Chuki ya Yericko Nyerere dhidi ya Zitto Kabwe ni chuki yake binafsi na sio ya CHADEMA

Abdul Nondo

Abdul Nondo

Verified Member
Joined
Oct 28, 2016
Messages
269
Points
1,000
Abdul Nondo

Abdul Nondo

Verified Member
Joined Oct 28, 2016
269 1,000
Nimekuwa nikifuatilia maandiko ya Yericko Nyerere tangu 2013 dhidi ya Zitto Kabwe hadi leo.Nina diriki kusema kwamba Yericko Nyerere amehifadhi chuki binafsi nzito dhidi ya Zitto Kabwe hadi sasa .Chuki hizo husababishwa na mgogoro wa kinafsi (personal conflict) ndani ya Yericko kuona Zitto Kabwe aliyekuwa akimtusi na kumshambulia tangu zamani akiendelea kuwa mwanasiasa imara na wakuaminiwa na wana demokrasia,vijana , watanzania na vyama vingine vya upinzani .

Jambo hilo limekuwa likimfanya Yericko kuendeleza mapambano yake binafsi, kwa kuhusisha taasisi ya Chadema , wanachama dhidi ya Zitto Kabwe na ACT wazalendo.

Bahati mbaya sana,chuki zake binafsi amezihusisha na Chadema na wanachama wake baadhi wanaomuamini sio wanaomjua ,wanaomjua wanampuuza kila siku ila wasiomjua wanamuamini.Mimi nataka umjue Yericko Nyerere leo kuwa chuki zake dhidi ya Zitto Kabwe ni chuki binafsi na za muda mrefu .Sema haamini kuwa Zitto Kabwe hakuanguka alipitarajia Zitto aanguke.

Labda anajiaribu leo kwa kupata endorsement kutoka kwa wafitinishaji wengine kupitia yeye ,kujiaribu kama atamuangusha.

*2013* hadi leo Yericko Nyerere amekuwa na chuki binafsi dhidi ya Zitto Kabwe.Na amekuwa akimshambulia Zitto mitandaoni na Jamii Forum waziwazi kwa muda mrefu sana.

Tarehe 5/Januari/2014 katika blog ya Yericko Nyerere mwenyewe aliandika andiko shambulizi dhidi ya Zitto

Kichwa cha habari.
" *Uongozi wa Siasa Tanzania umekosa maadili ya uongozi wa Taifa kuzaa akina Zitto* " . Akimshambulia Zitto ,ila Zitto alimpuuza.

Tarehe 15 ,Novemba 2015 , Yericko Nyerere aliandika Jamii Forum kuwa tar 13/11/2013 saa tano usiku ,alipigiwa simu namba +4915739568962 ,kuwa akitishiwa .akaenda polisi kufungua RB 9833/2013 .Anadai polisi walivyomuliza ahisi aliyemtishia ,yeye akataja Zitto Kabwe.

Ila baadaye kwa taarifa iligundulika kuwa ni Yericko Nyerere mwenyewe alitengeneza mtu ili kutishiwa kwa kupigiwa simu kwa code ya ujerumani mtandao wa E-plus ,ili aseme ni Zitto Kabwe .Sababu eti siku kadhaa Zitto alikuwa ujerumani .Ila Zitto alimpuuza Yericko Nyerere.

Yericko huyu huyu ,alitamani Zitto asahaulike kabisa ,asitajwe asiandikwi popote kwa chuki zake binafsi.Tarehe 18,Januari 2014 Yericko Nyerere huyu huyu aliandika mitandaoni akishambulia magazeti ambayo yaliandika juu ya Zitto kabwe kulazwa Nigeria ,Yericko akaja akaandika kuwa habari hizo ni za uongo zimepikwa na Zitto mwenyewe aache kurubuni watanzania kupitia vyombo vya habari. Aliandika kana kwamba yeye ni mlinzi au PS wa Zitto Kabwe .

Unaweza kuona namna ambavyo ,Yericko Nyerere alibeba chuki dhidi ya Zitto kabwe.Ila Zitto Kabwe aliendelea kimpuuza Kijana.

2013 ,Yericko huyu huyu alianza kampeni kusema ACT ni tawi la CCM ,Juzi tuu hapa katika kundi moja la whaatsp kataja kuwa CUF sio chama pinzani tena ni Tawi la CCM ,bali wapinzani ni CHADEMA ,ACT ,NCCR na vingine isipokuwa CUF.


Yericko Nyerere,huyu huyu tarehe 15/Machi/2019 .Alianza kampeni yake rasmi kumshambulia Maalim Seif kuhamia ACT , akamshambulia Zitto Kabwe na akakishambulia chama kuwa ni chama kidogo ,hakina madhara kwa CCM na kinatumika kuua CHADEMA.

Nilimjibu Yericko Nyerere kuwa kama ACT inatumika kuuwa CHADEMA ,aje atuambie ni namna gani CUF ilitumika kuuwa NCCR , atuambie namna CHADEMA ilitumika kuwa CUF ,ndio aje atuambie namna ACT wazalendo inavyotumika kuuwa CHADEMA .

Una muita Zitto Kabwe msaliti anatumika ,umemuita hivyo muda mrefu sana Lowassa uliyekuwa una mpinga kaja CHADEMA,kaondoka CHADEMA kurudi CCM na akakuachia kesi mahakamani (kesi ya Amani bila haki) ila Zitto Kabwe bado yupo upinzani ,Dr.Slaa ulikuwa una muita mpinzani yupo CCM Zitto bado yupo upinzani,Mwita ,Shonza,Kafulila,Katambi ,Mtatiro na wengine wapo CCM leo Zitto bado yupo upinzani alafu una muita Zitto msaliti kwa chuki zako

Juzi huyu Yericko Nyerere ameibuka tena kwa kumshambulia Zitto Kabwe kuhusu mahusiano yake na Tundu Lisu,eti Zitto alimtusi Tundu Lissu ,Zitto aliwatusi CHADEMA.Mbona husemi kuwa ni Tundu Lissu ndiye aliyesoma press ya kumvua uongozi Zitto na baadaye kusema Zitto ni Mbunge wa Mahakama?

Yote haya hayana nafasi tena kwa sasa ,sababu viongozi hawa wajuu wameona hakuna haja ya kuwa na uwadui ambao hauna faida ikiwa adui wao wote anajulikana wazi kwa sasa .

Hivyo wameamua kwa pamoja kusahau yaliyopita na kuganga yajayo(Forward Ever Backward never).Na uzuri wote Mh.Tundu na Mh.Zitto wamehojiwa DW jana ,wameweka sawa juu ya mahusiano yao ya ukaribu.

Wafitinishaji wanakutumia kufitinisha umoja wa vyama vya upinzani na wamepata hiyo fursa kukutumia wewe sababu ya chuki zako binafsi dhidi ya Zitto Kabwe.

Uzuri ni kwamba Yericko hutaweza ,Sababu kila mtu anajua kuwa wewe ni kibaraka na unatumika kwa chuki zako kukwamisha umoja imara wa upinzani nchini .Kila mtu anajua kuwa wewe ni mtu wa kuzusha na muongo ,jambo zuri zaidi ni kuwa viongozi wakubwa wa CHADEMA wanakupuuza na hata wanachama pia wanakupuuza sababu wanakujua ,wasio kujua ndio wataamini hekaya zako za Abuniwasi.

Mbali na fitna zako na chuki dhidi ya Zitto Kabwe,umekuwa ukijisahau na kujikuta ukimsifu Zitto Kabwe kuwa ni kiongozi imara.Umemsifu tarehe 8 octoba 2017 kuhusu *ubatili juu ya uteuzi wa katibu wa Bunge* ,umemsifu tarehe 11/Februari / 2018 kuhusu *mabadiliko ya Sheria ya TISS na namna TISS* inavyopaswa kufanya kazi.Ukasau kuwa "Y can not be Y and be Y at the same time" Y ni Y tuu ,lazima ujue kuwa "Zitto ni Zitto tuu siku zote" .

Sijawahi muona Mh.Mbowe akimsema vibaya Mh.Zitto wala Mh.Zitto akimsema vibaya Mh.Mbowe.

Sijawahi kuona viongozi wajuu wa CHADEMA au NCCR wakimsema au kumshambulia Zitto Kabwe tangu alipo hamia ACT wazalendo .Wewe Yericko ni nani ndani ya uongozi wa CHADEMA hadi ujipe cheo cha kuisemea CHADEMA na kuaminisha umma fitna na chuki zako,kwani viongozi hawapo?

Ni kwasababu wanajua uimara na mshikamano wa vyama pinzani.

Nikuache na Maneno haya:

Kiongozi mkongwe wa chama pinzani nchini New Zealand Hon.Donald Thomas Brash (Don Brash) aliwahi sema hivi.

"Opposition parties don’t have the same resources as the Government and the Executive, so we have to work twice as hard to get the same results"

Kuwa upinzani hauna rasilimali kama ambavyo Serikali au chama kilicho madarakani wanalivyo ,hivyo upinzani una paswa kufanya kazi mara mbili yake au hata zaidi ili kufikia malengo na matokeo. Don Brash alilisitiza sana juu ya umoja,upendo na mshikamano wa upinzani na sio migogoro miongoni mwa wapinzani.


Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com
0659366125

Nyegezi-Mwanza.
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
35,862
Points
2,000
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
35,862 2,000
Tofauti za wapinzani ni advantage kwa CCM hivyo mwanasiasa yoyote makini wa upinzani hawezi kuziendekeza.

Wenzetu wanafanya maigizo ya kusameana,sisi tuko busy kuhujumiana!!
 
Hijja Madava

Hijja Madava

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2014
Messages
2,971
Points
2,000
Hijja Madava

Hijja Madava

JF-Expert Member
Joined May 14, 2014
2,971 2,000
uzi mrefuuu wote huu wanini ABDULI mdogo wangu siasa za namna hii haziko kwenye wakati huu
Abduli tunaijua mipango yako yote ww na Zitto
tunaelewa kwanini Zitto huenda Belgium kila uchao
Yeriko si wa CHADEMA na CHADEMA si ya Yeriko
mawazo yenu ya kukifanya ACT kuwa chama kikuu cha upinzani
haitofanikiwa kwa kipindi hiki cha chaguzi za karatasi dhidi ya mtutu
 
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Messages
5,553
Points
2,000
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2012
5,553 2,000
Dogo tuliza munkari,
Utapoteza sana. Ni afadhali kutafuta upatanishi kuliko kumwaga uharo humu.
Mtafute Jericho ni kijana mwenzio mkae mzungumze, hatimaye mtakubaliana kutokukubaliana. Lakini mtaheshimiana tu.
 
nipekidogo

nipekidogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2019
Messages
494
Points
980
nipekidogo

nipekidogo

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2019
494 980
Huyo Yeriko Nyerere ndio nani na anajihusisha na nini? Kwasababu mtu ukifanya utafiti kati ZZK na huyo unaemuita Yeriko Nyerere kila katika watu 30 utapata watu 2 ndio wanaomfahamu waliombaki watakwambia wanafahamu ZZK, huyo Yeriko Nyerere anafahamika hapa hapa jf! Hiyo sidhani km majungu yake na chuki zake vina impact yyt kwa siasa za ZZK.

Kama ZZK hakupotea wkt akipingwa na kutangazwa vibaya na chadema kama kama chama itakuwa huyo asiyejulikana? Ninatamani ifikie point chadema waachane na siasa za kudeal na mtu mmoja mmoja bali ziwe zile siasa za chama kwa chama, Sera kwa Sera km ilivyokuwa miaka ya 2000 mpk 2005 hapo tutakuwa na chadema bora kabisa.
 
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Messages
5,553
Points
2,000
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2012
5,553 2,000
Dogo kuwin mind za watu kwenye akili inahitaji umakini mkubwa, tulia soma game vizuri, majority ya members wa jf ni watu kwenye upeo mkubwa wa kuchambua mambo, hatupelekeshwi na hisia,
Nakuonya Mara ya mwisho kuwa makini au utapoteza
 
mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Messages
2,139
Points
2,000
mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2010
2,139 2,000
Akili ndogo ndo huwa zinasengenya watu, ukishajua watu wana personal issues kama wee ni akili kubwa you don't take your time discussing them, because it won't help you.

Tunahitaji watu wanaokuja na mada ngumu tumekwama wapi kama Taifa, na tufanye nn tuweze kuingia uchumi wa kati. Conflict zao binafsi zinatusaidia nn kama Taifa?
 
Mzizi wa Mbuyu

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
6,160
Points
2,000
Mzizi wa Mbuyu

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
6,160 2,000
Jingine wewe kama Nondo Abdul "aliejiteka" kwa umri wako na ili uje kuwa mtu wa maana baadae achana na kuabudu watu! Abudu falsafa na ukweli.

Epuka kutajataja majina ya watu kwa kuyaabudu.

Hao watu unao waabudu bado wanaishi, wanapitia mengi pengine kupita yako! Watakapo kengeuka utaweka wapi sura yako ilhali uliwaabudu!?
 
Tajiri mpole

Tajiri mpole

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2018
Messages
1,210
Points
2,000
Tajiri mpole

Tajiri mpole

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2018
1,210 2,000
Dogo umeongea Pumba sana,na umejikanyaga kanyaga sana kwenye andiko lako.MARA USEME TANGU 2013 MZEE WA MBUTU alikuwa na chuki binafsi na Zitto,lakini hapo hapo unasema mwaka 2017/2018 huyohuyo Yeriko alimsifu Zitto..
Kaachini jifunze kutunga uongo.Hivi umemaliza masomo kwanza dogo?
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
21,695
Points
2,000
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
21,695 2,000
Tofauti za wapinzani ni advantage kwa CCM hivyo mwanasiasa yoyote makini wa upinzani hawezi kuziendekeza.

Wenzetu wanafanya maigizo ya kusameana,sisi tuko busy kuhujumiana!!
Kwani Nondo ni mpinzani tangu lini?
 
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
12,790
Points
2,000
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
12,790 2,000
Nondo kama ulikuwa hujui Yeriko ni "litmus" paper ya Chadema.Anatumwa kufanya,kusema na kutukana watu.Hata yeye ajui alitendalo,adui mkubwa wa Zitto na ACT yake ni Chadema
 
mbikagani

mbikagani

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Messages
2,852
Points
2,000
mbikagani

mbikagani

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2014
2,852 2,000
Watu wote mliokuwa mnamshambulia Zitto Kabwe na kumuita mnafiki, mkibadirika na kuwa kama Abdul Nondo, ccm itakuwa na wakati mgumu sana.

Tubadirike, yule mkuu wa wilaya ya dodoma aliwai sema Zitto ni kibaraka, leo hii yeye sijui tumuite nani.

Zitto ni kiongozi wa mfano sana.
 
Mgirik

Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Messages
11,868
Points
2,000
Mgirik

Mgirik

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2013
11,868 2,000
Ilikufaa Sana ungejikita kwenye taaluma yako uliyosomea, ungejitahidi kubobea na ungekuwa assert.
Lakn umeamua kuingia kwenye maisha ya pata potea maisha ya ili uishi vzr lazma uwe mnafiki, maisha ya kuishi kwa kutafuta huruma kwa walala hoi!
 

Forum statistics

Threads 1,336,689
Members 512,697
Posts 32,547,763
Top