VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.
Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.
Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki