CHADEMA; wanajf na mh. Zitto tetesi na utabiri mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA; wanajf na mh. Zitto tetesi na utabiri mpaka lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MsandoAlberto, Mar 29, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha tetesi. Zitto! Chadema!

  Sasa imekuwa upuuzi. Hakuna ushahidi wa lolote. Kila siku 'kuna taarifa'.

  Nguvu inayotumika kuchangia au kujibu tetesi ingetumika kuweka mipango ya ukombozi tusingesubiri miaka 50 kuendelea.

  Yanayozungumziwa hapa ni majungu, fitna na umbea kuhusu Zitto, Chadema nk.

  Kama Zitto amesaliti chama mbona hajafukuzwa uanachama? Kama mtu anaweza kuwa msaliti akachaguliwa kuwa Naibu wa Kiongozi wa Upinzani, akaendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mbunge kwa tiketi ya chadema basi usaliti una maana tofauti. Wanaojiita wanachadema na kumshambulia Zitto huku uongozi hauchukui hatua ni wanafiki.

  Lazima tujifunze kufuata utaratibu tuliojiwekea. Kama kuna ushahidi wa Zitto kusaliti utolewe kwenye vikao husika na Zitto ataadhibiwa bila kuona haya.

  Kusema Zitto amesaliti au hafai halafu hakuna anachofanywa haina tofauti na Mwinyi na Vuai wanvyoachwa baada ya mauaji ya raia kwa risasi na mabomu.

  Upuuzi huo hauwezi kulelewa Chadema. Hakuna mtu ambaye ni zaidi ya chama. Hilo liko wazi na litasimamiwa siku zote. Chuki, fitna, porojo, wivu havina nafasi. Msaliti akithibitika anaondoka. Wameondoka wengi na hatujutii
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani bora wewe umesema, inachosha kila siku kusikia Zitto Zitto,
  let the man do his work
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  God Bless cdm and Dr Slaa
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunachotaka nyekundu ibaki kuwa nyekundu na kijani ibaki kuwa kijani na sio redblue colour! Hicho tu mkuu.Zitto tunampenda na tutamkosoa panapostahili
   
 5. k

  kikule Senior Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji tetesi ambazo ni more than 80% true lakn sio umbeya
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Penye utata umbeya haukosekani mkuu! Tatizo ni kiza na mfumo mpya wa kisiasa wa Zitto.bado tunamhitaji mwenzetu.
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  tatizo ukiwa kijani, njano, nyekundu au blue huwezi kujificha, sasa wewe unadai tusubiri mpaka chadema ndiyo watuambie kuwa rangi hii ni kijani ndiyo na sisi tukubari. Hii ni forum wewe huwezi pata humu dicipline ya aina yoyote. cha muhimu wewe vyonza vitu vya maana na achana na mengine, kuna nondo za maana nyingi humu na upuuzi wa khali ya juu sana pia.

  Zitto atavuna tu anachopanda kama mchicha basi atavuna mchicha na kama ni bange.............................
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ama ni chadema au ccm wanaoleta hizo "taarifa" au ''tetesi'' kama ulivyoziita. Cha msingi ni kuwapuuza. Ila tukumbuke ukiwa maarufu hautakosa maadui wengi. Chadema,Mbowe,Slaa,Zitto & Co. wanapitia kipindi cha kulipa gharama za umaarufu wao. Ama watasalimika au watajiangamiza kutokana na busara ya jinsi watakavyo-handle hii hali.
   
 9. G

  Gurti JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alberto wewe mwenyewe unaweza ukawa tatizo kama hoja zako zimekaa hivyo. Kinachopaswa si kuzuia watu kuleta tetesi au mashaka juu ya Zitto WALA kuwa na cheo ndani chama si kigezo cha kutosemwa.
  Mosi, kinachotakiwa ni zitto kujibu kila hoja moja baada ya nyingine. Inadaiwa kuwa zitto aliwasiliana au anawasiliana na usalama wa taifa, ajibu yeye alizungumza nao nini? Kumbuka hawezi kubisha kuwa hakuzungumza nao kwani ushahidi uliwekwa wazi.
  Zitto kuwa anataka kuingia kwa mikakati michafu kwenye uenyekiti limesemwa sana jf na magazetini. Yeye aseme kuwa anagombea au hagombei au hajaamua. Tatizo liko wapi?
  Lakini ulivyo mtetea inaonekana wewe utakuwa wale wanaoamini kuwa zitto anaweza kuwa mkiti wa chadema taifa. AU wewe kama kiongozi wa chadema una maoni gani kuhusu zitto?
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tunajua wewe ndo weboraye same ID UMEGONGA MWAMBA
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Zitto msaliti, Huo siyo umbea its true100% wabunge wote cdm wanajua yuko njian kwenda NCCR. Zitto go zitto go kichefuche..! Unataka ushahidi upi? UTAMTAMBUAJE? Tazama MATENDO
  1. Kwa nini hakutoka nje bugeni?
  2. Usaliti majibo ya chadema kgoma na kafulila wake.
  3. Kupigiwa kura bagamoyo na wabunge wa cdm.
  4. Kupuuza maandamano ya kanda ya ziwa( eti mama anaumwa) we nes or dr? Go go...
  5. Mawasiliano na idara ya usalama TISS (Wachakachuaji wa matokeo). For what?
  6. Mawasiliano na Rostam fisadi. For what?
  7. Kumuomba JK amsaidie uwenyekiti kamati ya bunge mashirika ya umma. For what?
  8. Mawasiliano ful time na lipumba, mbatia na kafulila kuliko hata viongoz wa cdm.
  9. Kutoshiriki maandamano ya Arusha?
  10....
  11....
  12...

  TAZAMA MATENDO
  eti anajifanya bize na uwenyekiti kuliko isue za cdm Go go go
   
 12. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Silazimiki kuwa naive namna hiyo! Ni wazi Zitto wa leo si yule tuliyemzoea,tuliyem-admire, tuliyeweka matumaini yetu kwake tukiamini wakati wa vijana si ndio huu sasa. Zitto amegeuka, hilo kila mmoja analiona,isipokuwa ameamua kufumba macho yake tu asione. If ther's any reason I do care about him now, is that slim hope that ,whatever happened to him just caught him off-guard and there is always room for repentence. Na si vinginevyo. Kuendelea kwake na nafasi zake za uongozi CDM kamwe haiwezi kuwa sababu ya mie kuamini kuwa yu safi na hajatokewa na lolote chafu. CDM ni chama cha watu makini,si kama CCM ya makamba. Wanaona mbali.Wanapima pros na cons za action yeyote watakayochukua dhidi yake,given the delicate nature of the situation this time around. They might have forgiven him (If he apologized....and we do not necessarily know); They might have put him under probation; they might have given him over to the fate of time; and many other things....Politics,politics...sometimes is like an iceberg, you only see the tip and you can't know the size of it beneath. Just allow me to see beyond the surface!
  Namna pekee kwa Zitto kurejesha imani ya wengi walioacha kumwamini,ni vitendo tu kwa sasa. Atende vyema tu,kila jambo litasahaulika,na heshima yake itathibitika. Ni kiongozi mahiri and everybody knows that! Ada ya mja kunena na Muungwana ni Kitendo!

  Ntaipenda CHADEMA na ntaaamini tu kuwa kwa sasa ndicho chama pekee ninachoweza kukipokea,mpaka pale kitakapobadilika na kuwa vinginevyo.
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu diwani Msando umenena, inabidid tuangalie mbinu za namna ya kusonga mbele badala ya kulaumiana kila siku
   
 14. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Upotofu wa kisiasa ni pale watu wanapotaka SIASA iwatenganishe watu na WATU wao!
  na mwisho wa siku HAWATATAKA wanasiasa wao WAKIFANYE KILE KINACHOTAKIWA KUFANYWA ILA KILE WANACHOTAKA WAO KUFANYIWA!!

  Sidhani wala sitarajii kwa haya malumbano yasio na HAJA wala HOJA kama kuna yatakapotupeleka!

  WENGI WATAKUWA KAMA KASUKU ANAPOSEMA "KARIBU" WAKATI HAWEZI KUFUNGUA MLANGO!
  .....Watanzania na mayowe yasio na tija....
  .....Watanzania na siasa za mapokeo zisizokuwa na mafanikio....
  .....Watanzania na ushabiki wa vyama watu....
  .....Watanzania na TETESI, zisizokuwa na MIGUU wala VICHWA.....
  .....Watanzania na Alinacha za Punda wa Dobi....
  .....Watanzania na Ahadi hewa, na Kutumai yasiokuwepo.....
  .....Watanzania na KUTAKA watendewe, BILA WAO KUONESHA UTENDAJI WAO!
   
 15. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  This is too harsh..
  Nafikiri Zitto kama mwanadamu anapitia matatizo yote yakiwamo ugonjwa, misiba n.k
  Pia kama raia anayo haki kimsingi kuwasiliana na yeyote kwa lolote ili mradi tu havunji sheria na taratibu za nchi.

  Pia kama mwanadamu anaweza kukosea, yes, anakosea. Cha muhimu ni kusonga mbele na kuacha kumkatisha tamaa. Sidhani kama alizaliwa anajua siasa. Wote hujifunza.
  Mie binafsi naona mchango wake unahitajika katika chama... ikumbukwe kwa namna moja ama nyingine ametumika kuwavuta vijana wengi kuziona siasa katika jicho la tofauti.
  Tumpe likizo
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ni kweli watu wanamuandama sana huyu jamaa lakini huwezi kuzuia watu kwa namna hiyo.
  Inabidi madai mengine yenye utata zaidi ajitokeze kuyajibu..
  Ni jambo baya kama watu wanapoteza imani na kiongozi wao na kiongozi hafanyi juhudi yoyote ya kuwarudisha.
  Suala la kwanini chadema hawamfukuzi hilo ni suala jingine na nafikiri lina utaratibu wake. Hiyo isikupe uhakika wa moja kwa moja kwamba yupo sawa. Inawezekana yupo/hayupo.
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwanamageuko,

  Naweza kusema kwamba hii ya kwako ni post ya mwezi uliopita.

  Kasuku kusema Karibu wakati hawezi kufungua mlango.........

  Katika hili umenena vizuri.

  Nashukuru sana.
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurti,

  Si lengo langu kuzuia tetesi wala mashaka juu ya Zitto. Ninachokisema ni kwamba kuwe na hatua baada ya tetesi na mashaka. Hatuwezi kuendelea kuishi kwa tetesi na mashaka. Mpaka leo hii wizi wa mamilioni ya EPA ni tetesi au mashaka? Dowans ni tetesi au mashaka?

  Haya ninayosema si tetesi wala mashaka:

  Zitto ni Naibu Katibu Mkuu CDM

  Zitto ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni

  Zitto ni Mbunge wa Kigoma n.k

  Sasa kwa nini abaki katika nafasi hizo huku tetesi na mashaka juu yake vinaendelea? Aidha sii kweli au CDM haina ubavu wa kumchukulia hatua. Au ni suala la muda bado anachunguzwa? Siamini katika la kwanza na la mwisho. CDM ina uwezo thabiti wakufanya maamuzii magumu hata kama muhusika atakuwa ni Zitto. Ukimya wa CDM unamaanisha kitu kimoja tu, Zitto bado si tatizo la kuhitaji maamuzi magumu. Kama CDM inaamini na inauthibitisho zitto ni msaliti asingeachwa kwani kwa kufanya hivyo CDM itaendelea kuhujumiwa. Zitto kwa nafasi yake atakuwa anapata taarifa nyingi muhimu za CDM sasa iweje aachwe aendee kuzipata kama ni msaliti?

  Kuhusu Zitto kuwa mwenyekiti wa Taifa anaweza. Yeye ni mwanachama wa CHADEMA na mwanachama yeyote anaweza kuwa kiongozi wa chama endapo tu atachaguliwa na wanachama. Suala kama Zitto anaweza kuchaguliwa na wanachama ni suala tofauti kabisa. Hilo siwezi kulijibu kwani kuna mambo mengi yanayotakiwa kutokea ili mtu achaguliwe. Kwa mfano, lazima nafasi iwe wazi. Pili lazima jina lipitishwe, tatu lazima kura zipigwe na ashinde. Sasa mimi nitawezaje kutabiri hayo? Sasa hivi tunaye Mwenyekiti ambaye anaendelea na nafasi yake, hakuna uchaguzi uliotangazwa nk. Kwa hiyo kuwa na subira, tusianze kujadili 'tetesi' 'mashaka' Zitto kuwa mwenyekiti CDM au Zitto kugombea nk. Tusubiri.
   
Loading...