Chadema wapigwa marufuku kufanya mikutano ya ndani, ila ccm ruksa popote pale

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimezuiliwa kufanya mikutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, kwenye jimbo la mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mikutano wilayani humo. [ 94 more words ]
Chadema yagonga mwamba kwa Mbowe, yapigwa marufuku
 
Magufuli anataka aombewe kwa Mungu, ili hali yeye alichopewa na Mungu anakitumia kutesa wapinzani.
Huyo Mungu angekuwa Magufuli, hata huyo Magufuli asingekuwepo leo hii.

Taifa linapojaa damu na ukandamizi hilo halitasimama! Ndio maana viongozi wenye hekima kama Mandela walianza na Maridhiano ya kitaifa, kujenga umoja wa kitaifa na kuondoa ukandamizaji na umwagaji damu.
Walijua haki ndio huinua taifa wala sio Stiglers gorge na midege mikubwakubwa.

Tutabaki tu kuomba kuombewa na kuwekewa mikono na miguu, lakini dhambi hii ya uonevu, dhuluma, ukandamizaji, uuaji hatatuacha salama!!!
 
Tabia zenu za kuombea na kushangilia nchi mabaya Leo imekuwa tamu? Wangekifuta na chama chenyewe kabisa, sioni jambo Jema kwenye chama hicho. Watuache watz tufanye maendeleo
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimezuiliwa kufanya mikutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, kwenye jimbo la mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mikutano wilayani humo. [ 94 more words ]
Chadema yagonga mwamba kwa Mbowe, yapigwa marufuku
Ili Jiwe apate usingizi kwenye kitanda kilichojaa mafaili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania tunahitaji chama kimoja kifanye kazi ili kupata maendeleo.

Hatuhitaji vyama vingi.

No need indeed!

Tuwe wakweli.

Vyama vingi ni vurugu.

Tujenge chama kimoja na taasisi imara za kiutawala.

CCM inatosha
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Back
Top Bottom