Ninaomba niseme kitu hapa
Mtumishi wa serikali hulipwa posho kazini na ni haki yake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.
Posho hulipwa pale ambapo mtumishi amefanya kazi nje ya masaa ya kazi na au nje ya kituo cha kazi.
Mtoa mada umesema vizuri kwamba watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa DSM wameenda Dodoma kikazi. Kwa hiyo walicholipwa ni haki yao kulingana na hadhi zao.
Je, laki 2.5 ni halali kwao?
Niwakumbushe: mwaka huu wakati Rais anahutubia Mei Mosi aliahidi kupandisha posho (Per diem) kutoka laki na 20 kwa siku na kuwa laki 2.5 kwa siku. Na hili limeanza kutekelezwa bajeti ya 2022/2023 iliyoanza July 2022.
Kwa hiyo, hizo posho ndugu zangu ni halali kabisa. Hakuna siasa hapo. Hapo ndipo hela inafanya kazi. Na ni kawaida. Hakuna jipya!