Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Pasco!
Ndugu yangu kwenye hii dunia kama hutatumia ubongo wako vizuri utakumbana na watu ambao kupandikiza chuki ,kupindisha ukweli,kuugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli,kupandikiza fitina kwa gharama ya maisha ya wengine,hivi mpaka leo hujajiuliza kuna tuhuma nyingi ambazo chadema wamesema wanaushahidi wa kutosha lkn hakuna hata moja ambayo wameshaifikisha sehemu husika ili sheria ichukue mkondo wake.Mchungaji Mtikila kuna sehemu anapotoka na kuna sehemu amekuwa na ushahidi na tumeona mara zote pale anapokuwa na ushahidi amekuwa akiibuka kidedea.Wacha tuwaruhusu watu wachache wajenge fitina ndani ya hii nchi bila ya kujiandaa kuongoza nchi kwa usalama tutafikia mahala tutaona majuto ni mjukuu.Angalia Tunisia waliona Rais ndiyo tatizo na ukweli inawezekana ndiyo huo lkn njia zilizotumika kumuondoa na kuondoka kuaicha nchi ilivyo hivi sasa kweli zimewasaidia nini watunisia waliowengi.Hivi huyu ambaye wote walikuwa wanamuona adui ameathirika vipi na matukio yanayoendelea hivi sasa Nchini Tunisia.
Ushahidi upi zaidi ya huu?
1. Tunadaiwa zaidi ya bil. 700 na wakandarasi, tumelipa? Kwa nini tunadaiwa?
2. Tunadaiwa na dowans, kisa uzembe!!
3. Deni la taifa ni mara mbili, kisa?
4. Wanafunzi wanakosa mikopo, kisa?
5. Huduma za afya?
6. Elimu?
Nachoka kukutajia ushahidi. Angalia maisha ya watu wanaokuzunguka then endelea kutafuta ushahidi.
Pasco anachotakiwa kuelewa ni kwamba sababu za uchaguzi wa arusha kuahirishwa mpaka January ni kutokana na MkuRugenzi pamoja CCM kupinga uhalali wa wabunge wa viti maalum wa CDM wakati Chitanda akiruhusiwa Arusha. Kisichoeleweka ni nini hapo?