Katika hali ya upepo ya kisiasa, Chadema wamekuwa wakihaha kila kukicha pindi Nape anapokuwa anatoa sera za kisiasa juu ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania bara (CHADEMA) kwa nukuu mbali mbali; Mfano: Nape hivi karibuni amesema Dr. Slaa ni mwanachama wa CCM, na yeye bila hiyana akajitokeza na kukiri kuwa ni kweli kwa kumiliki kadi ya CCM. Na nyingine nyingi hadi viongozi wa Chadema wakatishia kwenda Mahakamani kitendo ambacho sasa, kesho na keshokutwa hakitawezekana ama kwa uoga au kukosa wataalamu wa kisheria.
Wakimkimbilia Tundu Lissu Jimboni kwake pamemshinda hadi hivi karibuni alikiri kuwa CCM wamemshinda hivyo hawawezi tena, hii ilitokea pale alipo itisha Mkutano na Wananchi wa Jimbo lake bila Maandamano tarehe 08/12/2012 kijijini Mang'onyi. Si hayo tu alikiri mambo mengi na mengine alionekana anawadanganya wananchi na kufikia hali wa kuanza kumuaibisha pale aliposema CCM wameanzisha mradi wa kilimo na umwagiriaji na alishangaa kusikia CCM wanasema wamelima mashamba hekta 20 wakati yeye anajua shamba lililolimwa ni hekta moja mwananchi mmoja akanyosha mkono na kumtuliza kwa kumwambia Mheshimiwa tunaomba ulekebishe kauli yako kwani kwahili unasema uongo, eneo lililo limwa hadi sasa tunapo ongea ni zaidi ya hekta 21 na kudhibitishia hivi nami ni mmoja wapo wa wanakikundi hivyo Mheshimwa tunakukalibisha ujionee ili unapopanga sera zako zinyooke.
Mbali zaidi ni pale Nape alipotangaza kuwa sasa CCM wanawavua Magamba wanachama wao, Chadema wakadakia kwa kusema VUA GAMBA VAA GWANDA. Kwa hali hii inaonyesha wazi Chadema wanaishi kwa mgongo wa CCM hivyo wanatakiwa kujipanga zaidi.
Ukweli unagharimu lakini ili ufanikiwe lazima uufanyie kazi. Kwa asiyeamini awasiliane na wahusika wampe ukweli ulivyo.
Nawasilisha