'CHADEMA wanahusika'

'CHADEMA wanahusika'

Mkuu, nimevutika na uchambuzi wako.
Kwa hiyo marehemu Mwangosi (mwandishi wa habari) ni chama kwa maana ya CDM?
Na alizungukwa na kupigwa hadi kuuawa na polisi wapatao wanane akiwa katika kazi za chama-CDM?
Hakika kazi bado mbichi.
Mkuu kwani yule masikini mwandishi aliitwa pale na polisi?
Hebu chambua hilo!
 
Unaona Mkuu Mzee Tupatupa,
Haya ndio mawazo ya washauri wengi ndani ya CCM: kusema uongo kweupe bila hata aibu wala kupepesa macho!

Mkuu mimi si mshauri wala mjumbe wa NEC wala halmashauri ya CCM
Ni mwanachama tu wa CCM na kama ningekuwa na ushauri wa kutoa katika CCM ningesema JK amang'oe mafisadi waote ndani ya chama.
Lakini hili la kupimana nguvu na Mwema, CDM lina watouch!
 
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku. Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki
Twiga wa katar,pembe za ndovu chadema hao
 
Kila tukio lina specific circumstances zinazozunguka matukio hayo.

Lile la Mwangosi imebainika CHADEMA walitaka kupimana ubavu na polisi, yaliyotokea yametokea.
Mmmeambiwa kila kona kuwa at least wangetumia busara(wote CHADEMA na Polisi) kifo kile kisingetokea.
Kwa hiyo lawama zimeenda 50% polisi, na 50% CHADEMA/M4C.

Huwezi jivua lawama kama malaika, ukubali kukosolewa kama mnavyo wakosoa wengine.

ndiyo mkuu ndiyo maana hata mahakamani amepelekwa polisi 1 kwa kosa la mauaji na chadema kapelekwa 1.kwa hiyo ngoma droo.
 
ndiyo mkuu ndiyo maana hata mahakamani amepelekwa polisi 1 kwa kosa la mauaji na chadema kapelekwa 1.kwa hiyo ngoma droo.
Hayo ndiyo mawazo yaliyokaa kichadema-chadema, kupambana na polisi badala ya sera za kuwatumikia watanzania.
 
Hivi kwenye zile ahadi za mgombea wa CCM mwaka ule, CHADEMA ilikuwa ni ahadi namba ngapi? Je, wananchi wanaridhishwa na utekelezaji wa hii ahadi CHADEMA?

CCM hata kuwashangaa pekee inashangaza!
 
Nyie acheni hizo bana!
Hamjui hata mapigano ya Kongo chadema wanahusika?
Ndo maana serikali ya ccm imepeleka jeshi kupmbana na waasi we element za kichadema chadema
 
Mkuu na wewe nisaidie swali hili.
Tunaposema EL, RA na Chenge na wengine walipelekwa mahakama ipi.
Lakini ukweli unsbaki pale pale kuwa ni mafisadi.

Na nyie kubalini kukosolewa au kujikosoa.

Al lahaulaa! Haha huu mpango wa kuchanganya mbovu na mbichi tena!
 
Chaguzi za CCM kugubikwa na rushwa chafu Chadema wanahusika.
 
CCM hawana jipya,wao wamegeuza CHADEMA ndio kituo chao cha polisi,maovu wanatenda wao wanakimbilia kuisakama chadema.
CHADEMA haipo kiivyo,CHadema for tanzanians relief

Heeeeeeeh, wajameni, hii ni serias au
 
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.

Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.

Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki

Kuna uwezekano mkubwa CHADEMA inahusika na huu uzi kupitia kwa Mzee Tupatupa
 
Hata suala la Rais J.K kuhudhuria msiba wa Kanumba na kuhojiwa na vyombo vya habari huku kukiwa hakuna taarifa za Rais kuhudhuria na kutoa rambirambi " msiba " wa Daudi Balali,CHADEMA walihusika 100%
 
Hata rais kikwete na waziri Pinda kutokujua kwanini wananci ni maskinini CHADEMA inahusika.Hata kwapo kwa nyoka wenye ndimi mbili ndani ya CCM ni CHADEMA inahusika.Hata rushwa kwenye chaguzi zao za ndani, CHADEMA inahusika.Hata rais kuwataka CCM wasitegemee polisi kuwatetea dhidi ya hoja za CHADEMA, ni CHADEMA inahusika.

Nadhani sasa wamwambiea mwibaji wao kapteni Komba ashirikiane na afande Katembo na Kurutra Mapunda watunge wimbo ambao kibwagizo ni CHADEMA INAHUSIKA.Wamwombe Bi Kidude awaimbie wimbo huo labda utaaminika na sio kuwatumia ze OK kwani raia wataona ni kichekesho tu.
 
Back
Top Bottom