Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
Na Mwl Udadis, Tarime
Moja ya kosa kubwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanafanya na ndio inayopelekea wao kuendelea kushuka kila siku ni kudhani kuwa kupendwa na watu ni miujiza au kuna njia fulani ya mkato, ni mawazo haya yanawaaminisha kuwa ndani ya miezi 24 ijayo yatatokea maajabu fulani kisha wao watashinda Uchaguzi. Fikra hii haina tofauti na kuamini mazingaombwe.
Badala ya kufanya kazi hivi sasa Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wanagombana kwa madai kuwa Mbowe amechukizwa kitendo cha kundi la Dkt. Slaa na Wakili Mwabukusi kukusanya fedha kwaajili ya kuendesha mikutano bila kumshirikisha yeye na kisha kutaka kuwashirikisha Chadema katika hatua za mwisho. Msingi wa madai ya kundi la Mbowe yamejengwa katika tamaa ya fedha na ni uthibitisho wa namna baadhi ya viongozi wa Chadema wanavyotumia siasa kujinufaisha badala ya kujenga chama chao.
Wakati huo huo Ndugu Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama yeye bado yuko Ubeligiji akidai anajipumzisha kidogo baada ya kufanya mikutano katika Mikoa Mitatu. Japo habari za chinichini zinadai yuko katika matibabu kutokana na kuzorota kwa Afya ya akili bado wataalam wa siasa na mikakati wataungana na mimi kuwa Chadema imelala na inakisindikiza Chama cha Mapinduzi katika ushindi wa zaidi ya Asilimia 90.
Ni ukweli usiopingika kuwa ulozi au "Abracadabra" kwenye siasa haipo, hivyo Chadema inapaswa kufanya kazi kama CCM wanavyofanya yaani kufanya ziara, kutatua matatizo au kutoa njia mbadala, kusikiliza watu wanasema nini badala ya kujikusanya katika "WhatsApp group" na kutoka na maazimio ya kihuni ambayo wachangiaji wanayatoa wakiwa bar ya triple seven Mikocheni.