This is democracy at work. N matumaini yangu uongozi wa Chadema utapokea maneno hayo badala ya kutaka kuunda tume na kuyafanyia kazi. Miye nasubiri kuona wanachama wa CCM watakapoandamana kutaka uongozi wa chama chao kuwajibika kutokana na mlolongo wa kashfa za:
IPTL
Richmond
EPA
Ndege
Ripoti ya CAG
Wizi wa Benki Kuu
Buhemba
Matumizi ya nguvu Tarime
n.k
Maana wale wachache waliopiga kelele Tanga walikemewa vikali. Je CCM au kuna mwana CCM mwenye uwezo wa kufanya kile walichofanya Chadema Dar? Miye nawapo big ups hawa jamaa na Mtanzania yeyote yule ambaye haoni aibu kutaka mtu awajibike kwa sababu ya kuogopa chama, sura, jina, cheo, au hadhi ya mtu huyo. Je wana CCM wako tayari kuitisha mafisadi na viongozi wanaotuhumiwa kashfa wajiuzulu? Halafu Makambe ndiye aende kupokea maandamano hayo?
Hapa Chadema wanawafundisha CCM kuwa hakuna kuogopwa mtu, kupendelewa au kuonewa haya. Ila viongozi hawa wakitokea wanachama wengine wa Dar wakitaka wajiuzulu wasing'ake maana kuwajibika ni kuwajibishana.
Ungekuwa na uwezo wa kutofautisha Chama cha Siasa, Serikali, na Chama tawala ungekuwa na msaada mkubwa sana katika kupambana na matatizo yaliyopo. Au kwa kuwa unajua watu wanaosoma mawazo yako wanaamini chochote unachooandika? Labda tu nikuulize ni kwa nini EPA hukuiingiza kwanye wezi wa BOT au ulitaka kuongeza idadi ya kashfa? Please eti nk.
Let say viongozi wa CCM ameitikia wito wako wa kujiuzuru ni vipi itatatua matatizo yaliopo? Tutakuwa tuna recycle watu tu hakuna chochote kitachotokea. Nitakupa orodha ya viongozi wa CCM hapo chini.
Na kivipi CHADEMA wanawafundisha CCM na siyo TLP au NCCR?
Ukiingalia kwa undani utagundua wana-CHADEMA wameandamana kwa sababu wameona kuwa hayo mambo yanadhoofisha chama chao. Labda tu nikuulize ni kivipi EPA imeathiri CCM isipate kura ya 80% kwenye uchaguzi wa 2005?
Mwanakijiji, hizo kashfa ulizozitaja kama tukiendelea kuzitafutia ufumbuzi kwa njia tunayotumia sasa kuatakuwa hakuna ufumbuzi wowote. Ngoja nikupe mfano labda utanielewa, kwa mfano umeacha $100 mezani na mtu pekee unayeishi naye ni mke wako, uliporudi ukakuta imepotea hapo moja kwa moja utakayemhisi ni mke wako na hapo kuna kesi ya kujibu. Ila kama ulimpa hiyo hela wakati unaondoka na kumuambia akakununulie pipi na baadaye unaporudi anakupa pipi yako na receipt inayoonyesha kuwa amenunua pipi kwa $100 na ulipoenda dukani wakakudhibitishia kuwa wamemuzia pipi $100. Huu mfano una cover kashfa tatu IPTL, Richmond, EPA, Ndege. As a nation, this is the challenge we are facing, kama tukijaribu kufanya hizi ni political agenda au personal attach, we are not going anywhere in anytime soon.
Viongozi wa CCM wanaotakiwa kujiuzuru na Mwanakijiji.
Mwenyekiti wa CCM
Ndugu Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Yussuf R. Makamba
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Ndugu Jaka Mwambi
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa
Ndugu Amos Gabriel Makala
Katibu wa Organaizesheni wa CCM Taifa
Ndugu Kidawa Hamid
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
Ndugu John Zefania Chiligati
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM Taifa
Ndugu Bernard Kamilius Membe