'CHADEMA wanahusika'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,039
2,000
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.

Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.

Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,101
2,000
Tupatupa

Ukiona hivyo ujuwe Chadema sio chama cha msimu tena.

Ukiona hivyo ujuwe chadema wanatishia uhai wa ccm

Ukiona hivyo ujuwe Chadema imekomaa na sasa ni tishio lililokamilifu kwa CCM

Ukiona hivyo ujuwe mafisadi hasa watawala ndani ya ccm matumbo yanawauma maana siku za vilio na kusaga meno zinakaribia

Ukiona hivyo Jitu pekee linaloitisha ccm na udhaifu wake ni CHADEMA

Ukiona hivyo ............watanzania wanabadilika kwa kasi na muda simrefu nchi nzima tutaamka kuidai haki yetu haki ya

- Kupata elimu bora

-Haki ya kupata afya bora

-Haki ya kugawana raslimali za taifa kwa usawa sio mafisadi wachache

-Haki ya kuishi pamoja kwa amani na umoja kama watanzania na kuutupilia mbali upuuzi wa kugawanywana na ccm kwa dini zetu ili wadumu kututawala.........

nidhambi mbaya sana kuchomekea migogoro ya kidini kwa ulafi tu ubakie madarakani kama chama tawala lakini sisi akina yahe tuuwane kwanini?
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,711
2,000
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.

Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.

Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki
Kila tukio lina specific circumstances zinazozunguka matukio hayo.

Lile la Mwangosi imebainika CHADEMA walitaka kupimana ubavu na polisi, yaliyotokea yametokea.
Mmmeambiwa kila kona kuwa at least wangetumia busara(wote CHADEMA na Polisi) kifo kile kisingetokea.
Kwa hiyo lawama zimeenda 50% polisi, na 50% CHADEMA/M4C.

Huwezi jivua lawama kama malaika, ukubali kukosolewa kama mnavyo wakosoa wengine.
 
true

JF-Expert Member
Nov 26, 2011
506
225
Pinda kulia bungeni kwa ajili ya kuuwawa kwa albino? CHADEMA WANAHUSIKA!
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha ccm na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,chadema wanahusika;wakizomewa mawaziri na viongozi wa ccm,chadema wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,chadema wanahusika;wakiandamana waislam,chadema wanahusika(?).kila baya chadema.

Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo chadema inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,chadema huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.

Kama ni kweli chadema inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki

vema sana tupa tupa

ila we tambua tuh ya kwamba siku zote mfa maji haachi kutapa tapa
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,101
2,000
Kila tukio lina specific circumstances zinazozunguka matukio hayo.

Lile la Mwangosi imebainika CHADEMA walitaka kupimana ubavu na polisi, yaliyotokea yametokea.
Mmmeambiwa kila kona kuwa at least wangetumia busara(wote CHADEMA na Polisi) kifo kile kisingetokea.
Kwa hiyo lawama zimeenda 50% polisi, na 50% CHADEMA/M4C.

Huwezi jivua lawama kama malaika, ukubali kukosolewa kama mnavyo wakosoa wengine.

Mkuu

Teyari mahakama imetoa hukumu ya kifo cha mwangosi na adhabu ilikuwaje baada ya hukum hiyo kama ilitolewa?

Nimeuliza hivi ilikuthibitisha hizo lawama kwa 50% chadema na 50% polisi kuwa zinaukweli na ni halali!
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,711
2,000
Mkuu

Teyari mahakama imetoa hukumu ya kifo cha mwangosi na adhabu ilikuwaje baada ya hukum hiyo kama ilitolewa?

Nimeuliza hivi ilikuthibitisha hizo lawama kwa 50% chadema na 50% polisi kuwa zinaukweli na ni halali!
Hizi LAWAMA ZINA UKWELI KABISA!
Hilo limethibitishwa na kada wa CDM aliyejiuzulu Nd Nyimbo.

Yeye alisema alikwisha lifungua tawi la Nyololo, Iringa na hakuhusishwa katika "! Uzinduzi" wa kisanii uliofanyika wakati wa kifo cha Mwangosi.

Lengo la uzinduzi wa kisanii lilikuwa kupimana ubavu na polisi Iringa.

Kwa hiyo wote, Polisi na CHADEMA walihusika na kifo cha mwandishi wa habari huyu.

CHADEMA iwe na utamaduni wa kukubali kukosolewa na kujisahihisha amasivyo kitakuwa chama cha kidikteta, na upotevu wa maisha ya watu wasio na hatia utaendelea kwa ukaidi huu.
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
1,225
Ni kauli ya kuudhi na kukata tamaa. Hutamkwa sana na viongozi-tena wa juu wa chama changu cha CCM na 'washirika' wake pale linapotokea tukio lolote,hasa lisilovutia. Wakiuawa watu na polisi,CHADEMA wanahusika;wakizomewa Mawaziri na viongozi wa CCM,CHADEMA wanahusika;wakigoma wanafunzi wa vyuo vikuu,CHADEMA wanahusika;wakiandamana waislam,CHADEMA wanahusika(?).Kila baya CHADEMA.

Hizi ni siasa za kipuuzi. Hazitachelewa kuchosha. Sasa,kwahiyo CHADEMA inakubalika kuliko wengine hadi kukubaliwa mipango yao nchi nzima? Eti,CHADEMA huwanywesha watu viroba ili wazomee?! Hakuna cha viroba,magunia wala pakacha....watanzania wanabadilika. Hawasomeshwi vya kutosha shuleni lakini maisha ni shule kuu zaidi. Wanahitimu kila siku.

Kama ni kweli CHADEMA inakishinda chama changu kiushawishi mashuleni,vyuoni,vijijini,masokoni,mijini na kwingineko,mbona uchaguzini hakitangazwi mshindi mara kwa mara? Kinana na wengine,kuanzia leo hatutaki kusikia kauli hii.Ikome na mpambane tumwone mshindi wa haki
CCM hawana jipya,wao wamegeuza CHADEMA ndio kituo chao cha polisi,maovu wanatenda wao wanakimbilia kuisakama chadema.
CHADEMA haipo kiivyo,CHadema for tanzanians relief
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,101
2,000
Hizi LAWAMA ZINA UKWELI KABISA!
Hilo limethibitishwa na kada wa CDM aliyejiuzulu Nd Nyimbo.

Yeye alisema alikwisha lifungua tawi la Nyololo, Iringa na hakuhusishwa katika "! Uzinduzi" wa kisanii uliofanyika wakati wa kifo cha Mwangosi.

Lengo la uzinduzi wa kisanii lilikuwa kupimana ubavu na polisi Iringa.

Kwa hiyo wote, Polisi na CHADEMA walihusika na kifo cha mwandishi wa habari huyu.

CHADEMA iwe na utamaduni wa kukubali kukosolewa na kujisahihisha amasivyo kitakuwa chama cha kidikteta, na upotevu wa maisha ya watu wasio na hatia utaendelea kwa ukaidi huu.

Mkuu swali langu umelielewa? naomba unieleweshe kulingana na swali lilivyo.

Top Bottom