CHADEMA washtukia mchezo mchafu unaofanywa na CCM!

Kosa walilofanya sekeritariati ya cdm tangia mwanzo ni kujua juu ya huu usaliti na wakachukua hatua lakini wakasahau kukiondoa chanzo kikuu. Hatuwezi kuwalaumu sana kwa maana waliamini busara ingesaidia kumaliza hili jambo na kupelekea kufanya maamuzi magumu wakiwa wamechelewa kwa kiasi fulani. Kosa kubwa zaidi litakuwa ni kurudi nyuma.

Muda wowote unaweza kuwa mwanzo, busara ilitumika ilistahili, busara imedharauliwa, chukua hatua. Uamuzi umetoka simamia twende, wabaki wenye nia, wanafiki pembeni. 'Hata uwabebe kwa turubai wanapanda na viwembe ...........'
 
Tunashukuru sana kamanda , siku ya mwisho KILA GOTI LITAPIGWA ! Tunasubiri majina yao ili WAADHIRIKE .
 
KAMA ZITO HATOFUKUZWA NITANYA MAAMUZI MAGUMU,heri awe mbunge wa mahakama kulikokuwa mbungebwa chadema
 
Hiv ww huoni haya??? chuki zako na chama tawala subiria 2015
huu ni uongo wa kitoto sana, kawadanganye watoto wenzio wa bavicha

SIRI IMEFICHUKA BAADA YA CHADEMA KUSHTUKIA MCHEZO MCHAFU UNAOENDESHWA NA CCM KWA KUWAHONGA MAKADA WA CHADEMA ILI WAJIUZURU KWA MARENGO YA KUSHINIKIZA KURUDISHWA KWA ZITTO KATIKA NYAZIFA ZAKE!!;

Barua za matamko ya waliokuwa wanachama wa chadema wanaojiuzuru zimeandikwa na mtu mmoja, katika barua hizo mambo yote yanashabihiana,

1-Wote wanapinga maamuzi ya kamati kuu ya Chadema,

2-Wote wanamzungumzia mtu mmoja Mh Zitto,

3-Wote wametumia font moja,

4-Wote wamekosea herufi za mwisho badala ya kuandika kujiuzuru wao wameandika kujiudhuru,

5-Wote baada ya kujiuzuru uongozi wamesisitiza kubaki wanachama,

je Barua hizi ni kwanini zinafanana sana??

je ziliandikwa na mtu mmoja na wao wakapewa wasome tu??

je nikwanini hawakuwahi kunun'gunika kabla au kulalamika??

Interenjensia ya Chadema ipo makini kabisa na soon wanaoratibu jambo hilo watakuwa hadharani,

WE SHALL OVERCOME.
 
msimamo wa chadema mkoa wa singida

(i)tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii)tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.

(iii)tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv)
tunampa onyo kali katibu mkuu dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga singida ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.

(v)tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa
hatuna imani na mwenyekiti wa taifa wa chama, katibu mkuu wa chama, kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.

Mwisho, kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,singida tunasema kuwa ‘’
kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi kuzuia mpasuko ndani ya chadema.’’

Kwa mawazo yangu, mmepewa hela nyingi sana inaonekana, na si uwezo wa zito tu huu kuwapa hela kuweza kumtetea hivyo. C.c.c.m inahusika sana, zito ni msaliti mno. Soon mtajulikana , wait to see, hivi zito ndiyo nani hadi iwe hivi, eti mpaka wewe unakuwa hivyo, kazi ya fedha hii.
Na kwa nini hamuondoki kwenye chama, jivue uanachama basi, mmelenga kubaki ili mlete mgogoro na ndicho mlichotumwa, watanzania wafahamu. CHADEMA WATABAKI WACHACHE MNO, MTATOKA WOTE, HAKUNA KUFUGA NYOKA NDANI
 
Inteligensia ipi? Inteligensia baada ya barua kuandikwa na wengi? Au nawe wasema kwa vile wapata kula toka kwa chama! Timiza wajibu kama kweli wewe ni intelijensia. Siasa si fani yako waache waongo waseme maana wamezoea. Huwezi kusema upo makini wakati hujui wanaojiuzulu wako wangapi? na lin?na wapi? na kwanin? maana usiaminishe watu kuwa kwasababu ya Zito ndo wanafanya hivyo?
 
Nyinyi msitishiwe nyao zitto apigwe chini tuko tayri kupita katika kipindi hichi cha majaribu kwa gharama yeyote kamati kuu tunawapongeza sana kwa maamuzi yenu
 
SIRI IMEFICHUKA BAADA YA CHADEMA KUSHTUKIA MCHEZO MCHAFU UNAOENDESHWA NA CCM KWA KUWAHONGA MAKADA WA CHADEMA ILI WAJIUZURU KWA MARENGO YA KUSHINIKIZA KURUDISHWA KWA ZITTO KATIKA NYAZIFA ZAKE!!;

Barua za matamko ya waliokuwa wanachama wa chadema wanaojiuzuru zimeandikwa na mtu mmoja, katika barua hizo mambo yote yanashabihiana,

1-Wote wanapinga maamuzi ya kamati kuu ya Chadema,

2-Wote wanamzungumzia mtu mmoja Mh Zitto,

3-Wote wametumia font moja,

4-Wote wamekosea herufi za mwisho badala ya kuandika kujiuzuru wao wameandika kujiudhuru,

5-Wote baada ya kujiuzuru uongozi wamesisitiza kubaki wanachama,

je Barua hizi ni kwanini zinafanana sana??

je ziliandikwa na mtu mmoja na wao wakapewa wasome tu??

je nikwanini hawakuwahi kunun'gunika kabla au kulalamika??

Interenjensia ya Chadema ipo makini kabisa na soon wanaoratibu jambo hilo watakuwa hadharani,

WE SHALL OVERCOME.
mmefulia hamtainuka tena kaburi ni lenu malaghai nyie
 
Kwa mawazo yangu, mmepewa hela nyingi sana inaonekana, na si uwezo wa zito tu huu kuwapa hela kuweza kumtetea hivyo. C.c.c.m inahusika sana, zito ni msaliti mno. Soon mtajulikana , wait to see, hivi zito ndiyo nani hadi iwe hivi, eti mpaka wewe unakuwa hivyo, kazi ya fedha hii.
Na kwa nini hamuondoki kwenye chama, jivue uanachama basi, mmelenga kubaki ili mlete mgogoro na ndicho mlichotumwa, watanzania wafahamu. CHADEMA WATABAKI WACHACHE MNO, MTATOKA WOTE, HAKUNA KUFUGA NYOKA NDANI
Ni sawa ila kama unauelewa kila mtu yuko huru na halazimishwi kufuata mawazo ya mtu ingalikuwa watu wote wanafuata mawazo ya watu leo hii tusingekuwa hapa. Siku zote maendeleo yanaletwa na utofauti ila si kuendeleza ujima! Inaonesha upeo wako ni mdogo na uelewa wako ni mdogo na huenda umekaririshwa tu. Soma na tafakari kisha changia kwa busara na si kutukana na kulazimisha watu waamini unayoyaamin wewe! Ingelikuwa hivyo kwa mawazo yako pasingekuwa na upinzani leo hii maana utofauti ndo ulisababisha wakataka mabadiliko! Ongeza elimu utakuwa na upeo mzuri usiishie kukaririshwa na kauli za wanasiasa maana utakuwa mtumwa milele maana watakiwa ujikomboe kifikra kwanza!
 
Hawa masalia hawana bahati hata kidogo na kama wanataka na wajiuzulu tu hatuoni tija ya kuwepo na wanafiki ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo.

Intelejensia ya CDM tunaikubali na tuko nao bega kwa bega mwanzo mwisho.

WANAFIKI HAWANA BAHATI NG'O!


Wote wanaopingana na maamuzi ya Kamati Kuu ni wasaliti nao kwa kutumia ngazi zinazolingana nafasi zao katika Chama wawajibishwe na waelezwe waondoke tu siyo lazima wawe wanachama .Huwezi kupingana na uamuzi mkubwa na muhimu wa CHAMA kama huu halafu bado ukajidai wewe ni mwanachama.
 
Kama Viongozi wa CDM Taifa wanapitapita huku JF watakuwa wameona ushauri wa baadhi yetu. Kwamba hizi vurugu zote ambazo zimeibuka baada ya ZZK,Kitula Mkumbo na Samson Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya Chama hazifanywi na Wanachama waatifu na waaminifu kwa Chama. Hawa ni mamluki tu wanaotumiwa na CCM ili kutaka kuisambaratisha CDM!

Haiwezekani mwanachama mmoja awe juu ya Chama. Na kwa hili inaonekana ni Zitto pekee ndiye amefunika wote akina MM1-3 wenzake na anayelalamikiwa na kunung'unikiwa kwamba kwanini kavuliwa nyadhifa zake zote. Hakuna hata mmoja anayehoji kuhusu UHAINI ambayo Bwana ZZK na wenzake walikuwa wakikifanyia chama!!!


Wangelikuwa ni Wanachama halisi wa CDM wenye mapenzi mema na chama wasingekimbilia kulalamika,kuandamana na hata kujiuzulu kwa kisingizio cha kuvuliwa nyadhifa kwa ZZK. Walitakiwa kuipa CC muda wakti inaendelea na hatua inayofuata katika mchakato huu. ZZK na wenzake wamepewa 14 days wajieleze kulingana na tuhuma walizopatikana nazo. Kwamba wamepewa nafasi ya kujieleze kwanini wasifukuzwe Uanachama kwa UHAINI waliokuwa wanaufanya ndani ya Chama. Kama melezo yao yatakuwa na mashiko CC inaweza kuwasamehe kwa kuwapa Onyo,Karipio kali au kuwanyang'anya nyadhifa zao moja kwa moja kwa UHAINI walioufanya!

Inashangaza kuona eti Wanachama wana andamana na wanachoma moto ofisi za Chama na kutaka kuzuia ziara za Viongozi wakuu wa Chama kwa kisingizio cha Zitto! Zitto ni nani hasa ndani ya CDM? Hivi kuna mijuha inafikiri bila ya Zitto CDM haitakuwepo?Huu ni uhuni wa watu wachache wanaotumiwa na CCM kutaka kuidhalilisha CDM. Ndiyo maana mimi bado nasisitiza CDM kuimarisha ulinzi katika Ofisi zao nchi nzima na Mikutano yao popote itakapofanyika kwa sasa.

Zitto anatakiwa ajitafakari mara mbili au zaidi na apime na kuchukua maamuzi magumu ya aidha Kukihama CDM kabisa na kuanzisha Chama chake mwenyewe au arudi hukohuko CCM kwa Mafisadi waliomtuma kuivuruga CHADEMA. Hatutaki mtu anayetaka kuwa maarufu kuliko chama na Viongozi wake. Huyo hatufai asilani.

Mwambieni mwenyekiti kutumia rasilimali za chama kuimarisha kambi yake ni unafiki mbaya sana.
 
Back
Top Bottom