkopo wa gari! ana Hammer ya nguvu, sasa kama ni uchungu wa nchi mbona kachukua millioni tisini tena? kwanini asizipeleke kwenye hicho kifungu? asidanganye watu bwana angisimmia woote waliopata magari mwaka jana wasichukue tena ningeelewa. hili la posho wacha tune mwisho wake. ila wasiondoe za madaktari maana tutarudi kule kule!
 
Hii habari iko kishabiki zaidi, source not disclosed.

Rating 0.4/10.

Soma gazeti la Mwananchi la leo!

search0.png

Tues 21 June 5:31PM

Home Habari Habari za Siasa Posho yawagawa wabunge Chadema, watatu wapinga






Posho yawagawa wabunge Chadema, watatu wapinga
Send to a friend

Wednesday, 06 April 2011 21:57
 
Kauli hiyo ya Mnyika ilikuwa sawa na kumwaga petroli kwenye moto unaowaka ambapo wabunge watatu wa Chadema (majina tunayahifadhi kwa sasa) walikuja juu na kupinga vikali hoja hiyo.

Umbea mtupu, kama WAmetaja majina ya ZITTO NA MNYIKA HAYO MENGINE
WAMEYAFICHA YA NINI? UPISHI HUU,

Ni hatari sana kujishughulisha na jambo usililolijua, kwa sasa tunajua
wabunge wa chadema wanapinga hii kitu mpaka apo tutakapowasikia
wanaopinga kwa midomo yao wenyewe.

na kama wapo basi joto la chama limewazidia, Chama hakitaki mambo
ya kijinga jinga, na kukosa uwajibikaji, wakishindwa

wakiache alone
 
Back
Top Bottom