CHADEMA wanapoandamana Kumtaka Mbowe atoe Maelezo Kuhusuiana na Kifo Cha Wangwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wanapoandamana Kumtaka Mbowe atoe Maelezo Kuhusuiana na Kifo Cha Wangwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kevo, Oct 11, 2008.

 1. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Gazeti la Uhuru Limeripoti kwamba CHADEMA wameandamana ili kumtaka Mwenyekiti wao atoe maelezo ya kutosha kuhusiana na tuhuma zinazomkabili kwamba alihusika na kifi cha Chacha Wangwe.
  Vilevile wamemtaka Mwenyekiti wao ajielezee kuhusiana na ufisadi unaomkabili kuhusiana na fedha za ruzuku vilevile kuhusiana na UKabila ikiwa ni sababu ya yeye kuwateua wabunge zaidi ya watano wa viti maalumu kutoka kwenye Mkoa wake wa KIlimanjaro ambao ni Wachagga.

  MY TAKE

  Sasa ikiwa vyama vya siasa ambavyo ni upinzani ambavyo tunavipigia debe vichukue madaraka kutoka kwa CCM haviwajibiki vyema nadani ya vyama je wakipewa nchi watafanya vyema?Maana this is just party wise wameshindwa wataweza kitaifa?
  DR Slaa Mwenyewe wamemtuhumu kulinda ufisadi ndani ya chama chake ilihali huku nje ndio mpiga ufisadi.
  JE TUTAFIKA?
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapendwa mtanisamehe nimeiona hii mahala nimeona ni shee nanyi kidogo sija edit kitu....

  CHADEMA Dar waandamana, wataka Mbowe ajiuzulu


  Na Gladness Mboma

  WANACHAMA wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam wamemtaka Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, ajiuzulu ili kukinusuru chama vinginevyo watafanya maandamano mengine makubwa.

  Mwito huo ulitolewa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya CHADEMA, Bw. Bakari Shingo, kwa niaba ya wanachama, wapenzi na wapenda demokrasia ndani ya chama hicho, mara baada ya kuandamana hadi makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

  Maandamano hayo ambayo yalikuwa na lengo la kushinikiza kuitishwa kwa Baraza Kuu ili kuzungumzia migogoro ya chama hicho na mambo mengine, yalipambwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumshutumu Bw. Mbowe na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Wilbroad Slaa.

  Bw. Shingo alimtaka Bw. Mbowe kufuata nyayo za aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, ambaye alijiuzulu urais hivi karibuni.

  Alisema sababu nyingine za kumtaka Bw. Mbowe ajiuzulu ni kutokana na mambo mbalimbali zikiwemo tuhuma za kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe.

  "Sababu nyingine za kumtaka Bw. Mbowe ajiuzulu, ni juu ya uhalali wa viti vitano vya ubunge kati ya sita kuchukuliwa na watu kutoka mkoa wa mmoja wengi wakiwa ni kabila moja la Wachaga," ilisema risala.

  Ilidai kuwa Bw. Mbowe anatuhumiwa kwa mambo mengi kikiwamo kifo cha Bw. Wangwe na kwamba tuhuma hizo ni nzito kwa kiongozi mkuu wa chama, hivuo haziwezi kuachwa zipite bila kujadiliwa na vikao vya chama.


  Bw. Shingo alitaka Baraza Kuu likutane na kuziangalia kwa undani tuhuma zinazomkabili kwa maslahi ya chama ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi kuhusu mgogoro wa wanachama wa mkoa wa Dar es Salaam, badala ya taarifa zinazoandaliwa na Katibu Mkuu na Sekretarieti ya Makao Makuu na kupeleka taarifa ya kupotosha ukweli kwa Kamati Kuu.

  Alisema ili kumuenzi marehemu Wangwe, ni lazima viongozi wahakikishe kwamba jimbo la Tarime linarudi mikononi mwa CHADEMA.

  "Tunatambua wazi kufanya maandamano haya ya amani ambayo ni haki yetu ya msingi na ya kikatiba, viongozi wakuu wa chama kama ilivyo kawaida yao, wataona ni uasi na uchochezi.

  "Lakini lengo kuu ni kuwaonesha dira na maono viongozi wote wa vyama vya kisiasa ili wakubali kukosolewa na wakubaliane na njia yoyote ambayo wanachama kwa nia njema wataona ni sahihi katika kuwakilisha maoni na mawazo yao," alisema.

  Alisema miaka ya hivi karibuni viongozi hao wa CHADEMA wamekuwa wakijizolea sifa ya kuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali na kuibua mambo mazito mazito likiwamo la ufisadi na wananchi waliwaunga mkono kwa kuwapongeza.

  "Lakini cha ajabu ninyi viongozi wakuu wa CHADEMA na makao makuu kwa ujumla, mmekuwa wagumu wa kukosolewa, kamwe hampendi kukosolewa kabisa, mwanachama au kiongozi yeyote akiwakosoa, mnamchukia na kumwona kama msaliti na mchochezi," alisema.

  Bw. Shingo alimtaka Bw. Mbowe kusafisha kwanza ufisadi ndani ya chama chake ndipo asafishe kwa wenzake, na alimshtumu Bw. Slaa kulinda ufisadi ndani ya chama hicho.

  Alisema wamekuwa na utaratibu wa kiungwana wa kukosoa kwa njia ya maandishi, kutuma nyaraka mbalimbali kwa Katibu Mkuu Slaa, lakini zingine amekuwa hazijibu.

  Bw. Shingo alisema cha ajabu badala ya kuwaita wakakaa na kujadili kama wana CHADEMA, yeye amekuwa akitumia sekretarieti ya makao makuu na kupeleka ajenda Kamati Kuu kwamba wao ni waasi na wakorofi wachokozi.

  Alisema wanatambua fika kupigania haki ya kidemokrasia ya kweli, kunaweza kuwagharimu maisha yao, hivyo wanayaweka rehani, lakini lengo kuu ni kuwa na demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya siasa.

  Bw. Shingo aliitaka pia Kamati ya Bob Makani isiendeshe mahojiano kama mahakama ambayo imepewa maelekezo na sekretarieti, kutafuta wahalifu ndani ya chama, bali ifanye mazungumzo ya kina na wahusika kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa hali inayokikabili chama na wanaokosoa wana hoja gani ya msingi.

  Alisema wangependa tume iwe huru, kwa maana hiyo Bw. Tundu Lisu na Mbunge wa viti Maalumu, Bibi Halima Mdee waondolewe kwenye Tume kwa kuwa wao ni sehemu ya tatizo na ni wajumbe wa sekretarieti, ambayo mara kwa mara wamekuwa wakitumiwa kwa mambo mbalimbali.

  Naye, Bw. Victor Kimesera aliwapongeza wanachama hao kwa kufanya maandamano ya amani, lakini aliwaeleza kwamba hayuko hapo kwa ajili ya kumjibia Bw. Slaa, bali risala yao ataiwasilisha katika ngazi ya utekelezaji.

  Alisema risala wataiangalia kama itakuwa ni ya msingi wataitisha Baraza Kuu, kama si ya msingi watahitaji wapelekewe mambo mengine ya msingi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya maandamano hayo, Bw. Kimesera alisema ana imani maandamano hayo yana 'mkono wa mtu', kwa sababu yamekuja ghafla mno.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tunatumia mifano ya Mbeki hata mahali pasipostahili. Uchaguziwa CHADEMA si ni mwaka huu? Kwanini wasisubiri kama wana watu wa kutosha kumng'oa kwenye uchaguzi?
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbeki kuiuzulu amegeuzwa na exemplary ya kila top political leader kujiuzulu anapokabiliwa na shutuma nzito ili kupisha upelelezi wa ziada.
  I think CHADEMA inamtegemea Mbowe sana no wonder he runs it like a personal business together na akina mzee Mtei na mzee wa Keys Hotel!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama huyu Mbowe na Slaa wanawaletea longlongo kwenye Chadema si mkajiunge CUF, TLP au CCM?
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mpitanjia wewe jipitie na nazo hilo hawalikubali kamwe!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ok, huu unaweza kuwa ushauri mbovu, basi waanzishe chama chao na wawaache Slaa na Mbowe na chadema yao ya kifisadi
   
 8. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  You nailed it right Mpita njia.
  Inaelekea na wao wameshapatiwe vijisenti wapige kelele ambazo hazina kichwa wala miguu. Kama Kimesera alivyosema ni lazima kuna mkono wa mtu.
  Hizi njaa zitatumaliza jamani!!
   
 9. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Poverty may be the mother of crime,corruption,irresponsibility and poor governance but lack of good sense is the father.
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hii mpita njia duu

  Mkuu tunachopigana ni kutokomeza ufisadi ktk ardhi yetu.Hivyo kuwaacha Mifisadi na chama chao bao wanaibia wananchi kodi zao maana wanapata posho.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  taratibu Mkuu tutaelewana tu kwa sababu nimeshaona kuwa tupo pamoja. hata mimi sipendi mafisadi waendelee kulelewa. Kama hawa wanaolalamika ndani ya Chadema wakiondoka, Mbowe na Slaa watakuwa dhaifu kwa sababu watakuwa wamep[ungukiwa na nguvu kwa kiasi kikubwa (hasa ukizingatia kuwa they will be leaving on a good course). Huo ndio mwanzo wa anguko la mafisadi ndani ya Chadema kwa sababu chama chao kitakufa kwa udhaifu.
  Hii inaweza kufanyika popote pale, mimi naamini kuwa if yo cant beat them, leave them
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Mkuu
  Unajua hiyo taktiki ya kuhama watu wameitumia sana kuihama ccm wakidhani kitazoofika lakini imeshindikana.
  Siri ya kumimaliza mifisadi ni kujiunga nao mpigane nao humo humo.Chama chenye mapesa kama ccm eti kujiengua hakutasaidia chochote hivyo hivyo kwa mafisadi wa chadema wana ukwasi tayari wa posho hizo.

  Siri ya aliye juu mfuate huko huko juu,ukimsubiri chini utasubiri weeeee mpaka mwisho wa dunia.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Hivi inaingia akilini kweli kwa mtu kama Dr.Slaa ambae ni mwiba wa ufisadi akumbatie ufisadi?


  Mkamap na Mastu,jaribuni kufikiria mbele kidogo. Sasa mbona hata siku moja hamjawahui kuwahamasisha wenzenu waihame CCM iliyozingirwa na ufisadi toka juu hadi Chini?
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini kinachonitia mashaka ni kuwa hizi mbinu zao za mapambano, hazionekana kama zina uthabiti fulani. labda ni wakati sasa kwa wapinga ufisadi wa kweli wakajiunga pamoja na kutengeneza chama ambacho kitapamba na mafisadi wote kokote kule waliko
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  mkuu
  ukianzisha chama bado mafisadi wataingia ktk chama hicho nacho kupoteza mwelekeo.
  Dawa hapa ni sisi wote kuwapeleka puta mafisadi wote bila kujali wanatoka wapi na chama gani.
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Ungekua na nia ya dhati,ungeshaanza kwenya chama chako ambako ndiyo mzizi wa ufisadi.Acha unafiki mkuu
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  ?????????????????? wenzangu CCM?
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Pole bro,and i'm so sorry.I didnt mean it!
   
 19. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wanachama hawa hawajui hata priotize? Poor we
   
 20. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  baada ya kikwete na kundi lake kushindwa kuwaletea maenedeleo watanzania... Na kuona uchaguzi unakaribia...na hawana cha kuwaambia watanzania... Wameamua kumwaga fedha ili wananchi wapoteze imani na chadema... Lol... Chadema inatisha.....
   
Loading...