CHADEMA Wamkubali Nape kwa maneno yake

CHADEMA Wamkubali Nape kwa maneno yake

Katika hali ya upepo ya kisiasa, Chadema wamekuwa wakihaha kila kukicha pindi Nape anapokuwa anatoa sera za kisiasa juu ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania bara (CHADEMA) kwa nukuu mbali mbali; Mfano: Nape hivi karibuni amesema Dr. Slaa ni mwanachama wa CCM, na yeye bila hiyana akajitokeza na kukiri kuwa ni kweli kwa kumiliki kadi ya CCM. Na nyingine nyingi hadi viongozi wa Chadema wakatishia kwenda Mahakamani kitendo ambacho sasa, kesho na keshokutwa hakitawezekana ama kwa uoga au kukosa wataalamu wa kisheria.

Wakimkimbilia Tundu Lissu Jimboni kwake pamemshinda hadi hivi karibuni alikiri kuwa CCM wamemshinda hivyo hawawezi tena, hii ilitokea pale alipo itisha Mkutano na Wananchi wa Jimbo lake bila Maandamano tarehe 08/12/2012 kijijini Mang'onyi. Si hayo tu alikiri mambo mengi na mengine alionekana anawadanganya wananchi na kufikia hali wa kuanza kumuaibisha pale aliposema CCM wameanzisha mradi wa kilimo na umwagiriaji na alishangaa kusikia CCM wanasema wamelima mashamba hekta 20 wakati yeye anajua shamba lililolimwa ni hekta moja mwananchi mmoja akanyosha mkono na kumtuliza kwa kumwambia Mheshimiwa tunaomba ulekebishe kauli yako kwani kwahili unasema uongo, eneo lililo limwa hadi sasa tunapo ongea ni zaidi ya hekta 21 na kudhibitishia hivi nami ni mmoja wapo wa wanakikundi hivyo Mheshimwa tunakukalibisha ujionee ili unapopanga sera zako zinyooke.

Mbali zaidi ni pale Nape alipotangaza kuwa sasa CCM wanawavua Magamba wanachama wao, Chadema wakadakia kwa kusema VUA GAMBA VAA GWANDA. Kwa hali hii inaonyesha wazi Chadema wanaishi kwa mgongo wa CCM hivyo wanatakiwa kujipanga zaidi.

Ukweli unagharimu lakini ili ufanikiwe lazima uufanyie kazi. Kwa asiyeamini awasiliane na wahusika wampe ukweli ulivyo.

Nawasilisha
Mkuu vipi mbona unabwabwaja hata unaloongea halieleweki, hujalipwa posho nini, au umeambiwa na Nape usipopost lolote kwenye forum hupewi kitu leo????

Ni kweli lakini tambua kuwa hata leo hii CCM wakiitisha mkutano wananchi watakuja wengi kuliko unavyofikiri wewe mmoja au hujalijua hilo. Uchukiavyo wewe si kama nichukiavyo mimi na yule. Slaa kwenye uchaguzi uliopita alisema hamtambui Kikwete kwa sababu ameibiwa kura, lakini hadi sasa amekuwa kimya na wakati wakiri wa Serikali alisema wazi mahakamani kwenye kesi ya Lema kuwa anayetakiwa kufungua mashitaka juu ya uonewaji wa uchaguzi ni mhusika mwenyewe au Slaa si muhusika mwenyewe anasubiri wananchi tuandamane kwa shinikizo lake?
Mbona unajadili vitu vya kipumbavu! kwani watu kwenda kwenye mkutano ni kutatua matatizo ya msingi? watu wakienda kwenye mikutano ya ccm ufisadi wa viongozi wa ccm utaisha? umaskini utaisha? huduma za afya zitaimarika? shule za kata zitaboreka? mfumko wa bei utashuka? Tafadhari usitupotezee muda wetu na propaganda za kipumbavu! mwambie Nape na wapumbavu wenzako hatuna muda wa kuchezea!
 
Mkuu vipi mbona unabwabwaja hata unaloongea halieleweki, hujalipwa posho nini, au umeambiwa na Nape usipopost lolote kwenye forum hupewi kitu leo????

Unataka kuelewa ama kutukana. Kuna jipya ambalo hujalisikia? hata kama uko kijijini wantolakano umejuliswa. Kama hujui na hutaki kujua kweli hutajua. Ndo maana wakasema usimwamushe aliyelala! Mimi nakuamsha najua sitalala ni lipi ambo hujalijua liweke hadharani ni kjuze
 
Hivi kwa nini kila bomu analotoa nape linawafanya cdm wachanganyikiwe kwa nini hamko stable kama wenzenu ccm

bom lipi la Nape jr ? Au nitaarab anaimbia watu wana M4C ? Maswali ya humu ndani ameshindwa kujibu amekimbia! Labda kama amekutuma msaidie kuyajibu na sio uanze kutoa point za kimipasho!
Yaani hilo daftari la wapiga kura wakiliupdate +2015
sisiem chali!
Na propaganda zenu mlizotumia kudhoofisha NCCR na CUF this time around hamtemi!
 
We tata mura ni mzigo kama mizigo mingine tu ya magamba (CCM). Mnatoka na thread za kipuuzi/kijinga mkiamini wa tz wote ni wadanganyika. Wewe na Nape waathirika wa uchakachuaji wa elimu ambayo inatakiwa imuongoze binadam aongee nini, aseme mbele ya watu. Hoja ya kijinga ya umilikaji wa kadi inaonyesha jinsi msivyotambua mipaka ya umilikaji wa kadi za chama cha siasa. Kama alivyofafanua wakili Kimong'oro kadi ya chaam ni mali ya mwanachama hivyo pindi akiacha ana halali ya kuitunza au kuitupa au kuchoma moto. Kinachowanyanyua watu na akili zao kuingia barabarani na hoja yenye ***** inashangaza sana. Waambieni watz mna mpango wa kuwafanyia nini kuondoa umaskini baada ya kusota miaka 51 ya uhuru si vinginevyo. Tambueni kuwa watu sasa wameerevuka na kujua haki zao.
Bado mkuu wanazahama la Mabilion waliyoficha nje ya nchii huku Watanzania wakiachwa utupu wanakula mlo mmoja kwa siku wao wanatamba na vijisenti vya waheshimiwa!!!Mabilion ya Uswiss Mkuu wanatakiwa wayarudishe waache kutuyumbisha na story mara hoo kadi za CCM , mara hoo Nape, mara hoo nini tena, kama hawaturudishii fedha zetu tutajipanga kuandamana hapo watajua CDM ni nani katika siasa za nchi hii????

Kichwa cha Habari angeandika Chadema wamkubali Nape kwa Uzushi wake na Uongo, huyu mwana CCJ huwa alali bila kutaja uongo wowote juu ya CDM , Juzi kaipa CDM R.I.P wakati wao ndio hoi , mpaka imefikia kukomba mawaziri wote na kuwaangaisha huku na kule , wengi wanaishia kuzomewa, wengine waongo kama muhongo aliyetubambika umeme wa siku kumi heti ngao umeisha.
 
we boya kama unandoa nae sasa nadhani imeimarika

Busara na Hekima huendana na ukweli, kwani wewe Ndoa yako na CCM umeivunja lini? au hujui umeolewa na CCM? Siku zote aliyeolewa matatizo yake hupenda kumjulisha mumewe kama ufanyavyo wewe. Unaongozwa wewe na Viongozi wako na CCM au na hili hulijui?
 
Kwa nini kila wakati ni mambo ya kinapenpe. Nape ni nani, huyu mtu kaishiwa busara kabisa mdomo wake unanuka matusi tu hata sijui kwa nini unamsifia. Labda na wewe ni mmoja wa aina ya kina Nape. Watanzania tuna matatizo lukuki yaliyosababishwa na viongozi wenye hulka za Kinape, kwa nini tusitumie muda wetu kujadili jinsi ya kupata ufumbuzi? Kwa nini tunakwepa kuongea juu ya ufisadi, kuibwa kwa ndovu, kuficha hela nje ya nchi, kutorosha wanyama wetu, mikataba inayowafaidisha viongozi dhaifu, mauaji ya wananchi wasio na hatia nk. ambavyo ni mali ya watanzania wote, kuliko kujadili upuuzi huu. Unanikera kweli, be mature mentally.
Mkuu tusisahau RICHMOND, DOWANS, BUZWAGI KAHAMA GOLD MINE, NYAMONGO GOLD MINE MUSOMA yako mengi yaliyolididimiza taifa la Tanzania, bado tunatakiwa kulipa DOWANS sijui nani hasi Lowasa ua Rostamu??? Halafu huyu jamaa anakuja na Manepi ili kutupoteza bado tunahitaji kujibiwa na fedha zetu zirudi!!!!

[/COLOR]Ni ukweli usiopingika watu wameelimika na wanautambuzi wa uhakika kwa kujua uongo na ukweli. Jaribu kufuatiria na ya Tundu Lissu kama na yeye anasingiziwa. Sema mtu akiwaamsha ili uendelee kuleta upinzani nchini kwa ujuha wenu munaona kuwa yu mjinga.

SUN OF A BEACH at work!!!
 
Bado mkuu wanazahama la Mabilion waliyoficha nje ya nchii huku Watanzania wakiachwa utupu wanakula mlo mmoja kwa siku wao wanatamba na vijisenti vya waheshimiwa!!!Mabilion ya Uswiss Mkuu wanatakiwa wayarudishe waache kutuyumbisha na story mara hoo kadi za CCM , mara hoo Nape, mara hoo nini tena, kama hawaturudishii fedha zetu tutajipanga kuandamana hapo watajua CDM ni nani katika siasa za nchi hii????

Pole sana kwa uelewa mbovu, maandamano unafikiri nitija au mahamasisho ya umwagaji damu kama mganga wenu alivyo aambia, Mkiona nchi imetulia kwa maendeleo mnafikilia maandamano ni kwa nini msitumie mikutano kuelimisha wananchi ili waelewe kwanza pindi wanapoandamana hata mtu akiumia anajua ameumia kwa jambo la kutoka moyoni mwake?. Tofauti na ilivyo sasa Maandamano yanakuwepo kwa sababu ya watu wachache kutafuta sifa. Kaa chini fikilia je ni kweli maandamano yanatatua matatizo yetu?. Zitto alisema anawataja watu walioficha pesa USWISS lakini hadi leo kimya. Mimi nafikiri kazi si kuwataja tu bali hata kuwashitaki pia, au yeye si mtanzania? Hatuwezi kuumia kwa maneno tunatakiwa tutende sasa.
 
Kumbe unarusha madongo kwenye chaka, uone kutatoka nini??? Basi umekwama mura hupati kitu kwa njia hiyo, mwambie Nape kuwa amenoa!!!!
Unasema tu, ni wangapi wamekuja kwenu wakapewa vyeo wengine vya juu kabisa?
 
bom lipi la Nape jr ? Au nitaarab anaimbia watu wana M4C ? Maswali ya humu ndani ameshindwa kujibu amekimbia! Labda kama amekutuma msaidie kuyajibu na sio uanze kutoa point za kimipasho!
Yaani hilo daftari la wapiga kura wakiliupdate +2015
sisiem chali!
Na propaganda zenu mlizotumia kudhoofisha NCCR na CUF this time around hamtemi!

Daftari la wapiga kura lipo ila wafuasi waliowengi wa Chadema ni wa maandamano labda na kujiandikisha maandamano yaitishwe. Ili kukusanya wapigadebe, wavuta bangi na wengineo wengi na wala si hivyo tu, Hata siku ya kupiga kura maandamano yaitiswe pia. Dawa kuelimisha wananchi kwa ruzuku inayotolewa kwanza na kama mnasema ni kazi ya Serikali na kweli itakuwa kazi ya serikali miaka nenda.
 
Kumbe kukaa kimya kwa ccm ndo kulikoifanya cdm kuonekana ina nguvu mara ccm ilipoanza kujibu mapigo cdm imeanzakusinyaa kwa kasi na kitendo cha kukimbiwa na wanachama wake kila kona ya nchi ni dhahiri kwamba haina muda mrefu.na tabia ya cdm ya kutopenda kukosolewa ni janga ambalo litaangamiza chama bila kusahau ukabila ambao ni donda ndugu
 
Pole sana kwa uelewa mbovu, maandamano unafikiri nitija au mahamasisho ya umwagaji damu kama mganga wenu alivyo aambia, Mkiona nchi imetulia kwa maendeleo mnafikilia maandamano ni kwa nini msitumie mikutano kuelimisha wananchi ili waelewe kwanza pindi wanapoandamana hata mtu akiumia anajua ameumia kwa jambo la kutoka moyoni mwake?. Tofauti na ilivyo sasa Maandamano yanakuwepo kwa sababu ya watu wachache kutafuta sifa. Kaa chini fikilia je ni kweli maandamano yanatatua matatizo yetu?. Zitto alisema anawataja watu walioficha pesa USWISS lakini hadi leo kimya. Mimi nafikiri kazi si kuwataja tu bali hata kuwashitaki pia, au yeye si mtanzania? Hatuwezi kuumia kwa maneno tunatakiwa tutende sasa.
Mkuu hujaeleweka bado mbona nilipogusia maandamano umekuja juu unastuka nini kama maandamano hayana tija???? CCM na viongozi wake ndio walificha fedha zetu Uswiss na kwingineko, wao kama serikali ni wajibu wao kufanya upelelezi na kuwakamata wezi au kukamatana, lakini unfortunately boss wetu anasema mwizi akirudisha fedha kama ilivyo kuwa EPA eti asamehewe!!! Kwa hapo uwezekano wa kutendea haki Watanzania waliodhurumiwa hakuna, ndio maana nasema tutahamasishana hata kama hampendi tuandamane kama Misri hadi haki itendeke, wezi woote wakamatwe na kuwekwa lupango, uongozi unaoficha wezi uondolewe madarakani!!!( Lets call a spade a spade not a folk) Mkuu upo hapo????
 
Mbona unajadili vitu vya kipumbavu! kwani watu kwenda kwenye mkutano ni kutatua matatizo ya msingi? watu wakienda kwenye mikutano ya ccm ufisadi wa viongozi wa ccm utaisha? umaskini utaisha? huduma za afya zitaimarika? shule za kata zitaboreka? mfumko wa bei utashuka? Tafadhari usitupotezee muda wetu na propaganda za kipumbavu! mwambie Nape na wapumbavu wenzako hatuna muda wa kuchezea!
Kumbe na wewe bado umelala hujui kukutana na watu faida yake huwa ni kubwa sana kuliko kila kukicha kujiamlia tu? Mfano; Wewe kwa kuwa unaitwa baba wa familia kila kukicha unatoa amri tu kwenye familia yako, unafikiri maendeleo yatakuwepo? Kama yatakuwepo ni mfu siku ndoka tu yanaisha. Ndivyo Chadema wanavyojilea, siku Slaa akiondoka tu wanaanza kuhaha tete. Ugonjwa huu utafutiwe dawa
 
Daftari la wapiga kura lipo ila wafuasi waliowengi wa Chadema ni wa maandamano labda na kujiandikisha maandamano yaitishwe. Ili kukusanya wapigadebe, wavuta bangi na wengineo wengi na wala si hivyo tu, Hata siku ya kupiga kura maandamano yaitiswe pia. Dawa kuelimisha wananchi kwa ruzuku inayotolewa kwanza na kama mnasema ni kazi ya Serikali na kweli itakuwa kazi ya serikali miaka nenda.
Mkuu hao wapiga debe na wavuta bangi ni nyinyi mliowatengeneza na sekondari zenu za kata mkawaacha bila ajira za maana, safari hii ni wengi saana kwa taarifa yako labda mtafute mbinu nyingine lakini hilo mnalo na manjua ukweli!!! Kuandamana kisiasa ni kudai haki kama hamtendi haki tutaandamana mtauwa wengi lakini The Hague inawangoja mifano mingi mnayo, mmeisha anza kushtuka, si ni kweli????

Back
Top Bottom